Profesa Longinus Rutasitara. Picha kwa hisani ya Mchuzi blog
Kwa ufupi
- Profesa Rutasitara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dk Nyamajeje Weggoro ambaye muda wake umemalizika.
Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).
Profesa Rutasitara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dk Nyamajeje Weggoro ambaye muda wake umemalizika.
Kwa mujibu wa Sheria TCAA ya mwaka 1977, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka hiyo huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo Mwenyekiti akitoka Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti hutoka Tanzania Zanzibar na kinyume chake.