NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

UN yapongeza uchaguzi Tanzania

Written By CCMdijitali on Saturday, October 31, 2015 | October 31, 2015


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Kimoon, ametuma salamu za pongezi kwa Watanzania, Serikali na vyama vya siasa, kwa namna walivyoshirikiana katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu na kumpata Rais Mteule wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli.

Taarifa ya Ki-moon iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari, imeeleza kuwa Katibu Mkuu huyo amepongeza namna uchaguzi huo ulivyofanyika katika utaratibu mzuri na kwa amani na uwajibikaji mzuri walioonesha Watanzania. Akifafanua uwajibikaji huo, Kimoon amesema hatua ya Watanzania ya kupiga kura na kusubiri matokeo ya uchaguzi huo kwa amani, ni uthibitisho thabiti wa dhamira yao ya kujenga mfumo wa kidemokrasia, kulinda amani na ustahimilivu.

Salam za Odinga Mbali na Ki-moon, salamu zingine za pongezi zimetoka kwa Kiongozi wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) cha nchini Kenya, Waziri Mkuu mstaafu wa nchi hiyo jirani, Raila Odinga kwenda kwa Watanzania na kipekee kwa Dk Magufuli, ambaye ni rafiki yake wa karibu. Katika salamu zake, Odinga ambaye ni Kiongozi wa Upinzani nchini humo, amesema Watanzania wengi wamemchagua Dk Magufuli kuongoza nchi yao na kusimamia hatma yao kwa miaka mitano ijayo kutokana na uwezo na uadilifu wake.

“Tafadhali pokea pongezi zangu za dhati, kwa niaba yangu na kwa niaba ya ODM na Wakenya. Naipongeza CCM kwa ushindi mkubwa na muungano wa vyama vya upinzani, kwa mapambano mazuri. “Ushindi wako ni matokeo ya kujitoa kwako bila kuchoka katika kutumikia nchi yako na chama chako. Pia ni mafanikio makubwa ya kampeni zako za kipekee,” amesema Odinga katika salamu hizo.

Amesema ukubwa na ubora wa kampeni za Dk Magufuli, umedhihirisha kukomaa na ubora wa demokrasia ya Tanzania na kuongeza kuwa, Dk Magufuli anaingia madarakani, wakati kukiwa na matarajio makubwa ya Watanzania kwake na kutoka kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. “Nakushauri uweke kipaumbele katika kudumisha umoja na ustahimilivu wa Watanzania na kuendeleza na kuongeza nguvu katika ushirikiano wa Afrika Mashariki na demokrasia ndani ya Bara la Afrika.

“Sisi Wakenya siku zote tumekuwa pamoja na Watanzania kwa historia, desturi na urafiki na ni matumaini yangu kuwa tunu hii ya kihistoria, itaimarisha ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, chini ya uongozi wako,” amesema Odinga katika salamu hizo. Waangalizi waridhika Pongezi zingine zimetoka kwa Kiongozi wa Waangalizi wa Kimataifa kutoka Jumuiya ya Madola, Rais mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan, ambaye amesema mchakato wa Uchaguzi Mkuu umekuwa wa haki.

Kauli hiyo ya Jonathan ni sehemu ya mfululizo wa matamko ya waangalizi wa kimataifa yaliyoonesha kuridhika na mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu uliomalizika Jumapili iliyopita kwa Watanzania kupiga kura na kuhitimishwa jana kwa Dk Magufuli kukabidhiwa cheti na NEC, kuthibitisha ushindi wake.

Wengine waliokwishatoa tamko, ni waangalizi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), waliosema uchaguzi wa Tanzania kwa kiasi kikubwa umeendeshwa vizuri, ingawa kumekuwa na kasoro chache zilizosababisha baadhi ya wanasiasa kutilia shaka uhuru wa tume za uchaguzi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Zanzibar.

Mwangalizi Mkuu wa Umoja huo wa Ulaya, Judith Sargentini, alisema waangalizi wa umoja huo waliofikia 141 waliotembelea vituo 625 vya upigaji wa kura, wataendelea kusalia nchini hadi Novemba 15 wakijihusisha na majukumu kadhaa ikiwamo kukutana na vyama vya siasa, maofisa wa uchaguzi wa asasi za kiraia. 

Waangalizi wengine kutoka nchi za Maziwa Makuu, nao walisema wameridhishwa na kutosheka na hali ya utulivu na kukomaa kwa demokrasia nchini, wakati wote wa kampeni licha ya kuwepo na tofauti za kisera.

Mkuu wa msafara wa waangalizi hao kutoka Wizara ya Mambo ya Nje nchini Kenya, Balozi Zachary Mumbuli, alisema lazima Watanzania wahakikishe wanapiga kura baada ya kumaliza kampeni kwa utulivu.

Alisema katika uangalizi wao, wameridhika kuwa maandalizi pia yako vizuri na nchi hizo 12 zinazounda Jumuiya ya Maziwa Makuu (ICGLR), wamepata mengi ya kujifunza hasa kufanyika kwa kampeni kwa utulivu licha ya tofauti za kisiasa. Balozi Mumbuli aliwasihi Watanzania kuendelea kukaa kwa utulivu na amani, kwani uchaguzi ni suala la muda hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha nchi inabaki kuwa kielelezo kwa nchi nyingine.

Alisema baada ya kuangalia mchakato mzima wa uchaguzi, wametosheka na hali ilivyo na kusisitiza kwamba kila mwananchi ahakikishe anakuwa mlinzi wa usalama wa kisiasa wa nchi, kwa kuwa bila usalama huo, ni dhahiri hakutakuwa na biashara na uchumi wa nchi na kila mmoja utaathirika. Akitambulisha wajumbe wa kundi hilo la waangalizi, Balozi Mumbuli alisema miongoni mwao, kuna viongozi wa vijana kutoka nchi za Maziwa Makuu, ambao waliokuja kuangalia mchakato wa Uchaguzi Mkuu unavyoendelea nchini, jambo ambalo limekuwa likifanyika kwa nchi zote wanachama wanapokuwa na uchaguzi.

Alisema jukumu kubwa ni kuendeleza jamii kwa kuwaunganisha vijana, akinamama na wafanyabiashara kwa kuhusisha sera za kisiasa na maendeleo ya makundi hayo, ili kustawisha nchi kwani biashara pasipo na usalama ni vigumu. *Uchaguzi wa Zanzibar Pamoja na kuridhika na Uchaguzi Mkuu, waangalizi hao na Umoja wa Mataifa, walitoa angalizo lao kuhusu kufutwa kwa Uchaguzi wa Zanzibar, kulikosababishwa na hitilafu ikiwemo ya kura kuzidi idadi ya wapigakura katika vituo vya kupigia kura.

Katibu Mkuu wa UN, Ki-moon katika taarifa yake, ametaka hitilafu yoyote iliyojitokeza katika mchakato wa uchaguzi wa Zanzibar, ufanyiwe kazi kwa kufuata sheria zilizopo kwa amani na kwa uwazi. “Katibu Mkuu amewataka wadau wote wa uchaguzi wa Zanzibar kuwa watulivu, waepuke ushawishi wowote wa kufanya vurugu na kujizuia kutoa matamko yoyote yanayoweza kuzidisha sintofahamu,” ameeleza Katibu Mkuu huyo wa UN. Rais mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan, alitaka suala la Zanzibar litatuliwe mapema na kwa amani ili kuepusha vurugu za kisiasa zinazoweza kujitokeza.

Raila Odinga ampongeza Dkt Magufuli, amshauri Lowassa aende mahakamani kama hajaridhika

Written By CCMdijitali on Friday, October 30, 2015 | October 30, 2015


Waziri Mkuu wa zamani Kenya Raila Odinga amempongeza Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada yake kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Urais Tanzania.

Akiongea katika mahojiano na BBC, Mhe Odinga amemshauri mgombea wa upinzani Mhe. Edward Lowassa Kuwa Kama Hajakubaliana na Matokeo basi Aende Mahakama kushtaki Kama yeye Alivyofanya wakati akigombea Urais Kenya na kushindwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Ameeleza pia matumaini yake kwamba Dkt. Magufuli atahakikisha kuendelea kwa uhusiano mzuri uliopo katia ya Tanzania na Kenya, na kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuendeleza ndoto ya kuelekea kwenye Shirikisho la nchi hizo.

Judge Lubuva presents the winning certificate to Dr John Pombe Magufuli


  NEC Chairman Judge Lubuva presenting the winning certificate to Dr John Pombe Magufuli president elect.


 Magazetini leo.

NDEREMO NA VIFIJO VYATAWALA JIJINI ARUSHA

Written By CCMdijitali on Thursday, October 29, 2015 | October 29, 2015

Jiji  lazizima , mara baada ya matokeo ya Urais wa Jamhuri ya Tanzania kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kusababisha baadhi ya shughuli kwenye  Mitaa ya :
  • Idara ya Maji
  • Bondeni
  • Pangani 
  • Barabara ya Fire
  • Barabara ya Friends Corner kuelekea Samunge
kusimama kwa muda.
#Hapa Kazi Tu..... 
Hakuna Mchezo.... baadhi ya Mashabiki na Wakereketwa wakigufulika.......











#Hapa Kazi Tu.............




Chipukizi wa CCM Bi Asha Mfaume akifurahia ushindi wa Chama Cha Mapinduzi,katika Mtaa wa Bondeni leo (aliyeshika picha ya Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli)mara baada ya kutangazwa rasmi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi . 



 #Hapa Kazi Tu.......  
Katibu wa UVCCM Kata ya Sokon I ,Ndg Charles Kagoza ,akishindwa kuficha hisia zake........    


 Furaha na nderemo kila kona katika Jiji la Arusha leo.
Katibu wa UVCCM Kata ya Sokon I ,Ndg Charles Kagoza ,akishindwa kuficha hisia zake........  
Hapa Kazi Tu........
 Kada wa CCM na familia yake Ndg Hussein Maslahi  ,wakisherehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli ,mara baada ya Tume ya Uchaguzi ,kutangaza rasmi matokeo hayo leo.


 Umati wa Wanachama wa CCM kutoka baadhi ya Kata za Unga Ltd, Daraja II ,Sokon I, Ngarenaro na Kati ,wakishrehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli katika barabara ya Mtaa wa Bondeni Kata ya Kati  kuelekea barabara ya Stadium ,mara baada ya Tume ya Uchaguzi ,kutangaza rasmi matokeo hayo leo.





  Umati wa Wanachama wa CCM kutoka baadhi ya Kata za Unga Ltd, Daraja II ,Sokon I, Ngarenaro na Kati ,wakishrehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli katika barabara ya Idara ya Maji kuelekea barabara ya Sokoine ,mara baada ya Tume ya Uchaguzi ,kutangaza rasmi matokeo hayo leo.

 Kada maarufu Jijini na Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Sokon I Ndg Masalu,akipiga push up katikati ya barabara,baada ya kulitelekeza gari lake na abiria wakiwemo ndani ,kusherehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli ,mara baada ya Tume ya Uchaguzi ,kutangaza rasmi matokeo hayo leo.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munissi ,aliyeshika bango ,akisherehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli ,mara baada ya Tume ya Uchaguzi ,kutangaza rasmi matokeo hayo leo.
 Wanachama wa CCM kutoka baadhi ya Kata za Unga Ltd, Daraja II ,Sokon I, Ngarenaro na Kati ,wakishrehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli katika barabara ya Friends kuelekea Samunge ,mara baada ya Tume ya Uchaguzi ,kutangaza rasmi matokeo hayo leo.
 Vijana nao hawakuwa nyuma kuonyesha furaha yao, wakiwa na picha ya Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, katika maandamano yalifanyika kuzunguka baadhi ya barabara za Jiji la Arusha leo.
 Maeneo ya Mtaa wa Pangani ,nyumbani kwa Diwani wa CCM ndg A. Tojo
 Wanachama wa CCM kutoka baadhi ya Kata za Unga Ltd, Daraja II ,Sokon I, Ngarenaro na Kati ,wakishrehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli ,mara baada ya Tume ya Uchaguzi ,kutangaza rasmi matokeo hayo leo.
 Wanachama wa CCM Kata ya Kati ,wakishrehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli nyumbani kwa Diwani wa CCM Kata ya Kati Ndg Abdul Tojo.
Wanachama wa CCM  Kata ya Kati ,wakishrehekea ushindi wa Dr J.P.Magufuli nyumbani kwa Diwani wa CCM Kata ya Kati Ndg Abdul Tojo.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha - Ndg Jasper Kishumbua


MATOKEO RASMI MAJIMBO 10

Written By CCMdijitali on Tuesday, October 27, 2015 | October 27, 2015























 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link