NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

SERIKALI YAWEKA MPANGO MKAKATI MAALUM WA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA MALARIA NCHINI

Written By CCMdijitali on Monday, April 25, 2022 | April 25, 2022

 SERIKALI YAWEKA MPANGO MKAKATI 

MAALUM WA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI 

YA MALARIA NCHINI













Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI imeweka mpango mkakati maalum wa miaka mitano kuanzia 2021-2025 unaolenga kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria.


Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambayo yameadhimishwa kitaifa jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema mpango Mkakati huo unalenga kupunguza kiwango cha maambukizi ya Malaria nchini kutoka wastani wa asilimia 7.5 ya mwaka 2017 hadi kufikia wastani wa chini ya asilimia 3.5 ifikapo mwaka 2025.

“Mpango huu una mikakati mikuu mitatu ambayo ni udhibiti wa mbu waenezao Malaria, uchunguzi, tiba na tibakinga ya Malaria kwa makundi maalum; na ufuatiliaji na tathmini ya mwenendo wa ugonjwa wa Malaria hapa nchini”. Amesema Waziri Ummy.


Waziri Ummy amesema katika kipindi cha mwaka 2021 jumla ya vyandarua milioni 7.5 vyenye dawa vimegawiwa kwa wananchi kupitia kliniki za wajawazito na watoto, shule za msingi za Umma na kupitia kampeni maalum ya usambazaji na ugawaji wa vyandarua katika kaya.

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa zaidi ya nyumba 568,000 zimepuliziwa viuatilifu ukoko kwenye kuta ndani ya nyumba na hivyo kuwakinga zaidi ya watu milioni 2 dhidi ya maambukizi ya Malaria katika Halmashauri za Kakonko, Kasulu na Kibondo pamoja na Kambi za wakimbizi za Nduta, Mtendeli na Nyarugusu kwa Mkoa wa Kigoma; Halmashauri ya Biharamulo kwa Mkoa wa Kagera; Halmashauri ya Ukerewe kwa Mkoa wa Mwanza na Halmashauri ya Bukombe kwa Mkoa wa Geita.

Waziri Ummy ameongeza kuwa Serikali imeendelea kununua na kusambaza vitendanishi na dawa za kutosha za kutibu Malaria katika vituo vya kutolea huduma za afya, ambapo vipimo na matibabu ya Malaria yanatolewa kwa wananchi bila malipo na upatikanaji wake ni asilimia 98.

Kwa upande wa upatikanaji wa dawa, Waziri Ummy amesema Serikali imekua ikifuatilia ubora na usalama wa dawa za Malaria na kujiridhisha kuwa ni salama na zina uwezo wa kutibu kwa zaidi ya asilimia 96.

Waziri Ummy amesema Serikali imeendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kutekeleza afua mbalimbali za Malaria ambapo

KINANA ATEMA CHECHE ZIARANI MKOA WA PWANI

Written By CCMdijitali on Sunday, April 24, 2022 | April 24, 2022

 

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akifungua kitambaa ishara ya kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tabi la CCM Mwanambaya Wapili kulis bi Amina Ndomboroke Mwenyekiti wa Shina hilo.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akipanda mti  mara baada ya  kuweka jiwe la Msingi katika Ofisi ya CCM Tabi CCM Mwanambaya

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi mbalimbali alipowasili katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Mkuranga katika Ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na WanaCCM Pamoja na Viongozi  Mkoani Pwani


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana , Akifurahi pamoja na kikundi Cha Hamasa na Itifaki Wilayani Mkuranga  alipowasili katika Ziara yake ya kujitambulisha na kuzungumza na WanaCCM Pamoja na Viongozi  Mkoani Pwani

 


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Abdulrahman Kinana, akizungumza na Mwenyekiti wa CCM Mio wa Pwani, Ramadhani Maneno baada ya kuwasili patika ofisi za CCM Wilaya ya Mkuranga.

Makamu Mwenyekiti wa wa CCM Tanzania Bara, Ndg Abdulrahman Kinana akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Ramadhani Maneno wakiwa katika kutano wa ndani wa Chama wilayani Mkuranga.


 

Viongozi mbalimbali na wanachama wa CCM wakisimama kumpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM alipowasii katika ukumbi wa mkutano kwa ajili ya mkutano wa ndani wa Chama wilayani Mkranga.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, akizungumza na wana CCM katika mkutano wa ndani alipofanya ziara ya kujitambulisha mkoani Pwani. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mkuranga


 

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka akizungumza na wana CCM katika mkutano wa ndani alipofanya ziara ya kujitambulisha mkoani Pwani. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mkuranga


Viongozi mbalimbali katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mkuranga katika Ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania -Bara Ndg Abdulrahman Kinana kujitambulisha na kuzungumza na WanaCCM Pamoja na Viongozi Mkoani Pwani



Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana amepokelewa wilaya ya Mkuranga leo tarehe 24 Aprili, 2022 kwa ajili ya ziara mkoa wa Pwani ya uimarishaji uhai wa chama na kuhamasisha wana-CCM kujitokeza kushiriki uchaguzi wa ndani ya Chama unaoendelea.

Akizungumza na wanachama wa CCM ukumbi wa CCM wilaya ya Mkuranga Ndugu Kinana amewataka wana-CCM kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za uongozi ndani ya Chama katika uchaguzi unaoendelea pamoja na kuwahimiza viongozi wa ngazi zote kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa huru, haki na wenye kuzingatia katiba ya CCM na kanuni zake ili kuwapata viongozi waadilifu.

"Viongozi simamieni uchaguzi uwe huru na haki, acheni kubeba wagombea, epukeni dhulma na chukueni hatua kwa kuwakata wale wanaotafuta uongozi au umaarufu kwa fedha. Kwa kuwa tunataka uadilifu nje ya CCM basi ni lazima tuanze kwanza sisi kuwa waadilifu." Amesema Kinana

Kinana amesisitiza "Wana-CCM wanayo haki ya kuchagua na kuchaguliwa lakini haipo haki ya kununua au kununuliwa ili kupata au kutoa uongozi.  Kuna watu huwa hawana habari na chama wala wanachama wakati ambao sio wa chaguzi ajabu wakisikia uchaguzi tu wanaanza kujipitisha kuwasalimu, kugawa fedha na kuwachafua wengine tusiruhusu haya yajitokeze."

Aidha Kinana amesema mahusiano mazuri baina ya CCM na serikali ni chachu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM hali inayoimarisha imani ya wananchi kwa Chama na serikali yao. Pia amewataka viongozi wa CCM kuendeleza utamaduni wa kuwasikiliza wananchi na kuwasilisha changamoto zao serikalini kwa utatuzi. Amehimiza wajibu huo ni walazima kwa sababu ni CCM inayoomba kura na inayopigiwa kura.

Mapema wakati wa Mapokezi Ndg Kinana ameshiriki uzinduzi wa ofisi ya tawi la Mwanambaya kata ya Mipeko wilaya ya Mkuranga ambapo alichangia shilingi milioni tatu kuunga mkono juhudi za Wana-CCM na viongozi wa tawi hilo za kupata mazingira mazuri ya kufanyia shughuli za Chama. 

Katika ziara hii viongozi walioshiriki ni pamoja na mwenyeji wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndg Ramadhani Maneno, Kamati ya siasa ya mkoa wa Pwani, kamati za siasa za wilaya zote za Mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Ndg Abubakar Kunenge, wakuu wa wilaya zote, watendaji wote, wabunge na madiwani wote wa Mkoa wa Pwani. Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Ndg Abdulrahman Omar Kinana ameondoka mkoa wa Pwani kuelekea mkoa wa Tanga kuendelea na ziara yake akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka.

 




 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link