MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post
Showing posts with label MIKOANI. Show all posts
Showing posts with label MIKOANI. Show all posts

WANANCHI MAGU WAISHUKURU SERIKALI KUWAPATIA HATI ZA HAKIMILKI ZA KIMILA

Written By CCMdijitali on Saturday, September 27, 2025 | September 27, 2025



Na Munir Shemweta, WANMM MAGU 

 

Wananchi wa vijiji vitatu vya Chandulu, Salama, Mwabulenga vilivyopo kata ya Ng'haya wilaya ya Magu mkoa wa Mwanza wameishukuru serikali kwa uamuzi wake wa kuwapimia na kuwamilikisha maeneo yao kwa kuwapatia Hati za Hakimilki za Kimila.

 

Zoezi hilo la kuwapatia Hati za Hakimilki za Kimila limefanyika baada ya kufanyika mipango wa matumizi ya ardhi pamoja na upimaji ardhi katika vijiji hivyo vitatu.

 

Mipango ya Matumizi ya Ardhi huwekwa katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuboresha usalama wa umiliki wa ardhi, kukuza matumizi endelevu ya ardhi pamoja na kupunguza migogoro ya ardhi.

 

Wananchi wa vijiji hivyo wametoa kauli hiyo tarehe 26 Septemba 2025 katika kijiji cha Chandulu wilayani Magu wakati wa zoezi la kutoa hakimilki za kimila kwa wananchi waliomilikishwa maeneo yao.

 

Jumla ya Hati za Hakimilki za Kimila 1,415 zimeandaliwa huku takriban hatimilki 5000 ukamilishaji wake ukiendelea ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga alikabidhi Hati za Hakimilki za kimila 50 kwa niaba ya wannachi wote waliomilikishwa.

 

Wananchi hao wamesema, wanajisikia furaha kubwa kumilikishwa maeneo yao waliyoyaelezea kuwa sasa umilikishaji wake umeongeza thamani ya maeneo hayo.

 

"Najisikia vizuri sana kwa sababu ardhi yangu nimemilikishwa kwa hati na sitokuwa tena na uharaka wa kuiuza, niipongeze sana serikali kwa uamuzi wake huu wa kutumilikisha" amesema mkazi wa Chadulu Bw. Mashiku Machunge.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amewataka wananchi waliokabidhiwa Hati za Hakimilki za kimila kuhakikisha wanazitunza na kuacha tabia ya kuuza ardhi hovyo ili ziweze kusaidia vizazi vijavyo.

 

"Ndugu wananchi hati hizi inatakiwa mzitunze kwa sababu huu ni urithi wenu, ardhi hii ni ya kwenu mzitunze na pili tusiwe na tabia ya kuuza ardhi, ardhi tuitunze itusiadie sisi, watoto wetu, wajukuu zetu na watakaotufutia katika vizazi vyetu" amesema.

 

Ametaka hati milki walizokabidhiwa wananchi zilete mabadiliko ya kimaisha kwa kuwa mbali na kuwatambulisha kisheria lakini zinasaidia kupata mikopo na kueleza matarajio ya serikali ni kwamba pawepo matokeo chanya ya kimaendeleo na kusisitiza kuwa hati hizo zisiwe sehemu ya migogoro ya kudhulumiana.

 

Kwa upande wake Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Mwanza Bw. Wilson Luge ameeleza msingi mkubwa wa ofisi yake ni kuhakikisha wanawamilikisha wananchi maeneo yao kwa kuwapatia hati milki kwa kuwa ardhi ni rasimali itakayowawezesha kiuchumi.

 

"Ndani ya mkoa wa Mwanza katika halmashauri zote sita tutashirikiana na kampuni za upimaji kuhakikisha ardhi za wananchi wetu zinapimwa na kuwapatia hati zikiwemo hizi Hati za Hakimilki za kimila bila kuwacheleweshea" amesema Luge.

 

Zoezi la upimaji maeneo katika wilaya ya Magu limefanywa kwa ushirikiano na kampuni za upimaji za GMS Geo tech Consultancy Co.Ltd, GNT Property Ltd na CAIWAY Company Ltd ambazo zinatekeleza mazoezi katika vijiji 16 kati ya vijiji 82 vilivyoko ndani ya Wilaya ya Magu.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

DAY [3] WABUNGE WA JIMBO LA ARUSHA KATA YA OLASITI

Written By CCMdijitali on Monday, August 4, 2025 | August 04, 2025

 Mkutano wa  kujitambulisha Wagombea Ubunge na Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha, Kata ya OLASITI

 MKOA WA ARUSHA

Jimbo la Arusha Mjini


(1) Ndugu Ally Said BABU
(2) Ndugu Hussein Omarhajji GONGA
(3) Ndugu Aminatha Salash TOURE
(4) Ndugu Mustapha Said NASSORO
(5) Ndugu Paul Christian MAKONDA
(6) Ndugu Lwembo Mkwavi MGHWENO
(7) Ndugu Jasper Augustino KISHUMBUA


📆 August 31, 2025

📍OLASITI, ARUSHA



PICHA YA WABUNGE WATEULIWA


Ndg Hussein Gonga akijitambulisha mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Olasiti.

Ndg Hussein Gonga akijitambulisha mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Olasiti.


















Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Olasiti.



Cde Makonda akijitambulisha mbele ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Kata ya Olasiti.














UTANI WA JADI SIMBA NA YANGA WAPAMBA UZINDUZI WA HARAMBEE UJENZI KKKT DODOMA

Written By CCMdijitali on Saturday, July 26, 2025 | July 26, 2025



Utani wa jadi wa Klabu za Yanga na Simba umepamba uzinduzi wa Harambee ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi Kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Dodoma iliyofanyika katika eneo la Mradi la Nzuguni C, Jijini Dodoma, ambapo upande wa Wananchi (Yanga) uliongizwa na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, wakati upande wa Ubaya Ubwela (Simba) ulisimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweli.

Matukio mawili yaliyosisimua waumini na wageni waalikwa walioshiriki Harambee hiyo ni mnada wa mbuzi ambapo mbuzi wawili, mwenye rangi nyeusi akiwakilisha upande wa Yanga alinadiwa kwa shilingi milioni 31 na mbuzi mweupe (Simba) aliuzwa kwa bei kama hiyo ya shilingi milioni 31 na kufanya mbuzi hao wawili kunadiwa kwa jumla ya shilingi 61m.

Kama utani huo haukutosha, viliwekwa vikapu viwili bya sadaka ambapo waumini wanaoshabikia Yanga na Simba walipambanishwa na waumini mashabiki wa Yanga waliibuka kidedea kwa kuchangia shilingi 1,800,000 na Wekundu wa Msimbazi Simba walichangia shilingi 1,210,700.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link