NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

KILUPI-AKABIDHIWA OFISI, ASEMA HAKUNA WA KUZUIA USHINDI WA CCM.

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 31, 2023 | January 31, 2023

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

KATIBU mpya wa Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Ndg.Omar Ibrahim Kilupi,amesema chini ya uongozi wake hakuna Chama chochote cha kisiasa kitakachozuia ushindi wa CCM  mwaka 2025.

Msimamo huo ameutoa leo wakati akikabidhiwa ofisi ya idara hiyo Kisiwandui na aliyekuwa Katibu wa Idara ya Organazesheni Ndg. Galos Cassian Nyimbo huko Kisiwandui Zanzibar.

Kilupi alisema Chama hicho kina tiketi ya kudumu ya kuongoza dola kutoka kwa wananchi wanaokiamini na kukipenda kutokana na usimamizi mzuri wa Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2022.

Alifafanua kwamba CCM ni Chama mwalimu na kiongozi wa vyama vingine vya kisiasa kwani imejiwekea mfumo imara wa kiuongozi na utendaji kuanzia ngazi ya shina hadi taifa.

Alisema kwamba CCM kupitia ibara ya 5 ya Katiba yake imeweka wazi dhamira yake ya kushinda bila vikwazo kwa kila uchaguzi wa dola.

Alisema idara hiyo inahusika moja kwa moja ma masuala yote ya uchaguzi hivyo jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025.

“ Nachukua nafasi hii kwanza kukishukru Chama Cha Mapinduzi kilichoamua kunipa dhamana hii kubwa, naahidi kutumia uwezo wangu wote kuhakikisha kinashinda kwa asilimia kubwa katika uchaguzi wowote utakaotokea kuanzia hivi sasa.
Pia ofisi yangu ipo wazi muda wote nipo tayari kushiriana na wanachama,viongozi na watendaji wote wa CCM na wale wenye mawazo na fikra za kujenga chama chetu.”, alisema Kilupi.

Aidha Kilupi aliahidi kutekeleza majukumu yake kwa uadili,ueledi na ubunifu ili kwenda sambamba na malengo ya Chama Cha Mapinduzi.

Katika maelezo yake Katibu huyo, amewataka maofisa wa idara hiyo kuwajibika katika majukumu yao ya kikazi.

Alisema kama dhamira ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) kinavyotaka ni kufanya kazi kwa ushirikiano na umoja na ndiye na yeye anavyotaka maofisa hao wa idara kuzingatia hilo.

"Kila mtu awajibike kwenye kwenye nafasi yake na ninachoamini ni kuwa tukifanya kazi kwa pamoja tutafanikiwa na hatutoweza kushindwa kufikia dhamira ya CCM ya kuhakikisha ushindi wa chama kila uchaguzi,"alisema

"Ninashukuru kwa mapokezi yenu pia ninampongeza Katibu aliyepita Galos kwa kazi nzuri yenye uadilifu hivyo anastahili pongezi kubwa,"alisema

Alisema kama ilivyokawaida na desturi ya chama ni kukabidhiana vijiti vya uongozi na kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Kupitia hafla hiyo ya makabidhiano Ndgu.Kilupi, aliwapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kasi yao kubwa ya kutatua changamoto za wananchi na kuwaletea maendeleo endelevu.

Naye Katibu mstaafu wa Idara hiyo Ndg. Casian Galos Nyimbo, amesema idara hiyo ndio chombo mahsusi cha kufanikisha masuala yote ya uchaguzi wa Chama hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa juhudi kubwa.

Pamoja na hayo aliwataka watumishi katika idara hiyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa kiongozi mpya aliyekabidhiwa ofisi ili wafikie kwa haraka malengo endelevu ya Chama Cha Mapinduzi.

KATIBU Mstaafu wa Kamati Maalum ya NEC, Idaraya Organaizesheni CCM Zanzibar Ndg. Casian Gallos Nyimbo (kushoto), akimkabidhi nyaraka za kiutendaji Katibu mpya wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organazesheni Ndg.Omar Ibrahim Kilupi, huku Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui leo Tarehe 31/01/2023.

KATIBU Mstaafu wa Kamati Maalum ya NEC,Idaraya Organaizesheni CCM Zanzibar Ndg. Casian Gallos Nyimbo(kushoto),akimkabidhi nyaraka za kiutendaji Katibu mpya wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni Ndg.Omar Ibrahim Kilupi, huku Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui leo Tarehe 31/01/2023.

WAZIRI MABULA AWEKA WAZI MAFANIKIO NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA SEKTA YA ARDHI NCHINI

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 3, 2023 | January 03, 2023

Na Munir Shemweta, WANMM

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameridhia ardhi yenye ukubwa wa ekari 1,492,703 iliyokuwa sehemu ya maeneo ya hifadhi na maeneo ya umma zikiwemo Ranchi za Serikali kumegwa na kurasimishwa kwa wananchi.

Aidha, Mapori Tengefu 12 yenye ukubwa ekari 707,962 na Hifadhi za Misitu Misitu 7 zenye ekari 46,715 nayo imefutwa na ardhi hiyo kukabidhiwa kwa wananchi kupitia usimamizi wa Serikali za Mikoa katika kupanga na kuyapima maeneo hayo.

Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. DKt Angeline Mabula wakati akizungumzia masuala mbalimbali ya sekta ya ardhi na muelekeo wa utekezaji wa Wizara hiyo kwa kipindi cha kuanzia  januari 2023.

"Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta imeielekeza Mikoa kusimamia utekelezaji wa uamuzi wa Serikali kwenye maeneo yao yote yalioainishwa na kutolewa uamuzi" alisema Dkt. Mabula. 

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mongoni mwa kazi zinazondelea kutekelezwa hivi sasa ni pamoja na uwekaji wa alama za mipaka baina ya maeneo ya hifadhi na maeneo ambayo Serikali imeridhia yabaki kwa wananchi, upangaji na upimaji wa maeneo yaliyorejeshwa kwa wananchi, utambuzi, uhakiki na uthamini wa maeneo ambayo wananchi watatakiwa kupisha shughuli au maeneo yatakayotumika kwa matumizi ya umma na uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi.

Amechukua fursa kupitia mkutano na vyombo vya habari kuomba kila Mkoa kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Serikali na kuhakikisha kazi zote zinakamilishwa ifikapo tarehe 30 Machi, 2023. 

Akizungumzia ulipaji kodi ya pango la ardhi hasa baada ya msamaha wa riba ya malimbikizo ya pango la ardhi uliotolewa na Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ambapo wananchi wenye malimbikizo walipewa nafuu ya kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo.  Waziri wa Ardhi alieleza kuwa, Kutokana na nafuu uliotolewa  Wizara yake imeweza kukusanya jumla ya shs 90,907,939,421 sawa na asilimia 75 ya lengo la nusu mwaka. 

Hadi kufikia Novemba, 2022 wananchi 2,819 wamenufaika na msamaha wa riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi yenye jumla ya TZS 6,946,930,272. Idadi hiyo haijumuishi wananchi waliojitokeza ambao wamehudumiwa kuanzia tarehe 1 – 31 hadi Disemba 31, 2022. 

Amewashukuru na kuwapongeza wamiliki wa ardhi waliojitokeza kunufaika na msamaha uliotolewa na Mhe. Rais na kubainisha kuwa, katika mwezi Disemba, 2022 Wizara ya Ardhi imeshuhudia idadi kubwa ya wamiliki waliojitokeza kulipa na kiasi cha bilioni 22.6 kimekusanywa katika mwezi Disemba pekee. 

Akigeukia suala la utatuzi wa migogoro ya ardhi, Dkt Mabula amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia kikamilifu mipango ya jumla, mipango kina na mipango ya matumizi ya ardhi vijijini kupitia kamati za ardhi za Vijiji ili kudhibiti ujenzi holela usiozingatia mipango iliyoandaliwa na kuidhinishwa kupitia Kamati za Mipangomiji. 

"wizara imekuwa ikipokea taarifa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu ukiukwaji wa taratibu mbalimbali zinazohusu Usimamizi wa Ardhi Mijini na Vijijini" alisema Dkt Mabula

Miongoni mwa malalamiko ni baadhi viongozi wa vijiji na Mitaa kuuza ardhi kinyume na utaratibu, kukosekana kwa udhibiti wa uendelezaji ardhi katika maeneo ya Vijiji na Miji. Hali hiyo imesabisha kuongezeka kwa migogoro ya ardhi na uendelezaji ardhi kinyume na mipango iliyoandaliwa na kuidhinishwa.

Dkt Mabula alisema Wizara yake inaandaa programu maalum ya kufanya ukaguzi wa uzingatiaji wa mipango ya matumizi ya ardhi kwa Mamlaka za Upangaji. Taarifa hizi zitatolewa kwa umma kama sehemu ya uwajibikaji wa mamlaka zetu kwa wananchi.

Kuhusu ujenzi wa vituo vya mafuta, Dkt Mabuka alisema hadi kufikia tarehe 31 Disemba, 2022 Wizara imepokea taarifa ya uendelezaji wa vituo vya mafuta kutoka Halmashauri 129 kati ya 184 zilizopo nchini sawa na asilimia 70.1.

Uchambuzi uliofanywa na Wizara ya Ardhi umebaini katika Halmashauri 129, kuna vituo 2,063 ambapo kati ya hivyo vituo vya mafuta ni 1269 (asilimia 61.6) na vituo vidogo vya mafuta ni 794 (asimilia 38.5) huku Vituo 1,868 vimejengwa katika umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka kituo kimoja na kingine sawa na asilimia 90.5 kama inavyoelekezwa na kanuni ya viwango vya umbali

Aidha,  Vituo 195 vimejengwa umbali wa chini ya mita 200 sawa na asilimia 9.5. Wizara inaendelea kufanya uchambuzi zaidi ili kubainisha vituo ambavyo vimejengwa kabla au baada ya kanuni za mwaka 2018 zinazoendelea kutumika ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa.

Pia Waziri wa Ardhi alizungumzia suala la program ya miaka 10 ya  urasimishaji makazi holela ambapo Wizara inayo Programu ya Urasimishaji Makazi iliyoanza kutekelezwa mwaka 2013. Programu hiyo mwisho wake ni mwaka huu 2023 na imekuwa ikitekelezwa katika Mitaa 3,397 kwenye Mikoa yote 26. 

Dkt Mabula alisema, Mitaa 1,961 imerasimishwa sawa na asilimia 57.7 na Mitaa 1,436 haijarasimishwa sawa na asilimia 42.3 na kubainisha kuwa prrogramu hiyo imewezesha upangaji wa viwanja 2,338,926 na kati ya hivyo, viwanja 1,170,638 upimaji wake umekamilika. Aidha, jumla ya milki 177,330 zimeandaliwa na kutolewa kwa wananchi.

Hata hivyo, alisema katika kutekeleza Programu hiyo, kumekuwepo na changamoto mbalimbali licha ya mafanikio yaliyopatikana na kuzitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na Uelewa mdogo wa wananchi juu ya umuhimu na namna zoezi la urasimishaji linavyofanyika, baadhi ya wananchi kutokuwa tayari kuchangia ardhi inayohitajika kwa ajili ya miundombinu na matumizi ya umma, baadhi ya wananchi kutolipa gharama za urasimishaji kwa wakati hali inayosababisha baadhi ya kampuni kushindwa kumudu gharama za utekelezaji na baadhi ya kampuni za urasimishaji kutokamilisha kazi kwa wakati pamoja na kutumia wataalam wasiokuwa na sifa.

Hata hivyo, alisema kutokana na uwepo wa changamoto hizo, Wizara imechukua hatua mbalimbali kuhakikisha kazi za urasimishaji zinakamilika na hatua hizo ni pamoja na Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri, kukwamua baadhi ya kazi zilizokwama, kuchukua hatua kwa kampuni zilizoshindwa kutimiza wajibu wao ikiwa ni pamoja na kusimamisha au kufungia baadhi ya kampuni hizo, kuhusisha taasisi za kifedha katika miradi ya urasimishaji na kuandaa na kusambaza mwongozo wa urasimishaji ikiwemo kupunguza gharama za urasimishaji hadi kufikia shilingi 130,000 kwa kiwanja.

Pamoja na jitihada hizo, Wizara ya Ardhi  kwa kushirikiana na Halmashauri na Sekta Binafsi inatekeleza programu ya Kupanga, Kupima na kumilikisha ardhi ili kuwa na miji nadhifu na iliyopangwa.

Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, Matokeo ya programu hii, yatasaidia kupunguza Mitaa isiyorasimishwa na kudhibiti kuendelea kukua kwa makazi yasiyopangwa. Aidha, baadhi ya Mitaa ambayo haijarasimishwa (Mitaa 559) imeingizwa kwenye Mradi wa Kuboreshaji Milki za Ardhi (Land Tenure Improvement Project) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ambapo utekelezaji wake umeanza. 

Wizara imeandaa Mkakati wa kushughulikia changamoto za urasimishaji baada ya kikao baina ya Wataalam wa Wizara na wadau wa urasimishaji kilichofanyika tarehe 22 Disemba, 2022. Mkakati huo, utawasilishwa kwenye kikao nilichopanga kukiongoza mapema wiki ijayo hapa Dar es Salaam ambapo ndiyo penye changamoto kubwa ya zoezi la urasimishaji.  

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alikutana na kuzungumza na vyombo vya habari kutoa salam za mwaka mpya kwa kuelezea masuala mbalimbali ya sekta ya ardhi na muelekeo wa utekelezaji kwa mwaka 2023.

---------MWISHO-----------

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya sekta ya ardhi na muelekeo wa utekezaji wa Wizara hiyo kwa kipindi cha kuanzia januari 2023 uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 3 Januari 2022.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula akizungumza kwenye mkutano na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam  tarehe 3 Januari 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link