MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
January 10, 2026

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazingira ya kujifunzia kwa kujenga skuli za kisasa zenye hadhi, viwango na ubora unaokidhi mahitaji ya elimu ya karne ya sasa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 10 Januari 2026 alipofungua Skuli mbili za Ghorofa za Ramadhan Haji Faki iliyopo Gamba, Mkoa wa Kaskazini Unguja, pamoja na Skuli ya Kifundi ya niaba iliyopo Pemba.
Amesema ujenzi wa skuli hizo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuondokana na skuli za mabanda na badala yake kuwa na majengo ya kudumu yanayokidhi viwango vya kisasa vya elimu, jambo litakalosaidia kuongeza ufanisi wa ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii na kutumia kikamilifu fursa ya miundombinu bora iliyowekezwa na Serikali.
Akizungumzia ujenzi wa dakhalia, Rais amesema utasaidia kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa nje ya mazingira ya skuli, hali ambayo imekuwa ikichangia kushusha uwezo wao wa kitaaluma, na kuwasisitiza wanafunzi kutumia fursa hiyo kufanya vizuri katika masomo yao.
Akitoa taarifa ya kitaalamu kuhusu ujenzi wa Skuli ya Gamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ndg. Khamis Abdalla Said, amesema skuli hiyo imegharimu Shilingi Bilioni 11.2 na imejengwa na Kampuni ya ZECON, ikiwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 800 kwa wakati mmoja. Ameongeza kuwa Skuli ya Kifundi ya Pemba imegharimu Shilingi Bilioni 9.4 na imejengwa na Kampuni ya SALEM Construction.
Skuli hizo zimejengwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Benki ya Maendeleo ya Kiarabu (BADEA), kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha sekta ya elimu na kukuza rasilimali watu Zanzibar.

MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Written By CCMdijitali on Saturday, January 10, 2026 | January 10, 2026

Labels:
ZANZIBAR
January 09, 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema maendeleo yanayoonekana hivi sasa katika sekta mbalimbali Zanzibar ikiwemo sekta ya elimu ndiyo lilikuwa lengo la Mapinduzi Matukufu ambayo yalidhamiria kuboresha Maisha ya watu.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa Ufunguzi wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi iliyopo Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Amesema hivi sasa inashuhudiwa ndoto ya waasisi wa Mapinduzi Matukufu ikiendelea kutimizwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Rais amesema fursa za masomo kwa wananchi wa Zanzibar zimeongeza ambapo, wakati wa Mapinduzi mwaka 1964, kulikua na Skuli 68 hivi sasa kuna zaidi ya skuli 1200, waliokuwa masomoni mwaka 1964 walikua elfu ishirini na tano hivi sasa zaidi ya wanafunzi laki sita wanapata elimu pamoja na kuwa na Vyuo Vikuu Vitano hivi sasa ikilinganishwa na mwaka 1964 ambapo hakukuwa na Chuo Kikuu.
Halikadhalika Makamu wa Rais amesema, Serikali imeendelea kufanya mabadiliko makubwa ya Mitaala ambayo imejielekeza katika kufundisha kujimudu katika kufikiri kutafiti na kubuni pamoja na mafunzo kwa vitendo. Ameongeza kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweza kuimarisha mitaala yake na kujielekeza katika ufundishaji wa kiteknolojia na kuboresha miundombinu ya maabara na madarasa na mfumo utakaowezesha vijana kujitegemea kupitia uwepo wa mkondo wa masomo ya jumla na masomo ya amali.
Makamu wa Rais ametoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuenzi na kulinda amani kwa namna yeyote kwa kuwa maendeleo yeyote yanahitaji uwepo wa amani na utulivu.
Amesema katika kipindi cha miaka 62 tangu Mapinduzi Matukufu, matunda ya Muungano yameonekana wazi ambapo, Tanzania imeendelea kuulinda na kuutetea uhuru, umoja, maendeleo, pamoja na amani.
Makamu wa Rais amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa maendeleo makubwa katika kipindi cha miaka mitano pamoja na kulinda Muungano na Amani.
Vilevile, Makamu wa Rais amewapongeza wananchi waliojitolea kwa uzalendo sehemu ya ardhi kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Makunduchi.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Khadija Salum Ali, amesema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaendelea kushirikiana katika kusimamia elimu ngazi zote ikiwa ni pamoja na mipango ya kuendelea kujenga majengo bora ya utoaji elimu unguja na pemba. Pia amesema Serikali itaendelea kuongeza karakana pamoja na vituo vya amali kwaajili ya kuongeza ujuzi kwa wanafunzi, kusimamia mitaala na miundombinu iliyojengwa na inayoendelea kujengwa.
Ujenzi wa Skuli hiyo iliyogharimu shilingi bilioni 6.1, inahusisha ghorofa nne ambazo zina madarasa 42, ofisi za walimu nne, ukumbi wa mitihani, maabara 2, maktaba, pamoja na chumba cha kompyuta,

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
09 Januari 2026
Zanzibar.
MAENDELEO YANAYOONEKANA KATIKA SEKTA MBALIMBALI ZANZIBAR IKIWEMO SEKTA YA ELIMU NDIYO LILIKUWA LENGO LA MAPINDUZI MATUKUFU
Written By CCMdijitali on Friday, January 9, 2026 | January 09, 2026

January 08, 2026

Kuanzishwa kwa chuo cha mafunzo cha Idara ya Uhamiaji Zanzibar ni hatua muhimu katika kuwaongezea uwezo wa kitaalamu, kiutendaji na kimaadili Maafisa na askari wa Idara ya Uhamiaji Tanzania.
Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la msingi la chuo cha Mafunzo ya Idara ya Uhamiaji Kitogani, Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema kupitia chuo hicho Maafisa wa uhamiaji wateweza kujengewa uwezo katika masuala ya udhibiti wa mipaka, usalama wa Taifa, matumizi ya teknolojia, sheria za uhamiaji na kuheshimu haki za binaadamu jambo ambalo litaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma na kulinda maslahi ya nchi.
Mhe Hemed ameuagiza uongozi wa Idara ya uhamiaji kwamba chuo hicho kisiwe kwa ajili ya kutoa mafunzo ya awali pekee bali kitoe mafunzo ya mara kwa mara kwa maafisa, kufanya tafiti, kubadilisha uzoefu na Mataifa mengine duniani ili Idara ya Uhamiaji iendelee kuongeza hadhi zaidi katika masuala ya kiuhamiaji kwa ngazi ya Kikanda na Kiamtaifa.
Ameutaka Uongozi na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji kuhakikisha nchi inakuwa salama dhidi ya wahamiaji haramu sambamba na wageni wanaoingia na kutoka kuendelea kufurahia huduma zinazotolewa na Idara hio kupitia mifumo ya kidijitali ili kurahisisha utoaji wa huduma mbali mbali kwa wageni na wanyeji wanaofika kwa ajili ya kupata huduma mbali mbali.
Hata hivyo, Makamu wa Pili wa Rais wa amemtaka mkandarasi na msimamizi wa chuo hicho kuhakikisha ujenzi huo unazingatia viwango vya ubora vinavyokubalika pamoja na kukamilika kwa wakati ili kutoa huduma kama kilivyokusudiwa.
Nae Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. George Simbachawene(MB) amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuendelea kuiimarisha Idara ya uhamiaji ili kuwa na hadhi ya Kitaifa na Kimataifa katika utoaji wa huduma zilizo bora kwa wananchi na wageni wanaoingia nchini..
Mhe. Simbachawene amesema Idara ya uhamiaji inaendelea kuimarika katika utoaji wa huduma kwa kutumia mifumo ya kielektroniki katika utoaji wa paspoti, uombaji wa vibali, ulinzi, udhibiti wa mipaka na wahamiaji haramu pamoja na kuongeza wigo wa makusanyo ya mapato yasiyotokana na kodi.
Aidha Mhe. Simbachawene ameahidi kusimamia vyema ujenzi na uendeshaji wa chuo hicho ili kiweze kuzalisha wataalamu wenye ujuzi, nidhamu na weledi katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo ulinzi wa mipaka na utoaji wa huzuma bora kwa wannachi.
Kwa upande wake Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Ndugu Hassan Ali Hassan ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupatiwa boti kwa ajili ya kufanyia doria baharini ambayo itasaidia kudhibiti mipaka ya baharini, kudhibiti wahamiaji haramu pamoja na kufanya doria za visiwani kwa lengo la kuhakikisha usalama na utulivu kwa watalii wanaofika visiwani humo.
Kamishna Hassan amefahamisha kuwa Idara ya Uhamiaji inajipanga kuhakikisha kuwa kabla Serikali ya awamu ya nane kumaliza muda wake Idara ya Uhamiaji Zanzibar imekamilisha ujenzi wa Ofisi zake kwa Mikoa na Wilaya zote za Zanzibar ili kuimarisha utendaji kazi kwa Maafisa wa Uhamiaji.
Amesema kukamilika kwa ujenzi wa chuo hicho kutaleta mageuzi makubwa Zanzibar kwa kuwa chachu ya kuboresha mashirikiano ya kiutandaji nadani na nje ya nchi.
Akisoma taarifa ya kitaalamu juu ya ujenzi wa chuo hicho, Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratib na Baraza la Wawakilishi Dkt. Islam Seif Said amesema ujenzi wa jengo hilo umetekelezwa kwa kuzingatia taratibu zote za kisheria uliogharimu shilingi za Kitanzania zaidi ya Bilioni kumi na mbili ambalo litalaza wanafunzi 320 kwa kila jengo na kwenda kutatua changamoto ya maeneo ya kufanyia mafunzo na kupatikana mazingira mazuri na salama ya kuishi maafsa wanapokuwa mafunzoni.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kutenga fedha za mgao zinazotokana na makusanyo ya Idara ya Uhamiaji ili kuweza kutekeleza Miradi mbali mbali ya maendeleo itakayorahisisha utowaji na upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Chuo cha Mafunzo cha Idara ya Uhamiaji kimejengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia fedha za makusanyo ya ndani ya Idara ya Uhamiaji na kuwa chuo cha Kwanza cha Idara ya Uhamiaji Zanzibar tangu kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Imetolewa na Kitengo Cha Habari ( OMPR )
Leo tarehe 08 / 01 / 2026
UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI CHUO CHA MAAFISA WA UHAMIAJI- KITOGANI
Written By CCMdijitali on Thursday, January 8, 2026 | January 08, 2026

Naibu Waziri Millya akutana na Uongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. James Kinyasi Millya (Mb), amekutana na Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania, Shekh Khawaja Muzaffar Ahmad, aliyetembelea Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kujitambulisha na kuwasilisha salamu za pongezi kwa Uongozi wa Wizara kwa utekelezaji uliotukuka wa majukumu yake.
Mhe. Millya, akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabiti Kombo (Mb), aliishukuru Jumuiya ya Ahmadiyya kwa juhudi zake katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii na kibinadamu maeneo mbalimbali nchini. Aliendelea kueleza kuwa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania imekuwa mshirika muhimu katika maendeleo ya taifa na kwamba Serikali inatambua na kuthamini mchango wa taasisi hiyo katika kuleta maendeleo endelevu nchini katika sekta mbalimbali.
Ameongeza kuwa Wizara ipo tayari kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za jumuiya hiyo, ikiwemo utekelezaji wa programu za kurejesha kwa jamii na mikutano, ikiwa ni pamoja na Mkutano Mkuu wa Mwaka (Jalsa Salana) unaotarajiwa kufanyika Septemba 2026, na Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Jumuiya ya Ahmadiya Duniani unaopangwa kufanyika mwezi July 2026 nchini Uingereza.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdalah Kilima pamoja na maafisa waandamizi wa Wizara.
Kwa upande wake, Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya Tanzania, Shekh Khawaja Muzaffar Ahmad, amesema kuwa tangu jumuiya hiyo ilipoanzishwa mwaka 1934, imefanikiwa kuanzisha matawi 450 nchini na kueneza mafundisho ya Dini ya Kiislam kwa misingi ya Qur’an Tukufu, huku ikikuza amani, upendo, udugu, uvumilivu, heshima, na kusaidia watu wote bila kujali kabila, imani au itikadi zao.
Sheikh Ahmad ametaja miradi na programu za kurejesha kwa jamii inayotekelezwa na jumuiya hiyo kuwa ni mradi wa hospitali, shule za msingi na sekondari mkoani Morogoro, chuo cha mafunzo cha ufundishaji dini kwa wazawa, uchimbaji wa visima kuunga mkono juhudi za serikali katika kampeni yake ya Kumtua ndoo mama, ambapo hadi sasa wamechimba visima 500 katika maeneo mbalimbali nchini na mradi wa kuendeleza Kijiji cha Kisasa katika Mkoa wa Geita.
Shekh Ahmad aliambatana na viongozi wakuu wa Jumuiya hiyo, wakiwemo Naibu Amiri-1Shekh Abid Mahmood Bhatti, Naibu Amiri-2 Shekh Abdurahman M. Ame, Katibu wa Mambo ya Ndani Bw. Yahya A. Kambaulaya, Katibu wa Mambo ya Nje Bw. Abdallah Kombo na Katibu wa Sauti na Video Shekh Asif M. Butt.

Millya akutana na Uongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya

KITAIFA
January 07, 2026

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar afungua Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla,amefungua rasmi Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 62 ya Zanzibar yanayiendelea katika viunga vya maonyesho vya Nyamanzi, Fumba mjini Unguja.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Abdulla amesisitiza umuhimu wa maonesho hayo kama chombo cha kukuza biashara, kuongeza fursa za uwekezaji na kuinua sekta ya uzalishaji hasa kwa wajasiriamali wa ndani.
Alieleza kuwa serikali itaendelea kuwa miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa biashara ndogo ndogo, za kati na kubwa ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa uchumi wa visiwa vya Zanzibar na Pemba.
Mheshimiwa Abdulla ametembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi zake za AICC,APRM na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt .Salim Ahmed Salim.
Katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Abdullah Abdullah alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Afisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bw. Ally Ally na wafanyakazi wa Wizara walioko katika afisi hiyo.
Mheshimiwa Abdulla amewapongeza watumishi wa Wizara na taasisi zake kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao.
Naye Mkurugenzi wa Maonyesho hayo amewataka wadau walioshiriki maonesho hayo kutumia fursa hiyo ya kipekee kuuza bidhaa, kutafuta washirika wa kibiashara na kupanua mitandao ya uwekezaji kwa kuwa maonyesho hayo ni jukwaa muhimu la kukuza soko la ndani na nje ya nchi.
Maonesho hayo yanashirikisha zaidi ya taasisi 316 kutoka serikalini, kampuni binafsi na washirika wa kimataifa yatamalizika Januari 16,2026.

Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar yafunguliwa
Written By CCMdijitali on Wednesday, January 7, 2026 | January 07, 2026