TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Habari hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na
Chama Cha Mapinduzi.
Aidha tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.
Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa Makamu wa Rais
10/8/2015