NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

GPE and CAMFED Host Roundtable on Education with Tanzanian CSOs

Written By CCMdijitali on Wednesday, November 29, 2023 | November 29, 2023

 Retired President Dr. Kikwete shares space in a Roundtable discussion on Education with Tanzanian CSOs in Dar es salaam

The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, in a group photo with members of CSOs after their roundtable today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam.

The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, participate in a roundtable discussion with CSOs today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam.


 

 
Dar es Salaam, 29th November 2023 - The Chair of the Board of Directors of the Global Partnership for Education (GPE), H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Retired President of the United Republic of Tanzania, along with GPE’s Chief Executive Officer, Ms. Laura Frigenti, are set to participate in a significant roundtable discussion today at the Campaign for Female Education (CAMFED) Tanzania offices in Dar es Salaam.
 
According to Ms. Anna Sawaki, CAMFED Tanzania’s Director of Programs and Partnership, the primary objective of the roundtable is to collectively emphasise the importance of prioritising education on the political agenda.  
 
Additionally, she said, the event aims to recognise the pivotal role of Civil Society Organisations (CSOs) in advocating for education and actively contributing to policy dialogue within local education groups.  
 
“The roundtable will also provide an opportunity for CSO representatives to share their successful practices and experiences in supporting the transformation of education systems”, Ms Sawaki explained.
 
Among the CSOs expected to attend the roundtable are HakiElimu, PESTALOZZI, Shule Direct, UWEZO, Ubongo Kids, Lyra in Africa, World Vision, Binti Salha Foundation, TEN/MET, TEM/MET, CAMFED, CAMFED Tanzania, Transforming Life Tanzania, and Gender Networking (TGNP).
 
The Global Partnership for Education (GPE) is  the largest global fund exclusively dedicated to reshaping education in lower-income countries. Operating as a unique, multi-stakeholder partnership, GPE works towards delivering quality education to ensure that every child, regardless of gender, has access to hope, opportunity, and agency.
 
For the past two decades, GPE has been actively disbursing funds and providing support to develop robust and resilient education systems in countries marked by extreme poverty or conflict. The focus is on enabling more children, particularly girls, to receive the education necessary for personal growth and contribution to building a more prosperous and sustainable world.
 
GPE's distinctive model has played a pivotal role in helping partner countries make significant strides in enhancing access, learning outcomes, and equity, resulting in improved educational opportunities for millions of boys and girls.
 
On the other hand, CAMFED, a pan-African movement, is leading a revolutionary approach to delivering girls' education. Through a gold-standard system of accountability to the young people and communities they serve, CAMFED has established a model that significantly improves the prospects of girls becoming independent and influential women.
 
CAMFED's work is driven at the grassroots level by local committees and teams comprising graduates, teachers, parents, government officials, and other volunteers who dedicate their time and expertise to ensure more girls successfully complete their education. The organisation’s governance structures include the boards of each national entity.
 
The roundtable represents a significant collaboration between GPE and CAMFED, bringing together key stakeholders and CSOs to reinforce the collective commitment to advancing education, particularly in regions facing the most pressing needs. This collaborative effort aligns with GPE's mission of transforming education systems and CAMFED's dedication to revolutionising girls' education across Africa.
 
Ends
 

PSSSF YATENGA MUDA MAALUM WA MAJUMA MANNE KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANACHAMA A

Written By CCMdijitali on Friday, November 24, 2023 | November 24, 2023

PSSSF YATENGA MUDA MAALUM WA MAJUMA MANNE KUSIKILIZA NA KUZIPATIA UFUMBUZI CHANGAMOTO ZA WANACHAMA NCHI NZIMA TANZANIA NA ZANZIBAR.

NA K-VIS BLOG/KHALFANS AID, ARUSHA

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umetenga muda maalum wa majuma manne kuanzia Novemba 27 hadi Disemba 22, 2023, kwa lengo la kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali za wanachama, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, CPA. Hosea Kashimba, amesema.

CPA. Kashimba amesema hayo kwenye banda la PSSSF katika Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Novemba 24, 2023.

“Iwapo kuna mwanachama yeyote mwenye changamoto yoyote inayohusu uanachama, michango na mafao, afike katika ofisi za PSSSF zilizo jirani naye Tanzania bara na Zanzibar, tutamsikiliza na kutatua changamoto yake.” Alisisitiza.

Alisema zoezi hilo litakuwa likifanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na moja jioni, Jumatatu hadi Ijumaa.

“Lakini hata baada ya kipindi hicho maalum kufikia ukomo, bado tutaendelea kuwapatia huduma wanachama wetu, lengo hasa ni kuhakikisha wanachama wetu wanafurahia huduma zetu wakati wote.” Alisema CPA. Kashimba.

Pia amerejelea angalizo kwa wanachama na wastaafu, kuwa wasikubali kupokea maelekezo yoyote kutoka kwa watu wasiowajua endapo wanahisi wanachangamoto yoyote kuhusiana na uanachama wao au mafao yao.

“Tunawaasa wanachama wetu hususan wale wanaokaribia kustaafu, watambue kuwa huduma zetu zinatolewa bure bila malipo yoyote, na kama wanachangamoto yoyote wapige simu namba ya bure ‪0800 110 040‬ au kupitia mitandao yetu ya kijamii kupitia anuani ya PSSSFTZ.” Alifafanua CPA. Kashimba.

CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu PSSSF,


 

CHONGOLO: WALIPENI MADENI, WAHISHENI MALIPO YA WAKANDARASI

Written By CCMdijitali on Thursday, November 23, 2023 | November 23, 2023

 

 


 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo amesema kupitia utekelezaji wa Ilani yake ya Uchaguzi ya 2020 – 2025, CCM itahakikisha Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na kuwajengea uwezo makandarasi na washauri waelekezi wazawa, ili waweze kutekeleza miradi mingi na mikubwa ndani ya nchi na hata kushindana nje ya Tanzania, ikiwemo kulipwa madeni yao na kuwahishiwa malipo ya kazi katika miradi wanayotekeleza.

Ndugu Chongolo amesema hatua ya kuwatumia wakandarasi na washauri waelekezi wazalendo wa Kitanzania katika miradi hiyo mbalimbali ya ujenzi itaokoa fedha nyingi, ambazo kwa sasa zinalipwa kwa makandarasi wa nje, hivyo zitabakia katika mzunguko wa fedha na uchumi ndani ya nchi, zitaongeza kipato kwa wahusika, huku pia wakipata nafasi ya kuongeza ujuzi na kutengeneza fursa za ajira kwa Watanzania.

Mbali ya kuwataka watendaji wa Serikali, hususan katika Wizara ya Ujenzi kuacha mitazamo hasi dhidi ya wakandarasi na wahandisi wazawa kuwa hawawezi kazi, pia amewataka baadhi ya makandarasi wa ndani nao kuacha kuichafua tasnia ya ujenzi, kwa kuwa na kampuni za mfukoni (briefcase company), ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi, hali ambayo inajenga na kuhalalisha dhana kuwa kuna wazawa wanafanya utapeli kwa kutumia taaluma hiyo.

Katibu Mkuu Ndugu Chongolo amesema hayo jana Jumanne, Novemba 21, 2023, wakati akitoa salaam za Chama Cha Mapinduzi kwenye Mkutano wa Makandarasi na Washauri Waelekezi Wazawa, uliofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention, jijini Dodoma, ambapo amewaambia kuwa CCM inatambua changamoto zote zinazowasibu, likiwemo suala la madeni wanayodai na kucheleweshewa malipo yao katika miradi anuai wanayotekeleza maeneo mbalimbali nchini.

“Mkutano huu ni muhimu sana. Jana nimekaa na mawaziri wote wawili hawa, Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Fedha hadi usiku wa manane, ilibidi tukae kwa muda mrefu sana. Nilitaka kwanza kujua masuala kadhaa kabla sijaja hapa leo. Na hasa nililowaita na kuzungumza nao ni kuhusu malipo yenu. Nina uhakika hapa tukisema tupitishe karatasi kila mtu aandike changamoto yake, jambo la kwanza kila mmoja litakuwa ni malipo, malipo, malipo.


“Wamenieleza kwa kina jinsi wanavyochukua hatua kadhaa, hasa kutekeleza maelekezo na maagizo ya Mhe. Rais Dokta Samia Suluhu Hassan amewaagiza kuhakikisha wanafanya msawazo wa malipo ya madeni ya wakandarasi na pia kila mkandarasi alipwe anapo-raise certificate. Pia labda niseme hapa, ni muhimu mkaenda pia kujifunza kwa wenzenu wa REA (Wakala wa Umeme Vijijini) ili utaratibu ule wanaotumia kulipa wakandarasi wa umeme, uweze kutumika pia huku Ujenzi. Kule hakuna malalamiko sana,” amesema Katibu Mkuu Chongolo.


Pamoja na kuipongeza Serikali kwa kufanya mabadiliko ya Sheria ya Manunuzi, iliyopandisha kiwango cha thamani ya miradi inayoweza kutekelezwa na wakandarasi wa ndani, kutoka mradi wa thamani ya Tsh. 10 bilioni, hadi kufikia mradi wa Tsh. 50 bilioni, Katibu Mkuu Ndugu Chongolo ameitaka Serikali, kupitia Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha, kuweka utaratibu wa kisheria ambao utakaolazimu ushirikishwaji wa makandarasi wazawa katika miradi yote mikubwa nchini.

“Hili la ushirikishwaji kwenye miradi mikubwa ya kimkakati kama SGR, Bwawa la Mwalimu Nyerere, hili tunaweza kulimaliza kwa kuweka sheria ya kulazimisha wakandarasi wakubwa wanapoomba miradi hapa kwetu basi waje na wakandarasi wa ndani kama ilivyo kwa Washauri Majenzi yaani consultants.  Hii pia ni nzuri kwa maslahi mapana ya nchi yetu.


“Mfano tunafanya mradi mkubwa wa SGR lakini mkandarasi akimaliza akiondoka siku tukitaka kufanya ‘ka extension kadogo hata ka kilometa moja, hatutaweza kwa sababu hatukuweka wakandarasi wetu wapate ujuzi.  Ni kupitia watu wetu kushiriki, ndiyo tungeweza kufanya kama ambavyo baadhi ya nchi zingine duniani zinafanya kujenga uwezo kwa watu wao kwa kitu kinachoitwa ‘Technological Transfer" amesema Katibu Mkuu Chongolo.


Ndugu Chongolo amewahakikishia Makandarasi na Washauri Waelekezi hao wa ndani kuwa CCM itasimamia maslahi yao, kwa kadri ambavyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025 ilivyoahidi kuwa Chama kitaielekeza Serikali kuhakikisha inaweka mazingira rafiki na bora, ikiwa ni pamoja na kujengewa uwezo wa kupata kazi nyingi zaidi za fedha za Mfuko wa Barabara na kuwawazesha kupata mikopo ili washiriki kikamilifu kwenye miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara, madaraja, majengo, maji na mingine mingi.

Katibu Mkuu Chongolo pia aliwataka wazawa hao kutanguliza mbele weledi, uaminifu, kujali rasilimali watu na thamani ya fedha wanapofanikiwa kupata miradi hiyo ya Serikali inayotumia fedha za umma, huku akitoa wito kuwataka waache ubinafsi wa kila mtu kupambana mmoja mmoja katika kutafuta miradi, badala yake watambue umuhimu wa kuungana (Joint Ventures), na wafanye hivyo mapema, si wakati wa kutafuta miradi pekee, ili kujenga kuaminiana katika ubia wa kibiashara wanaokuwa wameingia.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Daniel Godfrey Chongolo


MFUMO UNGANISHI KUONDOA CHANGAMOTO SEKTA YA ARDHI- PINDA

Written By CCMdijitali on Wednesday, November 22, 2023 | November 22, 2023

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda akizungumza na Menejiment ya Wizara pamoja na Timu ya wataalamu wanaoboresha Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023.  Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Lucy Kabyemera.



Na Munir Shemweta, WANMM ARUSHA

Serikali imesema Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi unaoboreshwa na timu ya wataalamu jijini Arusha utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa changamoto mbalimbali za sekta ya ardhi nchini.

Mfumo huo unaotarajiwa kuanza katika mikoa mitano ya Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Tanga utarahisisha na kuharakisha upatikanaji wa huduma za sekta ya ardhi kwa kuwa wananchi watakuwa wakipata huduma kwa njia ya mtandao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda mkoani Arusha tarehe 22 Novemba 2023 alipokutana na kuzungumza na Menejiment ya Wizara pamoja na Timu ya wataalamu inayooboresha Mfumo huo. 

Amesema, sekta ya ardhi imekuwa na changamoto nyingi lakini hatua ya wizara ya Ardhi kufanya maboresho ya kimfumo kutasaidia kuondoa kero na kelele za wananchi kwenye masuala ya ardhi.

‘’Kikubwa ambacho nimeanza kufarijika ni kwamba ‘mmeadvance’ mpaka hapa mlipofika katika kuboresha mfumo, hongereni sana baada ya muda tutakwenda kumaliza kelele za wananchi wa nchi hii’’ alisema Mhe. Pinda.

Kupitia maboresho ya mfumo huo unganishi wa kutunza taarifa za ardhi changamoto zote za sekta ya ardhi ikiwemo upatikanaji namba ya malipo, malipo ya ada mbalimbali, upatikanaji hati, uthamini pamoja na migogoro ya ardhi zinaenda kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya kimtandao.

Kwa mujibu wa Pinda, itachukua muda kufikia malengo yaliyokusudia katika kuboresha mfumo huo kwa sababu kinachofanyika sasa ni kuwahamisha wananchi kutoka kwenye mfumo waliouzoea na kwenda katika teknolojia mpya.

Hata hivyo, amewatahadharisha wataalamu wanaoboresha mfumo huo pamoja na maofisa wa wizara ya ardhi kuwa makini kutokana na upinzani wanaoweza kuupata kutoka kwa baadhi ya watu aliowaeleza kuwa ni wanufaika wa mifumo ya sasa ambayo wizara ya ardhi inaenda kuachana nayo.

‘’lazima mkawe standby wakurugenzi na maofisa, wale waliokuwa wanakula kupitia mfumo wa kawaida mjue ndiyo ‘threat’ namba moja wao ndiyo watakaoanza kusema mfumo wa ardhi bure kabisa lazima tutengeneze timu ya kuwaattack’’ alisema Pinda.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera alimueleza Mhe. Pinda kuwa, Menejiment ya wizara imepitia kila hatua ya jinsi mfumo unavyofanya kazi lengo likiwa kufanya maboresho yatakayowezesha idara za wizara hiyo kutekeleza majukumu kwa ufanisi.

‘’Kupitia mawasilisho ya wataalamu tungetamani mfumo ukamilike mapema lakini kwa kuwa kazi hiyo inahitaji utaalamu, tunaamini kazi hiyo itakamilika ndani ya muda mfupi’’ alisema Lucy

Mkurugenzi wa Tekonolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Ardhi Bw. Flateny Michael Hassan alisema, kufutia wizara ya ardhi kuwa na changamoto kadhaa kwenye mifumo yake imeonekana upo uhitaji wa kuunganisha mifumo yote ili kuwa na mfumo mmoja utakaohusika na sekta ya ardhi.

Amebainisha kuwa, kazi inayofanyika ya kuboresha mfumo kwa sasa imefikia asilimia 75 na ni matarajio yake mapema Januari 2023 mfumo utaanza kutumika katika mkoa wa Arusha kabla ya kuendelea na mikoa mingine.

Ameyataja maboresho yanayoendelea kufanyika kuwa ni pamoja na mfumo unaoruhusu watumishi wa sekta ya ardhi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi zao, mfumo unaoruhusu wananchi kuomba huduma kwa njia ya mtandao na huduma ya Mobile App ambapo mwananchi anaweza kupata huduma kupitia simu ya kiganjani.

‘’Katika maboresho yanayoendelea, kuna mifumo mitatu wa kwanza ni Back Office unaoruhusu watumishi kutekeleza majukumu yao ndani ya ofisi, wa pili ni Public Portal unaoruhusu wananchi kuomba huduma online na wa tatu ni Mobile App ambapo wananchi wanaomba huduma kupitia simu janja’’ alisema Flateny.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imekuwa katika jitihada   mbalimbali za kuhakikisha huduma za sekta ya ardhi zinapatikana kwa urahisi na haraka na uboreshaji mfumo huo pamoja na uwepo wa Klinik za Ardhi ni sehemu jitihada hizo ambazo zinaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wananchi.

--------------------------------MWISHO-------------------------------------


Sehemu ya Menejiment ya Wizara wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda (Hayupo pichani).

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera akizungumza wakati Naibu Waziri Mhe. Geofrey Pinda alipokutana na Menejiment na Timu ya wataalamu wanaoboresha Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023.

Menejiment na timu ya wataalamu wanaoboresha Mfumo Unganishi wa Kutunza Taarifa za Ardhi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geofrey Pinda (haupo pichani) alipokutana nao jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)







TANZANIA MWENYEJI WA TAMASHA LA DUNIA LA WATU WENYE USIKIVU HAFIFU



Na Eleuteri Mangi, WUSM

Tanzania ni mwenyeji wa tamasha la dunia la watu wenye usikivu hafifu (viziwi) likihusisha shindano la kumsaka mrembo, mtanashati pamoja na wanamitindo litakalofanyika Novemba 25, 2023 jijini Dar es salaam.

Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo Novemba 22, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Leah Kihimbi amesema maadalizi yanaendelea vizuri na Tanzania imejipanga kufanikisha tamasha hilo ambalo Tanzania imepewa heshgima ya kuwa mwenyeji kwa miaka miwili mfululizo.

Maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vyema kwa washiriki kujinoa ili kutoa taji la urembo, utanashati pamoja na wanamitindo dunia kwa viziwi ambapo mashindano hayo yanafanyika kwa mara ya pili mfululizo hapa nchini baada ya kufanyika kwa mara ya kwanza Afrika na Tanzania kwa 2022.

Hadi sasa washiriki zaidi ya 200 wa tamasha hilo wameshawasili tayari nchini wanatoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania. 





WAZIRI MAKAMBA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI EAC JIJINI ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb.) akiteta na jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki muda mfupi kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba (Mb) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 22 Novemba 2023.

 

Mkutano huo ambao ulianza tarehe 18 Novemba 2023 kwa ngazi ya wataalam na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu umepitia na kujadili mapendekezo yatakayowasilishwa katika Kikao cha Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha tarehe 24 Novemba 2023.

 

Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri wa EAC pamoja na mambo mengine umejadili masuala kuhusu Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 hadi 24 Novemba, 2023; utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya kuhusu Majadiliano ya Ombi la Shirikisho la Jamhuri ya Somalia kujiunga na EAC; juhudi za utafutaji wa  Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya; majadiliano kuhusu Katiba ya Fungamano la kisiasa la Jumuiya; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki; na Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya uandishi wa insha kwa wanafunzi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

Mkutano huo umehudhuriwa na Mawaziri ambao ni Wajumbe kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Rwanda, Sudan Kusini na Uganda.

 

Kukamilika kwa Mkutano huo wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kutafuatiwa na Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC uliopangwa kufanyika tarehe 24 Novemba 2023 jijini Arusha.

 

Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira ambao pia utahudhuriwa na Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya EAC.

 

Mkutano huo unalenga kupata msimamo wa pamoja wa Jumuiya ya EAC kuelekea katika Mkutano wa Kimataifa wa 28 wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP 28) utakaofanyika kuanzia Novemba 28, 2023 nchini UAE.

 
Meza Kuu wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha

Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angela Kairuki wakifuatilia Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha

Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania ukiwa umesimama wakati wimbo wa Jumuiya unapigwa kwenye Mkutano wa 44 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha

DKT. BITEKO AKAGUA MAJENGO YA WIZARA YA NISHATI; SERA, URATIBU NA BUNGE

DKT. BITEKO AKAGUA MAJENGO YA WIZARA YA NISHATI;  SERA, URATIBU NA BUNGE MJI WA SERIKALI- MTUMBA


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko leo amekagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Nishati na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) katika Mji wa Serikali- Mtumba jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo, Dkt. Biteko  aliambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jimmy Yonaz, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Petro Lyatuu pamoja na Watendaji mbalimbali kutoka Wizara hizo mbili.

Katika Jengo la Wizara ya Nishati, Dkt. Biteko ameshuhudia ujenzi ukiendelea ambapo kwa sasa umefikia asilimia 69 na Mkandarasi anayehusika na ujenzi huo ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

Aidha, ujenzi wa jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu), unaendelea vizuri huku ukiwa umefikia asilimia 74 na Mkandarasi ni SUMA JKT.







NAIBU WAZIRI KIKWETE AZINDUA USAMBAZAJI WA MIFUMO KUBORESHA UWAJIBIKAJI KAZINI

Written By CCMdijitali on Tuesday, November 21, 2023 | November 21, 2023



Uzinduzi wa Zoezi la Usambazaji wa mfumo wa kutathmini na kuhakiki utendaji wa kazi wa Watumishi na Taasisi yaani PEPMIS/PIPMIS NA HR Assessment limefanyika mapema tarehe 20 Novemba 2023 katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, mjini Iringa.

Akizungumza wakati anazindua mpango huo wa usambazaji wa Mfumo wa PEPMIS/PIPMIS NA HR Assessment katika shughuli ambayo ilihudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Halima Dendegu, Katibu Tawala wa Mkoa huo Mwandisi Masanja, na watumishi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri zote za mkoa huo na waratibu wa TASAF toka makao makuu ya TASAF - Dodoma ambao walifuatana na Naibu Waziri. 

Mh. Kikwete aliuelezea mfumo huu kuwa unakwenda kutatua pamoja na changamoto nyinginezo katika utumishi, mapungufu yaliyojitokeza katika mfumo wa OPRAS. 

Ndugu Naibu Waziri aliwakumbusha watumishi kujua kuwa mfumo huu imekuja kuleta ufanisi na faida nyingi ikiwemo kutambua mahitaji ya kweli ya kiutumishi






DKT. BITEKO AIAGIZA TPDC KUANDAA MPANGO WA MUDA MREFU WA UPATIKANAJI GESI NCHINI


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameagiza Bodi na Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuja na mpango wa muda mrefu utakaoonesha jinsi nchi itakavyoweza kuongeza kiasi cha gesi asilia

Amesema kuwa kufanya hivyo kutawezesha kuwepo kwa hazina ya kutosha ya nishati hiyo inayotumika kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme, viwandani, majumbani na katika magari.

Dkt. Biteko ameyasema hayo tarehe 21 Novemba, 2023 wakati wa kikao chake na Bodi na Menejimenti ya TPDC ambacho kililenga kufahamiana, kubadilishana mawazo juu ya utendaji kazi na Mhe. Dkt. Doto Biteko kuelekeza matarajio ambayo nchi inayahitaji kutoka TPDC.

“TPDC tujiulize, Je uwezo wetu wa kuzalisha Gesi Asilia unaweza kujibu mahitaji yetu  ya Gesi ? tujiulize hili na tuchukue hatua. Tutambue kuwa mahitaji ya Gesi Asilia ni makubwa kwa sasa kwani dunia inahama kutoka matumizi ya mafuta na kwenda kwenye Gesi Asilia hivyo lazima tujipange, na pia tukumbuke tumesaini makubaliano ya kusafirisha nishati hii kwenda Uganda, Zambia na Kenya hivyo lazima tuwe na Gesi ya kutosha.” Amesisitiza Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko pia amewataka TPDC kutokuwa na urasimu katika uchukuaji wa maamuzi mbalimbali ikiwemo kwenye shughuli za utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia ili kutorudisha nyuma sekta hiyo nchini.

Kuhusu maelekezo aliyoyatoa wakati wa ziara yake, katika Kisiwa cha Songosongo mkoani Lindi na Kijiji cha Madimba na Msimbati mkoani Mtwara, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, maisha ya wananchi katika maeneo hayo ambayo kuna visima na mitambo ya Gesi Asilia lazima yabadilike na wapewe huduma bora ikiwemo maji, umeme, afya na usafiri.

“Nashukuru mmeanza kufanyia kazi maagizo niliyoyatoa kwa haraka, ikiwemo ya kuweka taa za barabarani Kijiji cha Msimbati, kupeleka umeme wa uhakika Madimba na Msimbati unaotoka kwenye mitambo ya Gesi Asilia, kupeleka kivuko kisiwa cha Songosongo na malipo ya mafao kwa wastaafu wa Knight Support ambao walikuwa wakilinda mitambo na visima vya Gesi Asilia Songosongo ambao hawakulipwa muda mrefu, watu hawa wanahitaji huduma bora.”


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko


SHIBUDA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMTEUA MAKONDA KUWA MWENEZI WA CCM

Written By CCMdijitali on Monday, November 20, 2023 | November 20, 2023


MAGALLE SHIBUDA AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUMTEUA MAKONDA KUWA MWENEZI WA CCM KWANI AMEONESHA JUHUDI NA SHABAHA ZA KUUNDA DARAJA RAFIKI KWA KAZI ZA RAIS SAMIA NA WATANZANIA


  • Asema Makonda amejenga uhusiano rafiki wa Kanda ya ziwa kwa kutoa Ahsante kwa uwajibikaji wa Serikali ya awamu ya 6 ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan

  • Amejenga na kuleta wokovu wa mlango wa kutokea huzuni za ndani zilizounda ugumu wa mioyo katika kufumbua maono ya Ahsante_

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vyama Vya Siasa, MNEC Mstaafu na Mbunge wa (CCM 2005 & CHADEMA 2010) Mstaafu Magalle John Paul Shibuda ametoa barua aliyoandika Manufaa na Faida kwa Chama Cha Mapinduzi kutokana na Ziara ya Mikoa ya Kanda ya ziwa iliyofanywa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndg. Paul Makonda.

Katika Barua hiyo, Mstaafu Shibuda ameandika kuwa Ziara ya Mwenezi Makonda imebainisha wazi kuwa kuna maisha ya Wajibu wa Uzalendo hitajika wa kufaidisha manufaa ya Maslahi mapana kwa Ujenzi wa kuunda Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Uchumi na Taifa.

Mstaafu Shibuda amesema Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anastahili Tuzo za Utu kwa hali na sababu ni Kiongozi Mkwamuaji wa madhila yaundayo Huzuni.

Amesema kwa kuthibitishi hilo, Watanzania warejee kwa uundwaji wa Kamati kadhalika mfano ya Mhe. Jaji Mstaafu Othman Chande ya kuimairsha Haki za Raia.

Mstaafu Shibuda ameendelea kuandika kuwa Ziara ya Mwenezi Makonda imewadhiirishia Umma kuwa Serikali ya awamu ya 6 ina unyenyekevu wa kutumikia Maslahi ya Umma na kusema kuwa Simu zote kwa Mawaziri ni Fursa rafiki kwa Umma nao utambue kwa umakini na ukubali kuwa ni Uwazi na Ukweli pana mipango ya kazi za kutengua kasoro zinazounda sintofahamu kwa yao matumaini na matarajio ya Wananchi.

Pia, Mstaafu Shibuda amesema binafsi yake ameona Mwenezi Makonsa ameunda vema somo la kwamba Serikali ina wajibu wa kukithaminisha chama kinachoongoza Serikali hiyo ambacho ni CCM na vivyo hivyo CCM ina wajibu wa kuisadikisha Tija ya Serikali yake ndani ya Umma dhisi ya Propaganda Hasi za Vyama Kinzani.

Aidha, Mstaafu Shibda amemtaka Mwenezi Makonda kuendelea kusomesha kuhusu yeye anatenda uwajibikaji wake aminifu kwa Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

Kwa kumalizia, Mstaafu Shibuda ametoa rai kwa CCM kuwa macho na kupambanua akili zao dhidi ya mikakati ya wazuaji wa tafsiri ovu ambazo zinataka kuunda hali ya kuchafuana wenyewe kwa wenyewe na kuwataka kutokuwa malighafi au kitoweo cha Propaganda hasi za kujenga kuandika Uongo mtamu dhidi ya umoja na mshikamano wao.

MWISHO.



MHE. BITEKO ATOA MAAGIZO KWA MSAJILI WA HAZINA

Written By CCMdijitali on Friday, November 17, 2023 | November 17, 2023

MHE. BITEKO ATOA MAAGIZO KWA MSAJILI WA HAZINA KUELEZA SABABU YA MASHIRIKA YA UMMA KUTOSHIRIKI SHIMMUTA 2023


Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko amemuagiza Msajili wa Hazina kufikia Jumatatu Novemba 20, 2023 awasilishe taarifa kwa nini mashirika mengi ya Serikali hayajatoa kibali kwa watumishi wao kushiriki Mashindano ya Taasisi, Mashirika ya Umma na Binafsi (SHIMMUTA) mwaka 2023 jijini Dodoma.

Mhe. Biteko ametoa maagizo hayo wakati akifungua mashindano hayo Novemba 17, 2023 Uwanja wa Jamhuri Dodoma ambapo amebaini mashirika ya umma yapatayo 248 nchini hayakushiriki mashindano hayo huku mashirika 54 pekee ndio yametoka kibali kwa watumishi wao kushiriki mashindano hayo.

"Naipongeza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kuendelea kusimamia vyema michezo, kwa sasa tunashuhudia nchi yetu ikitangazwa vyema na hivi karibuni tumepata uwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa kushirikiana na wenzetu wa Kenya na Uganda" Mhe. Doto Biteko.

Mhe. Biteko amewaasa wanamichezo hao kutumia michezo hiyo kubadilishana uzoefu, kupeana mbinu za mafanikio lakini pia kujifunza kuweka alama mahali wanapofanyia kazi pamoja na kutimiza wajibu wa kuhakikisha wanatatua matatizo ya wananchi kupitia sehemu za kazi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma amezipongeza Taasisi za Serikali, Mashirika ya Umma na Binafsi yaliyotoa ruhusa kwa Watumishi kushiriki mashindano hayo, akisema ni hatua nzuri ya kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza michezo nchini.


"Katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Sita, tumeshuhusia Maendeleo makubwa katika Sekta ga michezo ikiwemo kupata uwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027, Klabu ya Simba kucheza hadi robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2022/ 23 na Klabu ya Yanga kucheza hadi Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2022/23" amesema Mhe Mwinjuma.

Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Gerson Msigwa amesema lengo la Mashindano hayo ni kuimarisha afya za watumishi na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza, huku akitoa rai kwa makampuni, taasisi za Serikali na binafsi kutekeleza  maelekezo ya Serikali ya kufanya mazoezi na kushiriki mashindano mara kwa mara.

Mashindano hayo yanajumuisha michezo 12 ikiwemo Mpira wa Miguu, Netiboli, Mpira wa Wavu, Riadha, Kivuta Kamba, na mingine ikihusisha wamichezo 3478.








RAIS MSTAAFU DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKUTANA NA BALOZI WA CANADA NCHINI MHE KYLE NUNAS JIJIJINI DAR ES SALAAM LEO

Written By CCMdijitali on Thursday, November 16, 2023 | November 16, 2023

Na Issa Michuzi

Mkutano huo wa siku tatu umeandaliwa na Wizara ya Afy na Ofisi ya Rais TAMISEMI  kwa kushirikiana na washirika kadhaa ikiwa ni pamoja na taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), kwa lengo la kuleta wadau muhimu pamoja ili kusambaza, kuthibitisha, na kujifunza mafundisho yanayopatikana kwa vitendo bora na hatua za msingi zinazotokana na ushahidi wa kisayansi ili kuhakikisha utekelezaji bora.

Mkutano huo hutumika kama jukwaa kubwa kwa wataalamu wa afya, watunga sera na wadau kukutana ili  kushirikiana maarifa, kutathmini athari za mikakati iliyopo, kushughulikia masuala magumu, kufikiria suluhisho za ubunifu, na hatimaye kuleta mabadiliko chanya.
 
Moja ya mada kuu ya mkutano huu ilikuwa ni mikakati ya Tanzania kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 (SDG) na malengo ya Mwaka 2025 yanayohusiana na ubora wa huduma za RMNCAH+N.
 
Tayari Tanzania imeandaa mfululizo wa mipango ya kitaifa muhimu kuboresha ubora wa huduma, ikiwa ni pamoja na Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo (2021-2025), Mpango wa Sekta ya Afya wa Mkakati (HSSP V, 2021), na Mpango Mmoja wa III (2021-2026).
 
Mipango hii inalenga kuboresha mfumo wa afya, kuongeza upatikanaji wa huduma za RMNCAH, na kupunguza viwango vya vifo vya  mama wajawazito na watoto wachanga. Kufikia malengo haya  kunahitaji kuweka kipaumbele katika mikakati ya kuongeza athari na kuanzisha mifumo bora ya kuhakikisha ubora.
 
Huduma za RMNCAH+N  zinaunganishwa katika ngazi mbalimbali za utunzaji, kutoka kwa wafanyakazi wa afya wa jamii hadi watoa huduma za afya katika hospitali za rufaa za kitaifa na hospitali maalum. Ushirikiano wa ufanisi kati ya ngazi hizi, sasisho la miongozo kwa kawaida, na motisha na fidia za kutosha kwa wafanyakazi husababisha kuongezeka
 
Ushirikiano wa ufanisi kati ya ngazi hizi, sahisisho la miongozo, motisha na fidia za kutosha kwa wafanyakazi husababisha kuongezeka kwa utoaji wa huduma na matokeo bora kwa ujumla. Hata hivyo, kuna masuala kadhaa na uchunguzi unaokwamisha ushirikiano huu.
 
Ubora wa huduma za RMNCAH+N unatumika kama kipimo cha mfumo wa afya wa Kitaifa. Ushirikiano kati ya wadau mbalimbali, kutoka kwa watoa huduma za afya hadi taasisi za serikali na wafadhili, ni muhimu kuhakikisha ustawi wa akina mama na mtoto. Kutekeleza changamoto na mapendekezo yaliyoainishwa ni muhimu kwa mustakabali bora kwa akina mama na watoto ulimwenguni.
 
Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) inalenga kubadilisha maisha ya jamii kupitia masuluhisho ya kibunifu na endelevu, wakati leongo lake katika RMNCAH+N  ni kufanya kazi kama mwendeshaji  ili kuhakikisha hakuna vifo visivyo vya lazima vya akina mama. Misingi yake mikuu ni kubadilisha Maisha watu, kukuza ushirikiano, na kuweka kipaumbele katika matokeo ya pamoja kupitia ushirikiano.


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  akisalimiana na baadaye kuongea na Balozi wa Canada nchini Mhe. Kyle Nunas pembezoni mwa  Mkutano wa Pili wa Kisayanzi ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto katika Ukumbi wa Kimataifa  wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo.

MCHAKATO HADHI MAALUM KWA DIAPSORA KUKAMILIKA MWAKA 2024

Written By CCMdijitali on Tuesday, November 14, 2023 | November 14, 2023

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajia kukamilisha utaratibu wa kuwapatia Hadhi Maalum Watanzania waishio nje ya nchi, yaani diaspora ifikapo mwaka 2024.

Hayo yamesemwa katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na diaspora wa Tanzania nchini Uholanzi kwa heshima ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) aliyepo nchini humo kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia tarehe ‪13 - 15‬ Novemba 2023.

Akifafanua masuala mbalimbali yaliyowasilishwa kupitia risala ya Watanzania iliyosomwa na Mwakilishi wa Umoja wa Watanzania waishio nchini Uholanzi, Bi. Sylvana  Lubuva, Mhe. Makamba alisema utekelezaji wa Hadhi Maalumu unategemea kufanyika kwa mapitio ya baadhi ya sheria za nchi kama ile ya ardhi na uhamiaji ili kurahisisha utekelezaji wenye tija kwa walengwa, yaani diaspora na kwamba mchakato huo unatajiwa kukamilika kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

“Miongoni mwa masuala yatakayopewa kipaumbele kwenye Hadhi Maalum ni haki ya kurithi au kurithishwa mali kwa diaspora wa Kitanzania aishiye nje ya nchi. Ili kutekeleza hili kuna maeneo ya sheria yetu lazima yabadilishwe ili watoto wenu wanaoishi huku nje waweze kurithi au kumiliki ardhi” alisema Waziri Makamba.

Sambamba na hilo, ni utaratibu wa kulipa visa pindi diaspora wa Tanzania wanaporudi nyumbani. “Kwenye Hadhi Maalum, mtaruhusiwa kuja nyumbani na kukaa kwa muda mnaotaka bila malipo ya visa. Lakini kwanza ni lazima sheria yetu ya uhamiaji ipitiwe na kurekebishwa, ili kuruhusu  kurudi nyumbani bila kulipishwa visa” alisisitiza Waziri Makamba.

Baadhi ya masuala mengine yatakayowanufaisha watumiaji wa Hadhi Maalum ni fursa na motisha mbalimbali za kuwekeza nchini Tanzania kupitia Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC).

Kadhalika, Mheshimiwa Makamba alisisitiza umuhimu wa kujisajili kwenye mfumo wa Diaspora Digital Hub ambapo alisema licha ya kusaidia kuwatambua Watanzania waishio nje ya nchi, pia inarahisisha kwa kiasi kikubwa kuwarejesha nchini pindi majanga makubwa yanapotokea maeneo mbalimbali duniani.

“Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi imara wa Mama Samia Suluhu Hassan, imeelekeza kuokoa Mtanzania au Watanzania popote pale walipo pindi majanga yanapowakuta. Imefanya hivyo kuwaokoa Watanzania waliokua masomoni Ukraine, imewarejesha nyumbani Watanzania waliokuwa Sudan na hivi karibuni Israeli” Mhe. Makamba aliongeza.

Mazoezi haya ya kuwarejesha Watanzania nyumbani hufanyika chini ya uratibu wa Ofisi za Ubalozi zilizopo nchi husika au nchi jirani na hivyo huratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mhe. Makamba yupo nchini Uholanzi kwa ziara ya kikazi ambapo siku ya pili ya ziara hiyo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uholanzi.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka katika ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi, jumla ya watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi nchini Uholanzi na maeneo ya karibu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikinao wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe aliofuatana nao katika ziara hiyo, watumishi wa ubalozi na watanzania wanaoishi nchini Uholanzi baada ya kumalizika kwa kikao.

Afisa Mwandamizi kutoka Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ramadhan Mzuzuri akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu Diaspora katika mkutano wa Mheshiwa Waziri na Diaspora uliofanyika Jijini The Hague, Uholanzi.

Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Carilone Chipeta akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Mheshimiwa Waziri na Diaspora uliofanyika Jijini The Hague, Uholanzi.
 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi katika kikao kilichofanyika Jijini The Hague, Uholanzi ambapo amewasisitiza Watanzania hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Taifa lao.


SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI

Written By CCMdijitali on Monday, November 13, 2023 | November 13, 2023


SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI WANAOFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-KIKWETE.    


Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete aliyasema hayo Bungeni wakati Swali ya Mbunge wa Same Mashariki Ndg. Anna Kilango Malecela . 

Naibu Waziri alisema, Serikali imeendelea kutoa motisha ya kifedha na isiyo ya kifedha kwa watumishi wote ikiwemo watumishi wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu kwa kuboresha viwango vya posho ya kazi baada ya masaa ya kazi, posho ya kujikimu wakati wa kusafiri, posho ya mawasiliano, kufikisha huduma ya umeme katika maeneo yao, kutoa magodoro, kutoa nyumba za walimu zenye staha na mengine mengi.

Akijibu swali la Ziada, alimuhakikishia Mbunge na Bunge kuwa Serikali inatambua changamoto za Watumishi katika Halmashauri yao na nyengine Nchini kwa kuwa iko timu iliyokwisha zunguka nchi nzima kukagua mazingira ya Watumishi hivyo upatikanaji wa fedha na mipango ya huduma kwa Watumishi itawahakikishia mazingira mazuri ya Watumishi wanaofanya kazi katika mazingira Magumu. 





#KaziInaendelea #Bungeni





MAJALIWA ASISITIZA NIDHAMU, MAADILI, UBUNIFU KWA WATUMISHI WA UMMA

Written By CCMdijitali on Saturday, November 11, 2023 | November 11, 2023



WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wafanye kazi kwa bidii, weledi, nidhamu, uadilifu na ubunifu ili kutimiza maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaletea maendeleo Watanzania.

Amesema kila mtumishi anapaswa kutambua kuwa mafanikio katika utekelezaji wa majukumu, mipango na mikakati wanayoisimamia yanahitaji juhudi ya kila mtumishi na nidhamu katika kufanya kazi.

Ametoa wito huo leo Jumamosi Novemba 11, 2023 katika kikao na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika ukumbi wa mikutano wa PSSSF jijini Dodoma.

“Nitoe wito kwa kila mtumishi kuzingatia nidhamu ya kazi na maadili ya utumishi wa umma, Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatekeleza falsafa ya Kazi Iendelee. Kwa msingi huo watumishi wote wa umma mnao wajibu wa kufuata na kutekeleza falsafa hii. ”

 Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza watumishi hao kwa kuendelea kutekeleza majukumu yao vizuri na kwa weledi. “Kujituma kwenu, ushirikiano na bidii vimewezesha Serikali na hususan Ofisi ya Waziri Mkuu kupata mafanikio makubwa. ”

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa tangu Rais Dkt. Samia aingie madarakani amekuwa anatoa msukumo wa kuboresha mazingira ya watumishi na kusisitiza kushughulikia stahiki mbalimbali za watumishi wa umma ikiwemo ulipaji wa malimbikizo ya mishahara, upandishaji wa madaraja na utoaji wa ajira mpya.

 “Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amelipa madai malimbikizo ya mishahara ya watumishi 121,858 yenye jumla ya shilingi bilioni 207.97, pia amepandisha madaraja watumishi 91,841 na shilingi bilioni 73.4 zimetumika kuwalipa watumishi hao” 

Pia, Mheshimiwa Majaliwa aliwakumbusha watumishi hao kusimamia kikamilifu na kwa makini miradi na programu zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ili Ofisi isipoteze fursa ya kuungwa mkono na Taasisi za Kimataifa “Endeleeni kutoa huduma bora za Serikali kwa umma pamoja na kuratibu na kusimamia shughuli za Serikali katika sekta zote kwa ufanisi na tija. ”





 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link