MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
TANZANIA MWENYEJI WA TAMASHA LA DUNIA LA WATU WENYE USIKIVU HAFIFU
Written By CCMdijitali on Wednesday, November 22, 2023 | November 22, 2023
Hadi sasa washiriki zaidi ya 200 wa tamasha hilo wameshawasili tayari nchini wanatoka mataifa ya Afrika Kusini, Australia, Belarus, Brazil, Ethiopia, Falme za Kiarabu, Guyana, Haiti, Hispania, India, Iran, Italia, Kenya, Kongo DRC, Malasia, Macedonia, Marekani, Mexico, Misri, Morocco, Msumbiji, Nigeria, Pakistan, Poland, Romania, Rwanda, Senegal, Siera Leone, Sudan Kusini, Thailand, Tunisia, Jamhuri ya Czechoslovakia, Ufaransa, Uganda, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.
WAZIRI UMMY ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI KWA AJILI YA UTAMBUZI NA ELIMU JUU YA SARATANI.
Written By CCMdijitali on Saturday, October 21, 2023 | October 21, 2023
Waziri Ummy katika matembezi hayo ambapo ameambatana na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mhe. Charlotta Azaki pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Afya.
TANZANIA YAPOKEA OMBI LA PALESTINA KUANZISHA KITUO CHA MICHEZO
Written By CCMdijitali on Thursday, October 19, 2023 | October 19, 2023
Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Tanzania Mhe. Hamdi Mansour Abuali Oktoba 19, 2023 Jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Mhe. Ndumbaro amepokea maombi ya nchi ya Palestina kupitia Balozi huyo, kuanzisha Kituo cha Michezo Jijini Dar es Salaam nakuahidi kulifanyia kazi mapema iwezekanavyo.
Mhe. Balozi Hamdi amewasilisha Ombi hilo akieleza kuwa nchi hiyo ina ushirikiano wa muda mrefu na Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo Utamaduni na Michezo, hivyo Kituo hicho kitakua na umuhimu kwa nchi mbili hizo katika kukuza michezo.
TANZANIA KUWASILISHA OMBI CAF MATUMIZI YA MATANGAZO YA KISWAHILI
Written By CCMdijitali on Monday, October 16, 2023 | October 16, 2023
Na Shamimu Nyaki
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inatarajia kuwasilisha ombi la kuweka matangazo kwa lugha ya Kiswahili katika Mashindano ya Kombe la Mataifa Barani Afrika AFCON yatakayochezwa mapema mwaka 2024.
Mhe. Ndumbaro amesema hayo Oktoba 16, 2023 alipofanya ziara Ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), ambapo amepongeza juhudi za Baraza hilo katika kubidhaisha lugha hiyo Kimataifa pamoja na kuzalisha wakalimani na Watafsri mbalimbali.
Amesema, Tanzania ikishirikiana na Kenya na Uganda imefanikiwa kupata uwenyeji wa mashindano hayo mwaka 2027 ambayo ni fursa ya kutangaza lugha ya Kiswahili katika mashindano hayo.
"Tunataka Kiswahili kitengeneze fursa nyingi, mwaka wa fedha wa 2024/25 tutatenga fedha kwa ajili ya kuuza lugha hii ambayo kwa sasa imeajiri Watanzania 103 Duniani, pamoja na kushirikiana na Sekta Binafsi katika kubidhaisha lugha yetu adhimu ya Kiswahili" amesisitiza Mhe. Ndumbaro.
Awali Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bi. Consolatha Mushi ameeleza kuwa, katika Mkakati wa miaka kumi wa Kubidhaisha Kiswahili wa 2022 - 2032, tayari wamefungua vituo 32 ambavyo 10 vipo katika Balozi za Tanzania na tayari limepokea maombi ya kuanzisha vituo vya kujifunza lugha hiyo kwa nchi za Ufaransa na Uturuki.
Bi. Consolatha amesema nchini Urusi kuna Vyuo Vikuu vitano ambavyo lugha hiyo inatumika kikiwemo Chuo Kikuu cha Moscow pia inatumika katika shughuli za Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika (SADC)
UJENZI WA HOSTELI MALYA KUONGEZA UDAHILI WA WANACHUO
Written By CCMdijitali on Sunday, October 8, 2023 | October 08, 2023
Na Eleuteri Mangi, WUSM
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Bw. Richard Mganga amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hosteli za chuo hicho ambacho ni ni chuo pekee kinachotoa mafunzo ya michezo kwa wataalamu wa michezo nchini.
Chuo hicho kipo mkoani Mwanza katika Wilaya ya Kwimba ambapo jukumu lake kuu ni kufundisha taaluma ya michezo, kutafiti na kutoa ushauri kuhusu masuala ya maendeleo ya michezo.
Ili kufikia azma hiyo ya Serikali, Bw. Maganga amesema chuo hicho kinaendelea na ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanachuo takriban 192 kwa wakati mmoja ili kuongeza idadi ya wataalam wa michezo nchini.
Bw. Mganga amesema hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wastani wa wanachuo 48 kwa kila ghorofa na itakuwa na vyumba nane vya kusomea, vyoo pamoja na sehemu ya kufulia na kunyoshea nguo.
Mradi huo wa ujenzi wa hosteli ya Ghorofa tatu linatarajiwa kutumika kwa ajili ya makazi ya wanafunzi na upo chini ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo unakadiriwa kutumia kiasi cha Shilingi 2,562,032,000 hadi kukamilika kwake ambapo hadi sasa Wizara imepokea kiasi cha Tshs 1,699,156,86.
Ujenzi wa hosteli hiyo umefikia asilimia 69 ikukamilika mwakani 2024 itasaidia kuongeza ya idadi ya wanafunzi chuoni hapo kwa kuwa hosteli inayotumika sasa inauwezo wa kuchukua wanafunzi 128.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASISITIZA KUWATUMIA WACHEZAJI WENYE ASILI YA TANZANIA WALIO NJE YA NCHI, AAGIZA WIZARA HUSIKA ZIKUTANE
Written By CCMdijitali on Wednesday, October 4, 2023 | October 04, 2023
Na Shamimu Nyaki
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ifanye kikao na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuona namna ya kuwatumia wachezaji wenye asili ya Tanzania wanaocheza nje, ili wapate nafasi ya kuitumikia Timu ya Taifa ya Tanzania.
Mhe. Majaliwa ametoa agizo hilo Oktoba 4, 2023 Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, katika hafla ya kuwapongeza na kukabidhi Hundi ya Shilingi Milioni 500 kwa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars), ikiwa ni zawadi ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya timu hiyo kufuzu kucheza michuano ya AFCON mwaka 2023 itakayofanyika mapema mwakani nchini Ivory Coast.
"Nawaelekeza Wizara ya fedha kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa zinafika kwa wakati ili ukarabati ukamilike kabla ya mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa kuwa nchi yetu ndio muandaji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda. Pia asilimia 5 inayotengwa kutokana na mchezo wa kubashiri kwa ajili ya Mfuko wa michezo ifike kwa wakati" amesisitiza Mhe. Majaliwa.
Ameilekeza pia Wizara ya Utamaduni, ishirikiane na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Baraza la Michezo Tanzania kuandaa mpango thabiti wa kuhakikisha unawezesha Taifa Stars kuwa na maandilizi mazuri na kuelekea mashindano ya AFCON mwaka 2023 na mwaka 2027 ili Timu hiyo ifanye vizuri.
Ameipongeza Wizara na Shirikisho hilo ihakikishe Tanzania inafanikiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON mwaka 2027 kwa kushirikiana na Kenya na Uganda huku akiviasa vilabu vinavyoshirirki mashindano ya Kimataifa vifanye vizuri kwa kuwa Goli la Mama bado linaendelea.
Awali Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Sekta ya Michezo inaendelea kufanya vizuri kwa kuwa hivi karibuni timu za Mpira wa Miguu za Wanawake Serengeti Girls na timu ya JKT Queens zilitwaa Ubingwa wa CECAFA na JKT Queens itashiriki Klabu Bingwa Afrika.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema mwezi Novema hadi Disemba wataendesha mashindano ya Mpira wa Miguu kwa wanaume na Wanawake chini ya miaka 17 Jijini Mwanza lengo likiwa ni kupata wachezaji wengi watakaotumikia Timu za Taifa.
DKT. NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP
Written By CCMdijitali on Thursday, September 21, 2023 | September 21, 2023
DKT. NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP
Na Shamimu Nyaki.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameiagiza Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya Samia Taifa Cup ambayo yatafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mhe. Ndumbaro ametoa maagizo hayo Septemba 21, 2023 Zanzibar wakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo ambayo yatahusisha michezo mbalimbali.
"Mwaka huu mashindano yatajumuisha pia Zanzibar na kutakua na Mashindano ya Muziki wa Kizazi Kipya. Lengo la mashindano haya ni kuendelea kuenzi Muungano wetu na kuhakikisha jamii inajishughulisha na michezo, Sanaa na Utamaduni kwakua ni Sekta ambazo zinaibua vipaji na kutoa fursa ya ajira" amesema Mhe. Ndumbaro.
Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema vifaa hivyo vitagawiwa katika mikoa yote ya Zanzibar na mashindano yataanzia katika ngazi ya Shehia mpaka Mkoa ili kupata wawakilishi wazuri Kitaifa.
Miongoni mwa vifaa alivyokabidhi Mhe. Ndumbaro ni pamoja na mipira ya michezo ya mpira wa Miguu, Kikapu na Wavu ambayo kila mchezo mipira 18 huku akiwakaribisha wadau kuiunga mkono jambo hilo katika michezo mingine.
MAKAMPUNI JITOKEZENI KUFADHILI VILABU VYA SOKA NCHINI
Written By CCMdijitali on Sunday, September 17, 2023 | September 17, 2023
Na Eleuteri Mangi, WUSM, Tanga
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu ametoa wito kwa makampuni mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kujitokeza kudhadhili vilabu vya soka na michezo mbalimbali nchini ili ziwe na ushindani katika medani za kitaifa na kimataifa.
Katibu Mkuu Bw. Yakubu ametoa wito huo jijini Tanga akiwa Mgeni Rasmi wakati timu ya Coastal Union ilpokuwq ikisaini mkataba na kampuni ya Elsewedy Electric Cable East Africa Ltd ambayo itaifadhili timu hiyo kwa msimu wa 2023/2024 pamoja na kuzindua jezi itakayotumika kwa msimu huu.
"Mpira sasa unahitaji vitu vitatu, ufundi kwa maana ya utaalam wa michezo kwa wachezaji na viongozi, vipaji vya wachezaji vinavyokuzwa na kulelewa na kuwaandaa kuwa wachezaji bora ambao watumiwa na vilabu, timu ya taifa na hata soka la kulipwa nje ya nchi pamoja na fedha ambazo ndiyo chachu ya soka na michezo mingine kwa kuzingatia michezo ni ajira" amesema Katibu Mkuu Bw. Yakubu.
Amewataka uongozi wa timu ya Coastal Union kutumia fedha zitakazotolewa na wafadhili hao kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuweka mikakati mizuri ya ushindi.
Aidha, ametoa wito kwa Mfadhili huyo Mpya na kusisitiza kuwa Coastal Union ni dude lililolala, ufadhili wao na utaalam utaiamsha timu hiyo ili ifanye vizuri katika medani ya soka kwa kuzingatia Misri ni taifa kubwa kisoka barani Afrika na kuwataka waisaidie timu hiyo kupate wasaa wa kuwa na maandalizi mazuri ya msimu ujao kwa kuwapa nafasi ya kuweka kambi nchini Misri.
Kwa upande wao Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Elsewedy Electric East Africa Mhandisi Ibrahim Qamar na
Mkurugenzi wa Biashara katika Miradi Bw. Muhammad El Shazly wamesema wanafuraha kufanyakazi na timu ya Coastal Union kwa kuwa historia zao zinafanana, kampuni hiyo imeanzishwa mwaka 1938 na timu ya Coastal Union imeanzishwa 1948.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu hiyo Steven Mguto amesema ufadhili ambao wamepata utasidia timu hiyo kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni kuijenga timu iwe na ushindani na kushika nafasi nne za juu katika ligi ya NBC ili mwakani washiriki mashindano ya kimataifa.
Timu ya Coastal Union imeanzishwa mwaka 1948 na imewahi kuwa bingwa mwaka 1988 huku wachezaji nguli kuchezea timu hiyo na timu ya Taifa. Wachezaji hao ni Mohamed Mwameja, Ally Maumba, Yasin Napili, Idrisa Ngulungu, Mohammed Salum, Hilal Hemed, Mchunga Bakari, Riffat Saidi, Juma Mgunda, Bakari Mwanyeto na Abdalah Sopu.























.jpg)


































