MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
ZIARA YA RAIS SAMIA BUMBULI, LUSHOTO MKOANI TANGA
Written By CCMdijitali on Monday, February 24, 2025 | February 24, 2025
BALOZI NCHIMBI: CCM KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO WA NDANI NA NJE
Written By CCMdijitali on Thursday, February 13, 2025 | February 13, 2025
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza dhamira yake ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa ndani na kimataifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
CCM ambacho ni chama tawala nchini kimeeleza kuwa kitasimamia Serikali ili kuendeleza uhusiano mzuri na mataifa na taasisi mbalimbali, ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alipokutana kwa nyakati tofauti na mabalozi wa Korea Kusini, Norway na Uingereza katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, leo Alhamisi, tarehe 13 Februari 2025.
Katika mazungumzo yake na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Ahn Eunju, Balozi Nchimbi alisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Korea Kusini, hasa katika nyanja za maendeleo ya kiuchumi na teknolojia.
Katika mazungumzo yake na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Mhe. Tones Tinnes, Balozi Nchimbi alibainisha kuwa Norway ni mshirika mkubwa wa maendeleo wa Tanzania, huku uhusiano wao ukiwa umejengwa katika misingi imara kwa miongo mingi.
Vilevile, katika mazungumzo yake na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Marianne Louise Young, Balozi Nchimbi alisema kuwa uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Uingereza, pamoja na ushirikiano wa karibu na Serikali ya Chama cha Labour, unalenga kuhakikisha wananchi wa pande zote mbili wananufaika na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Kwa nyakati tofauti, katika mazungumzo yao na Katibu Mkuu wa CCM, mabalozi hao walipongeza maamuzi ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliomchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Nchimbi kuwa mgombea mwenza, na Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM.
UCHAGUZI MKUU UTAFANYIKA, WANA-CCM, WANANCHI JIANDAENI - WASIRA
Written By CCMdijitali on Tuesday, February 11, 2025 | February 11, 2025
Na Mwandishi wetu, Mwanza
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uchaguzi mkuu wa mwaka huu utafanyika kama ulivyopangwa kwa taratibu za kisheria, na kwamba hakuna chombo cha serikali wala chama cha siasa chenye mamlaka ya kuuahirisha.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Stephen Wasira, leo Februari 11, 2025 alipohutubia mkutano mkutano katika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Wasira amesema watu wanaotoa hoja kwamba uchaguzi mkuu hautafanyika hadi yawepo mabadiliko ya Katiba wanajisumbua kwa kuwa makubaliano yalishafanyika kuwa mabadiliko ya Katiba yatafanyika baada ya uchaguzi mkuu, hivyo hakuna anayeweza kuahirisha kufanyika kwa uchaguzi mkuu kwa namna yoyote.
“Tumekubaliana tumalize uchaguzi, zile sheria za uchaguzi zifanyiwe marekebisho, wabunge wanajua Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani imepitishwa na Bunge, Sheria ya Vyama vya Siasa imefanyiwa marekebisho na imepitishwa na Bunge.
“Chadema wamekuwa na msemo wao maarufu ‘no reform no election’ (kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi), sasa mimi hapa nasema leo uchaguzi mkuu utafanyika. Wanaosema uchaguzi hautafanyika mpaka mabadiliko yafanyike wanajisumbua, uchaguzi utafanya na Watanzania wajiandae.
“Sisi ni Chama cha siasa lazima tufanye uchaguzi ili tuendelee kuleta maendeleo ya Watanzania. Tumewaambia hakuna tunachoogopa kwa sababu hata Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024 wameshindwa kuweka wagombea. Halafu wakishindwa wanasingizia CCM,” amesema Wasira.
Amesisitiza kuwa kwa taratibu za kisheria, si chombo cha serikali wala chama cha siasa kina uwezo wa kuahirisha uchaguzi mkuu, huku akifafanua kuwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kisheria inalo jukumu la kutangaza tarehe ya uchaguzi, lakini haina uwezo wa kuahirisha.
“Na kama kutakuwa sababu ya uchaguzi mkuu kusogezwa mbele au kuahirishwa basi ni kwa sababu ya uwepo wa vita lakini kwa bahati nzuri nchi yetu haina vita, iko salama na kazi ya kuleta maendeleo inaendelea. Hivyo hakuna chama cha siasa kinaweza kuahirisha uchaguzi na suala la mabadiliko ya Katiba ni la kisheria.
#KaziIendelee
SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI
Written By CCMdijitali on Monday, November 13, 2023 | November 13, 2023
SERIKALI KUENDELEA KUWABEBA WATUMISHI WANAOFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-KIKWETE.
Akijibu swali la Ziada, alimuhakikishia Mbunge na Bunge kuwa Serikali inatambua changamoto za Watumishi katika Halmashauri yao na nyengine Nchini kwa kuwa iko timu iliyokwisha zunguka nchi nzima kukagua mazingira ya Watumishi hivyo upatikanaji wa fedha na mipango ya huduma kwa Watumishi itawahakikishia mazingira mazuri ya Watumishi wanaofanya kazi katika mazingira Magumu.
Kinana:CCM INAMPA HEKO DKT. MWINYI
Written By CCMdijitali on Saturday, November 4, 2023 | November 04, 2023
Na Mwandishi Wetu
CHAMA Cha Mapindizi (CCM), kimeridhishwa na uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi.
Hayo yamesemwa leo Novemba 4, 2023, na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, katika maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wa Dk. Mwinyi.
Kinana amesema Dk. Mwinyi amejituma sana na kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Unguja na Pemba huku akiwaunganisha kuwa kitu kimoja.
Akiyataja mafanikio yaliyopatikana Zanzibar kwa miaka mitatu tangu Rais Dk. Mwinyi alipoingia madarakani, Ndugu Kinana amesema ni pamoja na kuharakisha maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na miradi ya wananchi ya kiuchumi.
Aidha, amesema amewaunganisha wananchi, hivyo kusahau tofauti za itikadi za kisiasa, na watu wote kuwa wamoja.
Ndugu Kinana amefafanua kwamba, hatua hiyo inatoa matumaini katika kipindi cha miaka miwili iliyobakia kufikia ukamilikaji wa malengo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.
“Rais Mwinyi tunakushuru sana, katika kipindi cha miaka mitatu umefanya mambo makubwa, ikiwemo kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuwaunganisha wananchi na kuimarisha amani na utulivu wa kisiasa,” amesema Ndugu Kinana.
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHURIA MISA MAALUM YA KUMBUKIZI YA KUMUOMBEA BABA WA TAIFA
Written By CCMdijitali on Saturday, October 14, 2023 | October 14, 2023
CHONGOLO AWA MBOGO BAADA MRADI WA MAJI KUCHELEWESHWA
Written By CCMdijitali on Wednesday, October 11, 2023 | October 11, 2023
RAIS SAMIA AKISALIMIANA NA RAIS WA INDIA
Written By CCMdijitali on Monday, October 9, 2023 | October 09, 2023
KARIBU MWENGE WA UHURU MKOANI TABORA
Written By CCMdijitali on Wednesday, September 13, 2023 | September 13, 2023
SERIKALI YATOA MWEZI MMOJA TATHMINI KUFANYIKA MGOGORO WA ARDHI UWANJA WA NDEGE MWANZA
Written By CCMdijitali on Friday, October 21, 2022 | October 21, 2022
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Serikali imetoa mwezi mmoja kuanzia Oktoba 19, 2022 kufanyika tathmini ya kina kwenye eneo lenye mgogoro wa ardhi linalozunguka uwanja wa ndege wa Mwanza.
Mgogoro huo unahusisha wananchi na Mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA) na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hayo yamebainishwa jana katika kata ya Shibula wilayani Ilemela mkoa wa Mwanza na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta ilipotembelea eneo hilo ikiwa ni sehemu ya ziara ya kamati hiyo kwenye mikoa mbalimbali nchini kuhusu utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975.
"Sasa tathmini ya kina itafanyika ndani ya mwezi mmoja, tunapoondoka hapa wataalamu wa timu ya kitaifa watapita nyumba baada ya nyingine kwa mitaa yote kufanya tathmini ya kina ndani ya mwezi mmoja tupate majibu" alisema Dkt Mabula.
Dkt Mabula ambaye ni kiongozi wa Kamati ya Mawaziri Nane wa Wizara za Kisekta aliwaambia wananchi kwenye mkutano huo kuwa, serikali ya awamu ya sita haikutaka kuchukua uamuzi wa mwaka 2019 mojamoja na badala yake imerudi kwa wananchi wa maeneo hayo ili kupata ushauri wa changamoto za eneo hilo kabla ya kutoa maamuzi
"Lengo hapa la kuja kwa timu ya kitaifa kufanya tathmini ni kujua nani ni nani na aliingia kwa wakati gani yote yatapatikana ndani ya mwezi mmoja" alisema Waziri Mabula.
Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, ushauri utakaotolewa na kamati yake baada ya timu ya mkoa kujiridhisha pamoja na kamati ya wataalamu kupitia tena eneo hilo kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta itatoa taarifa yenye maslahi kwa watanzania wote.
Ameitaka timu ya wataalamu kupewa nafasi na ushirikiano ili iweze kufanya kinachostahili ikiwemo kuonesha uthibitisho mbalimbali kama vile nyaraka na hatua zote za kiserikali zitafuatwa.
Kumbukumbu kuhusiana na mgogoro wa ardhi eneo la uwanja wa ndege wa Mwanza zinaonesha kiwanja hicho kilipimwa mwaka 1987 kikiwa na ukubwa wa hekta 1,470 kwa kuzingatia eneo lililokuwa limelipwa fidia kati ya mwaka 1978 hadi 1980
Hata hivyo, mwaka 2003 hadi 2004 Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ilijenga uzio kuzunguka eneo la kutua na kurukia ndege pamoja na miundombinu iliyopo ili kuimarisha usalama wa kiwanja cha ndege ambapo wakati wa ujenzi wa uzio iligundulika eneo pekee la kiwanja cha ndege lililovamiwa na wananchi ilikuwa ni mtaa wa Nyagungulu kata ya Ilemela.
Baada ya ujenzi wa uzio kulitokea tafsiri potofu kwa wananchi wakidhani kuwa mwisho wa mipaka ya kiwanja cha ndege ni uzio huo na kupelekea kuanza kuvamia eneo la kiwanja ambako kuna mitaa ya mhonze b, kihili, nyamilolelwa, shibula na bulyankhulu katika kata ya shibula.
----------MWISHO----------
MAKAMU WA PILI AKUTANA NA KATIBU UN WOMEN
Written By CCMdijitali on Thursday, October 13, 2022 | October 13, 2022
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Shirika la Wanawake Duniani katika kuhakikisha wanatimiza malengo yao waliyojiwekea.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa Kauli hiyo alipokutana na Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN Women) Bi Sima Sami Afisini kwake Vuga Jijini Zanzibar.
Amesema Umoja wa Mataifa unaendesha Miradi ya Maendeleo katika Sekta mbali mbali ambapo Serikali itaendelea kusimamia Miradi hiyo ili iweze kukamilika.
Mhe. Hemed ameeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua umuhimu wa Wanawake katika Maendeleo ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amewaamini Wanawake na kuwapa Nyadhifa mbali mbali katika Uongozi ikiwemo Mawaziri na kuongoza Taasisi mbali mbali.
Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amemuhakikishia Katibu Mtendaji huyo kuwa SMZ itaendelea kusimamia mikakati ya Shirika hilo ili kufikia malengo waliojiwekea.
Mhe. Hemed ametumia Fursa hiyo kumuomba Katibu Mtendaji huyo kuandaa utaratibu wa kuwaongezea uzoefu Wanawake wa Zanzibar ili kuendana na kasi ya Dunia kimaendeleo.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake Bi Sima Sami amefurahishwa kuona Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini mchango wa Wanawake kwa kuzingatia uwezo walionao.
Ameeleza kuwa Shirika hilo lina mikakati mingi kwa kuwainua Wanawake na kuiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa Mashirikiano ya kutosha kufikia malengo yao.
DKT.BITEKO: ATAKA MADINI KUONGEZA AMANI UKANDA MAZIWA MAKUU
Written By CCMdijitali on Wednesday, April 6, 2022 | April 06, 2022
![]() |
WAZIRI wa Madini, Dkt. Doto Biteko |
Aipongeza ICGLR kwa kuichagua Tanzania kufanya Mkutano wa 20 wa Kamati ya Ukaguzi
Na Steven Nyamiti- Kagera
WAZIRI wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema, Kamati ya Ukaguzi wa Madini ya Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa, madini yanayochimbwa katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo yanakuwa chachu ya amani na si migogoro.
Dkt.Biteko ametoa rai hiyo leo Aprili 4,2022 wakati akifungua Mkutano wa 20 wa Kamati ya Ukaguzi wa Madini ya Jumuiya ya Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) ambapo Tanzania ni mwenyeji wa mkutano huo unaofanyika mjini Bukoba Mkoa wa Kagera.
"Tunataka tuyaone madini haya yanachangia kwenye kuongeza amani kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu, hayachangii vita na mapigano na hayachangii migogoro," amesema Dkt. Biteko.
ICGLR inaundwa na nchi 12 ambazo ni Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Congo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Sudan Kusini, Sudan, Tanzania na Zambia.
Amesisitiza kuwa, Tanzania ikiwa miongoni mwa wanachama wa ICGLR itaendelea kuhakikisha madini yanayochimbwa katika nchi zetu hayageuki kuwa nyenzo ya kufadhili uhalifu.
Dkt.Biteko ameeleza kuwa, kikao hicho ni cha Kamati ya Ufuatiliaji wa Madini yanayozalishwa kwenye Ukanda wa Maziwa Makuu ambapo kamati hiyo ina jukumu la kufuatilia madini yanakochimbwa ili kusaidia kuleta faida kwenye nchi husika na kuongeza amani.
Akizungumzia umuhimu wa kamati hiyo amesema, madini ya Bati yanayochimbwa Kyerwa na maeneo mengine ili yaweze kuuzwa kwenye masoko ya nje lazima yawe na cheti cha uhalisia wa kule ulipoyatoa.
Dkt.Biteko amesema, kama hayana hicho cheti madini hayo hayajulikani na hayawezi kuingia kwenye soko.
Kwa upande mwingine, Dkt. Biteko amesema, mkutano huo ni muhimu kwa Tanzania hususani kwa wachimbaji huku akisisitiza wachimbaji wachimbe kwa kuzingatia Sheria na Utaratibu uliowekwa.
"Serikali imeweka mazingira mazuri sana na Rais wetu anasisitiza kila ambaye anahitaji kuchimba achimbe bila matatizo. Lakini utoroshaji wa madini hauwezi kuvumiliwa," ameongeza.
ZOEZI LA ANWANI ZA MAKAZI KUKAMILIKA IFIKAPO MEI 2022
Written By CCMdijitali on Thursday, March 31, 2022 | March 31, 2022
MAKAMU WA PILI KWENYE KILELE CHA SIKU YA MTUMIAJI
Written By CCMdijitali on Wednesday, March 16, 2022 | March 16, 2022
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezitaka Taasisi zinazohusika na kutoa huduma kuhakikisha wanashirikiana na Majukwaa ya Watumiaji katika kutoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali ili kumlinda Mtumiaji.
Mhe. Hemed ametoa wito huo katika kilele cha Maandimisho ya Wiki ya Mtumiaji kilichofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdulwakil kikwajuni jijini Zanzibar.
Amesema ni vyema kwa Taasisi hizo kuzifanyia kazi kwa vitendo sheria na Kanuni zilizopo ili kuweza kumsaidia Mtumiaji kupata huduma bora bila ya kikwazo chochote kile.
Ameeleza kuwa wapo baadhi ya watumishi hawawajibiki ipasavyo na kusababisha wananchi kuumia kutokana na uzembe wa watumishi hao hivyo amewataka viongozi kusimamia Sheria ili kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Nane kuweza kurahisisha huduma kwa wananchi wake.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amezitaka Mamlaka husika kuangalia njia bora za kiuendeshaji kwa lengo la kuwalinda watumiaji wa huduma mbali mbali.
Sambamba na hayo Mhe. Hemed amezitaka Taasisi hizo kuandaa malengo madhubuti ya kila mwaka kuweza kuwafikia wananchi kujua haki na wajibu wao .
Hata hivyo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amezitaka Taasisi husika zinazosimamia uingizwaji wa bidhaa Nchini kusimamia kutoingizwa nchini Bidhaa zisizokidhi vigezo ili kuwapunguzia wafanyabiashara wadogo wadogo kuingia katika hasara zinazoweza kuepukika.
Kwa upande wake Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaibu Hassan Kaduwara ameeleza kuwa katika kujali na kuzingatia hali za wananchi wizara imeweza kushusha bei ya Watumiaji wa umeme kwa Asilimia Hamsini ili kurahisisha huduma kwa wananchi wa Zanzibar.
Mhe. Kaduwara ameeleza kuwa baraza la kuwawakilisha watumiaji wa huduma za maji na nishati zanzibar (CRC) wanaendelea kutoa Elimu kupitia njia mbali mbali kwa wananchi ili Watumiaji kujua haki na wajibu wao katika matumizi.
Nae Mwenyekiti wa Jukwaa la Watumiaji Tanzania Bwana Leo Ngowi ameeleza kuwa Jukwaa hilo humlinda Mtoaji na Mpokeaji katika kupata huduma kwa kuweka sera na sheria madhubuti ya kulinda haki hizo.
Ameeleza kuwa TCF ndani ya Miaka mitatu ijayo imepanga kufanya tafiti ya Sera na Sheria pamoja na kuzifanyia mapitio Sheria zilizopo kwa Maslahi ya Mtumiaji.
Siku ya Mtumiaji Duniani huadhimishwa kila ifika Machi 15 ya kila mwaka ambapo kauli Mbiu kwa mwaka huu inasema USAWA KATIKA HUDUMA ZA FEDHA ZA KIDGITALI.
……………………
Abdulrahim Khamis
Ofisi ya makamu wa pili wa rais wa Zanzibar
15/03/2022
NAIBU WAZIRI SAGINI ATOA MUDA WA UKOMO WA HIARI WA UKAGUZI WA MAGARI.
Written By CCMdijitali on Friday, February 25, 2022 | February 25, 2022
NAIBU WAZIRI SAGINI ATOA MUDA WA UKOMO WA HIARI WA UKAGUZI WA MAGARI.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani Jumanne Sagini ameweka muda wa ukomo wa ukaguzi wa magari kwa hiari kwa wamiliki na madereva wa vyombo vya moto pamoja na ukaguzi unaoambatana na utoaji wa stika za usalama barabarani baada ya magari hayo kukaguliwa na Wakaguzi kutoka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani.
Aidha, Naibu Waziri Sagini amewaeleza wamiliki wa vyombo vya moto kuwa, baada ya Marchi 30, 2022 chombo chochote cha moto kitatakiwa kuwa na stika ya usalama barabarani baada ya chombo hicho kufanyiwa ukaguzi na kupewa stika na kwamba chombo cha moto kitakachoshindwa kufanya hivyo kitachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ya kushindwa kufanyiwa ukaguzi wa hiari sambamba na chombo hicho kupelekwa kwenda kufanyiwa ukaguzi wa lazima.
WATUMISHI WATANO WASIMAMISHWA KAZI MASASI MJINI
Written By CCMdijitali on Wednesday, February 9, 2022 | February 09, 2022
MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA KUZALIWA KWA CCM WILAYANI IRAMBA
Written By CCMdijitali on Monday, February 7, 2022 | February 07, 2022
MAADHIMISHO YA MIAKA 45 YA KUZALIWA KWA CCM WILAYA YA IRAMBA MWAKA 2022
Mbunge wa Jimbo la Iramba na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dr. Mwigulu Nchemba akipanda mti kwenye Maadhimisho ya miaka 45 yakuzaliwa CCM yaliyofanyika Kata ya Kidaru
Mbunge wa Jimbo la Iramba na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dr. Mwigulu Nchemba |
"TUUENDELEE KUMUUNGA MKONO MAMA YETU RAIS SAMIA" - WAZIRI KIKWETE
Vilevile Mhe Ridhiwani Kikwete ameomba tuendelee kumuunga mkono Mama yetu, Rais wa JMT Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kusudi jitihada zake kuwatumikia wananchi na kuendele kujenga nchi zizidi kuonekana. #RK #kaziinaendele #ardhimwendomdundo

,%20Balozi%20Dkt.%20Emmanuel%20John%20Nchimbi,%20akizungumza%20na%20Balozi%20wa%20Jamhuri%20ya%20Korea,%20Mhe.%20Ahn%20Eunju,%20walipokutana%20kwa%20ajili%20ya%20mazungumzo,%20Ofisi%20Ndogo%20ya%20Makao%20Makuu%20ya%20CCM,%20Lum%20(1).heic)
,%20Balozi%20Dkt.%20Emmanuel%20John%20Nchimbi,%20akizungumza%20na%20Balozi%20wa%20Jamhuri%20ya%20Korea,%20Mhe.%20Ahn%20Eunju,%20walipokutana%20kwa%20ajili%20ya%20mazungumzo,%20Ofisi%20Ndogo%20ya%20Makao%20Makuu%20ya%20CCM,%20Lumumba.heic)
















