NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

DK EMMANUEL NCHIMBI APATA MAPOKEZI MAKUBWA JIMBONI KWAKE.

Written By CCMdijitali on Friday, January 31, 2014 | January 31, 2014

 Juu wananchi waliojitokeza kwa wingi kumpokea mbunge wao Mhe Dkt Emmanuel Nchimbi leo mjini Songea. Chini Dkt Nchimbi akiongea na wapiga kura wake na amewashukuru sana kwa mapenzi waliyoonesha kwake baada ya kurejea kutoka Dar es salaam alikopata ajali ya kisiasa iliyomplekea kuwajibika kwa kujiuzuru nafasi yake ya waziri wa mambo ya ndani.

MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI CCM KATA YA SOMBETINI

MWENYEKITI WA UVCCM MKOA NDG ROBSON MEITINYIKU AKIMNADI MGOMBEA WA UDIWANI WA CCM NDG MWALIMU DAVID MOLLEL KURA KWA WANANCHI
MWENYEKITI WA UWT MKOA WA ARUSHA NDG ZELOTE AKIINADI ILANI YA CCM KWENYE MKUTANO ULIOFANYIKA JANA HUKO SOMBETINI
(Kulia - kushoto )MHESHIMIWA DIWANI OLE SEKIYANI,WA KATA YA TERRATI,MGOMBEA UDIWANI WA CCM NDG MWALIMU DAVID MOLLEL,MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA ARUSHA NDG WILFRED SOILELI NA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA NDG ROBSON MEITINYIKU WAKIWA MEZA KUU KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
KATIBU WA CCM WILAYA YA MERU NDG AKYO AKITEREMKA JUKWAANI MARA BAADA YA KUONGEA NA WANANCHI WALIOJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA KAMPERNI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
BAADHI YA WANANCHI NA WAPENZI WA CCM WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MWENYEKITI NA MGENI RASMI MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA NDG ROBSON MEITIYIKU AKIELEZA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CCM KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
WAGENI KATIKA MEZA KUU KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI

BAADHI YA UMATI WA WATU WALIOJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA KAMPERNI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MGOMBEA UDIWANI WA CCM MWALIMU DAVID MOLLEL LESIKAR AKIJIELEZA NAMNA ATAKAVYOITEKELEZA ILANI YA CCM KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI
MWNDISHI WA HABARI AKICHUKUA HABARI KATIKA MKUTANO WA KAMPENI YA UCHAGUZI WA DIWANI KATA YA SOMBETINI

NDG. ABDULRAHMAN KINANA AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA JIJINI MBEYA

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Inspekta Isack Lema Mlezi wa Bodaboda Mkoa wa Mbeya kwa upande wa jeshi la Polisi wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Mtenda uliopo Soweto mjini Mbeya kwa ajili ya kuzungumza na waendesha Bodaboda wa mjini Mbeya, ambapo wamemweleza matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi wanavyoshirikiana na jeshi la polisi na polisi jamii katika kulinda usalama wa wananchi, wao wenyewe na mali kwa ujumla, Chanagamoto mbalimbali za kimaendeleo zimetatuliwa na zitaendelea kutatuliwa ili waendesha bodaboda wafanye kazi zao kwa ufanisi na utulivu. 1AKatibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia waendesha Bodaboda ambao wameonekana kufurahia sana mkutano huo uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mtenda Soweto jijini Mbeya. 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Blogger wa Mbeya yetu Blog Bwana Joseph Mwaisango.
3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katika meza kuu kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo.
4Waendesha Bodabona wakimshagilia Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akiongea nao leo. 5
Msafara wa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ukitoka uwanja wa ndege wa Songwe kuelekea mjini Mbeya leo mara baada ya kuwasili mkoani humo. 6
Shangwe za waendesha bodaboda zikiendelea. 7
Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. 8
Pikipiki zao zikiwa zimeegeshwa nje ya ukumbi. 9Waendesha Bodaboda wakifuatilia hotuba za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi wakati wa mkutano huo. 10
Nape Nnauye Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza wakati wa mkutano huo leo. 11
Hapa ni Shangwe tu 12
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea risala ya waendesha Bodaboda kutoka kwa Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda. 13
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibebwa juujuu na waendesha bodaboda mara baada ya kuwahutubia kwenye ukumbi wa Mkenda leo. 14 
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na uongozi wa waendesha Bodaboda kushoto ni mwenyekiti Vicent Mwashoma na kulia ni Msumba Makya Katibu wa Waendesha Bodaboda.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MBEYA)

RAIS KIKWETE AFURAHISHWA NA HUDUMA ZA NMB KATIKA MPANGO WA KILIMO WA STAKABADHI GHARANI

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 28, 2014 | January 28, 2014

 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya jinzi mpango wa Stakabadhi Gharani ulivyo na manufaa kwa mkulima toka kwa Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal alipotembelea banda lao leo baada ya kufungua kongamano la kilimo Afrika Mashariki katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kilimo katika Benki ya NMB Bw. Robert Pascal akitoa maelzo kwa Rais Kikwete juu ya mafanikio ya benki hiyo katika mpango wa Stakabadhi Gharani ambao amesema unaendeshwa kwa mafanikio makubwa.

BONANZA LA MAVETERANI YOMBO MAKANGARAWE,TEMEKE LAZINDULIWA

 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Matemvu akikagua timu ya Veterani ya Yombo Kilakala wakati wa uzinduzi wa michuano ya maveterani ya Ujirani Mwema, katika Kata ya Yombo Kilakala, Temeke, Dar es Salaam juzi. Timu 12 kutoka sehemu mbalimbali za jiji zilishiriki kwenye michuano hiyo. Timu hiyo ilicheza na Kigamboni Veterani.
 Mtemvu akikagua timu ya Kigamboni Veterani. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Makangarawe, Victor Mwakasendile.
 Mtemvu akihutubia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, ambapo aliahidi kuyadhamini kwa timu zote kuzinunulia jezi za TMK. Kushoto ni Mwakasendile na Mungia Mbwana mratibu wa michuano hiyo.
 Timu za New Kivule Veterani (waliovaa Bluu) na Kitunda (waliovaa bluu nyeusi) wakipepetana
 Ni mtanange kwa kwenda mbele
 Hapiti mtu hapa
 Sasa nawatoka
 Wanachi wakishuhudia mpambano huo
 Timu za Yombo Makangarawe Veterani (BLUU)  wakicheza na Kigamboni Veterani huku wananchi wakishuhudia
 Mlinda mlango wa Kigamboni akiwania mpira na mchezaji wa Yombo Makangarawe
PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG.

Rais Kikwete aamuru Jeshi kusimamia utoaji huduma kwa waathirika wa mafuriko Morogoro

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua Daraja la Mto Mkundi mkoani Morogoro linalokarabatiwa baada ya kuharibiwa na mafuriko hivi karibuni.Rais Kikwete alitembelea eneo hilo na sehemu nyingine zilizokumbwa na mafuriko hayo kujionea uharibifu. Picha na Freddy Maro wa Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi la Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameliamuru Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuanza mara moja kazi ya kusimamia utoaji huduma kwa watu walioathiriwa na mafuriko katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni pamoja na kusimamia ujenzi wa nyumba za muda wa wahanga hao.

Rais pia ameliamuru Jeshi kupeleka mashine za kusafisha maji katika makambi ambako wahanga hao wa mafuriko ya Januari 22, mwaka huu wanaishi kwa muda.

Aidha, Rais Kikwete amewahakikishia wahanga wa mafuriko hayo kuwa Serikali itahakikisha inawapatia huduma zote za msingi ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, maji na huduma za afya hadi hapo watakapokuwa na uwezo wa kuanza kujitegemea tena.

Rais Kikwete ametoa amri hizo kwa Jeshi leo, Januari 27, 2014, wakati alipotembelea kambi za wahanga wa mafuriko hayo kuwajulia hali walioathirika katika makambi yaliyoko Shule ya Sekondari ya Magole katika eneo la Dumila na katika Kijiji cha Mateteni kilichoko Dakawa, Wilaya ya Kilosa.

Katika hotuba zake fupi baada ya kuwa ametembelea na kuona mahema ambamo wahanga hao wanalala, Rais Kikwete amesema   ameagiza Jeshi kuongoza harakati za kuwahudumia wahanga hao kwa sababu zikifuatwa taratibu za kawaida za Kiserikali huduma zitachelewa sana kuwafia waathirika.

“Kazi yetu ni kusimamia maisha ya watu hasa   kipindi cha shida za namna hii. Tukifuata taratibu za kawaida za Kiserikali za tenda tutachelewesha sana huduma za dharura kwa waathirika. Ndiyo maana nimeliamuru Jeshi kufanya kazi hii ikiwa ni pamoja na kujenga haraka makazi ya muda wa waathirika,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Katika mazungumzo hayo na Mkuu wa Majeshi, nimemwagiza pia kuleta mashine za kusafishia maji ili kuhakikisha kuwa watu wanakunywa maji salama kwa sababu katika hali ya sasa maji yasiyokuwa salama yanaweza kuwa chanzo cha magonjwa.”

Kuhusu upatikanaji wa chakula cha msaada kwa wahanga, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali inacho chakula cha kutosha kwa ajili yao. “Tunacho chakula cha kutosha na hata kile tusichokuwa nacho tutanunua. Tutabanana ndani ya Serikali ili tupate fedha za kutosha za kuwahudumia.”

Kuhusu malazi, Rais amesema:”Naambiwa kuna upungufu wa magodoro. Tutahakikisha kuwa yanapatikana na yatafika katika siku mbili zijazo. Hatutaki watu walale chini na waje kupata vichomi.”

                        Kuhusu maji, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali itaendelea kutoa huduma ya maji bure kwa wahanga. “Tutaendelea kutoa bure huduma hii mpaka hapo huduma ya kawaida ya maji itakapoanza kupatikana tena.”
Kuhusu huduma za afya, Rais amesema kuwa anafurahi kuwa kila kambi ya wahanga inayo huduma ya afya ambayo itaendelea kutolewa kwa kadri watu wanavyozidi kuishi kwenye makambi.

Rais ameagiza kuwa baada ya muda mfupi viongozi wa Mkoa wa Morogoro na wilaya husika wakae chini ya viongozi wa ngazi za chini na wahanga kujadili na kutafuta mwafaka kuhusu maisha ya baadaye ya wahanga – hasa kuhusu namna gani wanaweza kupatiwa maeneo yaliyoko nje ya mikondo ya mafuriko.

                        “Hili ni lazima kwa sababu hata kama imechukua miaka mingi kwa mafuriko ya sasa kutokea ni dhahiri kuwa iko siku yatakuja tena – inaweza kuwa hata mwaka huu kwa sababu zipo mvua za masika. Kwa hiyo ni lazima tukubaliane jinsi gani ya kurudi ama kutokurudi katika maeneo yetu tulikotoka.”   

KIKWETE AKABIDHIWA JEZI YA TIMU YA CHICAGO CUBS TOKA KWA MWENYEKITI WA TIMU HIYO,JOE RICKETTS,PIA APOKEA TABLET 61 KWA AJILI YA WANAFUNZI WA SHULE YA WAMA NAKAYAMA

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi ya timu ya baseball ya Chicago Cubs toka kwa mmiliki wa timu hiyo na Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea akipokea moja ya Tabuleti 61 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts wakati alipomtembelea Ikulu Jumapili Januari 27, 2014.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakipokea moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.
Mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya WAMA Nakayama Dkt Ramadhani Dau na Mkuu wa Shule hiyo wakiangalaia matumizi ya ya Tabuleti 61 katika darasa la kidato cha pili katika Shule ya Wama Nakayama iliyoko kijijini Nyamisati, Rufiji, Mkoa wa Pwani leo Januari 27, 2014 toka kwa Mwenyekiti wa taasisi ya kusaidia elimu ya Opportunity Education Foundation wa Marekani Bw. Joe Ricketts akikabidhi moja ya Tabuleti 61 alizozitoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha pili katika Shule hiyo.PICHA NA IKULU.

Mkutano wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM

Written By CCMdijitali on Sunday, January 26, 2014 | January 26, 2014

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na vijana Chipukizi  alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa Uwakilishi  Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akivalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma   baada  ya kuvalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwapungia mkono wanaCCM waliohuduria katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,mara alipowasili katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimnadi na kumuombea kura kwa wanaCCM na Wananchi, Mgombea wa  CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM katika viwanja vya mpira Kiembesamaki.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo 
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa uwakilishi wa  CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link