NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

AWAMU YA TATU KAMPENI YA CHANJO YA POLIO KUANZA TAREHE 1-4 SEPTEMBA 2022

Written By CCMdijitali on Tuesday, August 30, 2022 | August 30, 2022




Na Englibert Kayombo WAF - Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Afya inatarajia kuanza Kampeni ya Awamu ya tatu ya kutoa matone ya chanjo ya Polio kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kuanzia Septemba 1 hadi 4 Mwaka huu 2022.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya Mhe @UmmyMwalimu kwenye taarifa yake aliyoitoa leo kwa umma wa Watanzania akiwatangazia kuanza kwa Kampeni ya utoaji wa Chanjo ya Polio kufuatia mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea katika nchi jirani ya Malawi na Msumbiji.

“Sasa tunaelekea kufanya Awamu ya tatu ya Kampeni ya kutoa chanjo ya matone ya Polio ambayo itaanza terehe 1 hadi 4 Septemba, 2022 na zoezi hili litakuwa nchi nzima” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Waziri Ummy amesema kuwa zoezi hilo la utoaji wa matone ya Chanjo ya Polio litafanyika nchi nzima huku kwa Awamu hii ya tatu wakiwa wamelenga kuwafikia watoto 12,386,854 walio chini ya umri wa miaka mitano.

“Shirika la Afya Duniani (WHO) linaelekeza kuwa unapotokea mlipuko au tishio la mlipuko wa Ugonjwa wa Polio nchini, nchi husika na nchi Jirani zipaswa kufanya Kampeni ya kutoa chanjo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa awamu nne mfulilo” amesema Waziri Ummy Mwalimu akifafanua kwa nini zoezi la Chanjo hilo limekuwa likirudiwa mara nyingi.

“Awamu ya kwanza ya kampeni ilifanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Machi 2022 na ilitekelezwa katika Mikoa minne inayopakana na nchi ya Malawi ambayo ni Mbeya, Songwe, Ruvuma na Njombe na kufanikiwa kuchanja watoto 1,130,261 sawa na asilimia 115 ya watoto walio chini ya miaka mitano” amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Amesema Awamu ya pili  ilifanyika nchi nzima kuanzia tarehe 18 hadi 21 Mei 2022 na kuwafikia watoto 12,131,049 sawa na asilimia 118.8.

Waziri Ummy amewasihi na kuwaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa timu za wachanjaji watakapofika katika maeneo yao na kupita kwenye nyumba ili kutoa matone ya chanjo ya Polio kwa watoto walio chini ya miaka mitano.

MAFUNZO KWA VIJANA SEPTEMBA 2 NA 3 MAKUMBUSHO YA TAIFA (POSTA) DAR ES SALAAM YATAKAYOENDESHWA NA TAASISI YA JAKAYA MRISHO KIKWETE NA UNA-TANZANIA

Written By CCMdijitali on Monday, August 29, 2022 | August 29, 2022







Serikali ya awamu ya nane inayakaribisha mashirika ya bima kuja Zanzibar kuwekeza - Dr Mwinyi.




Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema
Serikali ya awamu ya nane inayakaribisha mashirika ya bima kuja Zanzibar kuwekeza kwenye miradi inayoipanga kuitekeleza.
Ameyasema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 44 wa Umoja wa Wanabima Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI),uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Madinat Al Bahr iliopo Mbweni jijini Zanzibar.
Rais Dk.Mwinyi amesema wakati Serikali inafanya mageuzi makubwa ya kiuchumi kuna haja ya sekta ya bima kuwepo kwenye eneo la uwekezaji ili kuwa na kinga katika fedha za miradi hiyo.

📆 29 Agosti, 2022


📍Madinat Al Bahr



28/08/022 JAPAN YATOA DOLA BILIONI 30 KUSAIDIA NCHI ZA AFRIKA

Written By CCMdijitali on Sunday, August 28, 2022 | August 28, 2022

Serikali ya Japan imetangaza kutoa kiasi cha Dola za Marekani bilioni 30 katika kipindi cha miaka mitatu (2022 – 2025) kwa Nchi za Bara la Afrika ili kuziwezesha kutekeleza programu na miradi ya maendeleo itakayoleta mageuzi ya kiuchumi barani humo. 

 

Kiasi hicho cha fedha kimetangazwa kutolewa na Waziri Mkuu wa Japan Mhe. Fumio Kishida wakati wa mkutano wa 8 wa Wakuu wa Nchi na Serikali kati ya Japan na Nchi za Afrika  kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 8 Summit) uliofanyika mjini Tunis nchini Tunisia terehe 27 - 28 Agosti 2022.

 

Kupitia Mkutano huo Mhe. Fumio amezihakijishia nchi za Afrika  kuwa Serikali ya Japan itaendelea kushirikiana nao kwa karibu kwa kuchangia maendeleo kupitia programu na miradi mbalimbali.

 

Mhe. Fumio pia amezihakikishia nchi hizo kuwa Serikali ya Japan itaendelea kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na changamoto zinazokwamisha juhudi za Afrika za kujikwamua kiuchumi. Amezitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kama vile milipuko ya magonjwa, mabadiliko ya Tabia Nchi na upungufu wa chakula.

 

Akizungumzia kuhusu kiasi cha fedha kilichotelewa, Mhe. Fumio amesema kupitia mpango wa TICAD sekta binafsi za pande zote mbili (Japan na Afrika) zimeendelea kustawi, hivyo Serikari yake itaendelea kuhamasisha Kampuni za Japan kuendelea kuwekeza Afrika katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda, kilimo, Afya, nishati ya umeme na teknolojia. 

 

Kuhusu mgawanyo wa fedha hizo Mhe. Fumio amesema kuwa pamoja na TICAD kufanikiwa katika maeneo mengi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya na elimu, Japan katika kipindi cha miaka miatatu ijayo (2022/23-24/25) itaangazia pia maeneo muhimu yanayogusa maisha ya watu ya kila siku. 

 

Ameyataja maeneo hayo kuwa ni mapinduzi ya kijani, Mabadiliko ya tabia nchi, kukuza uwekezaji, kuendeleza hali ya maisha ya Waafrika, ambapo kiasi cha Dola za Marekani bilioni 5 zitatolewa kufanikisha mpango huo. 

Maeneo mengine ni Afya na maendeleo ya rasilimali watu. Katika sekta ya afya Japan itachangia kiasi Dola za Marekani bilioni 1.08 kuiwezesha Afrika kukabiliana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.  Mhe. Fumio aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Serikali yake inatarajia kuwajengea uwezo zaidi ya watu 300,000 kutoka bara la Afrika katika sekta ya viwanda, afya, elimu, sheria na utawala.

 

Akizungumza katika mkutano huo Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameeleza umuhimu wa Bara la Afrika kuendelea kushikirikiana na Jumuiya ya Kimataifa katika kutatua changamoto zinazolikabili bara hilo katika ukuzaji wa uchumi. 

 

Mhe. Mjaliwa akiongelea madhara yaliyo sababishwa na athari za UVIKO 19 na Vita vya Urisi na Ukraine ikiwemo mfumuko wa bei wa bidhaa, ametoa rai kwa Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kushirikiana na nchi za Afrika katika jitihada zake za kujigemea kiuchumi, ili kuhakikisha zinaendelea kutoa huduma bora na muhimu kwa wananchi wake na kuwawezesha wananchi katika shughuli zao zinazowagusa moja kwa moja kama vile kuendeleza kilimo na utalii.

 

Naye Rais wa Tunisia Mhe. Kais Saied ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Mkutano wa TICAD 8, akifungua mkutano huo amesema Japan ni mbia wa kweli wa maendeleo ya Afrika kwa kuwa wakati wote imekuwa mstari wa mbele kushirikiana na Afrika katika kutafuta suluhu ya changamoto zinazolikabili bara hilo, na kuchangia katika kundeleza sekta mhimu kama vile elimu, kilimo, teknolojia, ujenzi wa miundombinu ya uchukuzi na usafirishaji, mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kutoa mikopo yenye riba ndogo na masharti nafuu. 

 

Mkutano wa 8 wa TICAD umehudhuriwa na zaidi ya washiriki 3000 kutoka nchi 55 za Bara la Afrika na Mashirika mbalimbali ya Kimataifa, umebeba kauli mbiu isemayo “Kukuza Maendeleo Endelevu ya Afrika kwa ajili ya Waafrika” (“Promoting Africa-led, African-owned sustainable development”) 




Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) akifuatilia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) unaoendelea mjini Tunis, nchini Tunisia. Waliopo kando yake niNaibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Mbarouk (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba (kushoto)

 



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Rais wa Tunisia Mhe. Kais Saied alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Palais de Congres mjini Tunis nchini Tunisia. 

 




Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Rais wa Tunisia Mhe. Kais Saied wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa TICAD8.

 



Viongozi wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika, Ujumbe wa Serikali ya Japan, watendaji na wawakilishi wa mashirika mbalimbali ya kimataifa walioshiriki mkutano wa TICAD8 wakiwa katika picha ya pamoja. 



MKUTANO WA NANE WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA TICAD (TICAD 8) WAANZA KUFANYIKA MJINI TUNIS, TUNISIA

Written By CCMdijitali on Saturday, August 27, 2022 | August 27, 2022

Mkutano wa 8 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (Tokyo International Conference on African Development – TICAD 8 Summit) umeanza kufanyika leo tarehe 27 Agosti 2022 mjini Tunis, Tunisia. Hii ni mara ya pili kwa mkutano huu kufanyika katika ardhi ya Bara la Afrika tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 baada ya ule wa Kenya (TICAD 6) uliofanyika mwaka 2016. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anawakilishwa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.) katika Mkutano huu. 

Mkutano wa TICAD 8 utafanyika kwa siku mbili tarehe 27 na 28 Agosti 2022; na umetanguliwa na Kikao cha Maafisa Waandamizi wakiwemo Mabalozi wanaoziwakilisha nchi za Afrika nchini Japan, kilichofanyika tarehe 25 Agosti 2022. Pamoja na masuala mengine, Mkutano huu unatarajiwa kukubaliana kuhusu namna ya kuiwezesha Afrika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Dunia ili kuiwezesha kufikia Agenda ya Maendeleo ya Umoja wa Afrika (Agenda 2063). 

Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na janga la UVIKO 19, amani na usalama, mabadiliko ya tabia nchi, upatikanaji mgumu wa malighafi na mfumuko wa bei kwa bidhaa zinazotegemewa na nchi za Afrika kama vile gesi, mafuta na pembejeo za kilimo ambazo ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa Bara la Afrika. 

Agenda 2063 ilikubaliwa na viongozi wa Afrika wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Umoja wa Afrika kwa lengo la kuliunganisha Bara la Afrika katika masuala ya kukuza uchumi; kuhamasisha utawala bora na utawala wa sheria; kuhakikisha maendeleo kwa mtu mmoja mmoja; kuhakikisha amani na usalama unaimarika na kuiweka Afrika katika nafasi ya mchangiaji mkuu wa uchumi duniani

Mhe. Kassim Majaliwa katika mkutano huu anatarajiwa kuwa na mazungumzo ya pembezoni na Waziri Mkuu wa Japan, Mheshimiwa Fumio Kishida na watendaji wakuu wa kampuni na taasisi za Japan ikiwemo Shirika la Maendeleo la Japan (JICA); Kampuni ya Mitsubishi; Bodi ya Japan Tobacco Inc (JT Group); na Taasisi ya Japan inayojishughulisha na masuala ya Uchumi na Maendeleo ya Afrika (Association of African Economy and Development - AFRECO). 

Tangu kuanza kufanyika kwa mikutano ya TICAD, Japan imekuwa ikiongeza kiasi cha fedha za mkopo wa masharti nafuu na msaada katika kuchangia maendeleo ya Afrika kutoka Dola za Marekani bilioni 0.6 kwa mwaka 1993 (TICAD 1) hadi kufikia Dola za Marekani bilioni 20 kwa mwaka 2019 (TICAD 7). Kwa upande wa Tanzania misaada na mikopo ya masharti nafuu kutoka Japan imesaidia katika utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, maji, afya, nishati ya umeme, kilimo na elimu.

Ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Japan unazingatia mwongozo wa Agenda ya Umoja wa Mataifa ya Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu inayojikita kwenye kupunguza umasikini na kukuza maendeleo. Japan ni miongoni mwa washirika wakubwa wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania kupitia JICAkuanzia mwaka 1962. Tanzania ni nchi pekee inayoshirikiana na Japan katika maeneo matatu ya ushirikiano yaliyopewa kipaumbele na nchi hiyo ikiwemo, ushirikiano katika misaada na mikopo ya kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo; ujuzi na uzoefu kupitia program ya wajapani ya kujitolea chini ya Japan Overseas Cooperation Agreement; na fursa za mafunzo na masomo


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) akifuatilia Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) unaoendelea mjini Tunis, nchini Tunisia.



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Tunisia Mhe. Najla Bouden alipowasili katika uwanja ndege wa kimtaifa wa Carthage mjini Tunis nchini Tunisia kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Nane wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kimataifa  kuhusu Maendeleo ya Japan na Afrika (TICAD 8) ulio anza kufanyika leo tarehe 27 Agosti 2022



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Tunisia Mhe. Najla Bouden alipowasili mjini Tunis, Tunisia.



WAZIRI MULAMULA APOKEA BARUA ZA UTAMBULISHO MKURUGENZI MKAZI UNAIDS

Written By CCMdijitali on Tuesday, August 23, 2022 | August 23, 2022



Taarifa kwa Umma kuhusu kuanza kwa vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge

Taarifa kwa Umma kuhusu kuanza kwa vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge 




Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia Taifa kuhusu Sensa ya Watu na Makazi , Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Written By CCMdijitali on Monday, August 22, 2022 | August 22, 2022


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akilihutubia Taifa kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwenye shughuli ya uandikishaji wa Sensa ya Watu na Makazi Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Agosti 2022.

TANZANIA, OMAN KUONGEZA MAENEO YA USHIRIKIANO



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa Oman nchini Mhe. Saudi Hilal Al Sidhani katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa Oman nchini Mhe. Saudi Hilal Al Sidhani katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahesabiwa kwenye Zoezi la Sensa na Makazi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Karani wa Sensa Phausta Ntigiti wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi. 



Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan azungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya Kuhesabiwa katika shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 katika shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi. 



UMITASHUMTA Yaenda Sambamba na SensaBika

Written By CCMdijitali on Thursday, August 4, 2022 | August 04, 2022

Na Shamimu Nyaki - WUSM

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema wizara hiyo imebuni Kampeni maarufu kwa sasa nchini ya SensaBika ambayo lengo lake ni kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi mwaka huu 2022.

Dkt. Abbasi ameeleza hayo Agosti 04, 2022 Tabora katika Ufunguzi wa Mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA ambapo amesema kuwa, wizara hiyo ndio nguvu shawishi ya Taifa pamoja na kutoa furaha kwa watanzania, imeanzisha Kampeni hiyo kutokana na wadau wake wengi kuwa na ushawishi katika jamii ambao wataweza kuhamasisha watanzania kushiriki zoezi la Sensa.


"Sisi ni wizara ya kutoa furaha na kupitia sekta zetu tuna wadau wengi ambao wakitumia Kampeni hii kupitia umaarufu na ushawishi walionao kwenye jamii itarahisisha kufikisha ujumbe kwa haraka zaidi kwa jamii kushiriki Sensa", amesema Dkt. Abbasi.

Dkt. Abbasi ametumia nafasi hiyo kumuongoza Mgeni Rasmi, Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa pamoja na Viongozi, Wanamichezo na Wananchi waliohudhuria ufunguzi huo kucheza kibwagizo maarufu sana nchini cha SensaBika.




















Michezo ya UMITASHUMTA Yawakutanisha Wanafunzi Zaidi ya 3000

Na Shamimu Nyaki - WUSM

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amesema mashindano ya michezo kwa shule za Msingi (UMITASHUMTA) mwaka 2022 yameshirikisha Wanafunzi zaidi ya 3000 kutoka Mikoa 26 ya Tanzania Bara na miwili kutoka Zanzibar.

Ameyazungumza hayo leo Agosti 4, 2022 mkoani Tabora katika hafla ya Uzinduzi wa mashindano hayo yaliyofanywa na Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania.
Prof. Shemdoe ameeleza kuwa wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo Wana vigezo na wameandaliwa vizuri kuanzia ngazi ya shule.

"Mashindano haya yalianza mwaka 2000 ambapo lengo lake ni kukuza vipaji vya Wanafunzi na kuimarisha upendo, ushirikiano na kuboresha afya kwa Wanafunzi", amesema Prof. Shemdoe.

Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuendesha shughuli za michezo nchini.

Mashindano ya UMITASHUMTA yatahitimishwa Agosti 08 mwaka huu na Agosti 9,2022 yataanza mashindano ya UMISSETA.
Mwisho






 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link