NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

VITABU 16 VYAPIGWA MARUFUKU KUTUMIKA SHULENI, TAASISI ZA ELIMU

Written By CCMdijitali on Monday, February 13, 2023 | February 13, 2023

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imepiga marufuku matumizi ya vitabu 16 vinavyokwenda kinyume na maadili kwenye Shule na Taasisi zote za Elimu.

Vitabu hivyo vimepigwa marufuku na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 59 cha Sheria ya Elimu Sura ya 353.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dodoma  Prof. Mkenda amesema kama taifa tuna mila na desturi za  kufuata na katika kufundisha na kulea watoto na kwamba shule zina wajibu wa kuendana na taratibu hizo katika kuwaandaa watoto.

"Nahimiza wazazi mkague mabegi ya wanafunzi kuhakikisha vitabu hivi havitumiki nyumbani; ukaguzi na ufuatiliaji huu ni endelevu ili kubaini kama vitabu kama hivi hipo katika shule tuweze kichukua hatua,"amesema Profesa Mkenda

Amevitaja vitabu hivyo kuwa ni Diary of a Wimpy Kid, Diary of a Wimpy Kid -Rodrick Rules, Diary of Wimpy Kid - The Last Straw, Diary of Wimpy Kid-Dog Days, Diary of a Wimpy Kid The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid -Cabin Fever, Diary of a Wimpy Kid - The Third Wheel na Diary of a Wimpy Kid - Hard Luck.

 Vingine ni Diary of a Wimpy Kid - The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid -Old School, Diary of a Wimpy Kid -Double Down, Diary of a Wimpy Kid-The Gateway,  Diary, Diary of a Wimpy Kid-Diper Overlode, Is for TANSGENDER ( you know best who you are!), Is for LGBTQIA ( find the words that make you you) na Sex  Education a Guide to life.

Prof. Mkenda ametoa rai kwa watanzania kupiga namba 0262160270 ya mezani na 0737 962965 ya mkononi ili kutoa taarifa ya uwepo wa vitabu hivyo shuleni na kwamba hatua kali zitachukuliwa kwa shule  yoyote itakayokutwa na vitabu hivyo ikiwemo kufutiwa usajili. 

@ikulu_mawasiliano @ikulu_habari @wema.smz2020 @shuledirectkids @shuledirect @maelezonews @maelezozanzibar

DKT.DIMWA- ATOA MKONO WA POLE KWA FAMILIA YA MAREHEMU TAKRIMA.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar, Dkt.Mohammed Said Mohammed (Dimwa), ametoa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg.Hassan Mussa Takrima aliyefariki juzi nyumbani kwake Fuoni baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Dkt.Dimwa, akizungumza na familia hiyo amesema Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa kifo cha Mwanasiasa na kada  huyo.

Amesema Chama na Serikali wamepoteza mtu muhimu aliyekuwa ni kiongozi na mwalimu aliyebobea katika masuala ya sisasa na uongozi.  

Katika maelezo yake Dkt.Dimwa, amesema marehemu Takrima alikuwa ni kiongozi muadilifu na mchapakazi aliyefanya kazi kwa ufanisi ndani ya Chama na Serikalini.

“Natoa pole kwa familia ya marehemu, tulipata taarifa za kifo chake wakati mimi nikiwa katika ziara ya kujitambulisha Kisiwani Pemba na niliporudi tu nikaona nije kuwapa pole kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi.

Kama mnavyojua kuwa Mzee wetu Takrima alikuwa ni mtu muhimu sana kutokana na uhodari wake wa kiutndaji ametufundisha mambo mengi katika uwanja wa siasa pamoja na utendaji serikalini.”, alisema Dkt.Dimwa.

Pamoja na hayo aliwasihi wanafamilia hao kuendelea kuwa na subra na uvumilivu katika kipindi chote cha kuombeleza msiba huo.

Marehemu Takrima, alizaliwa mwaka 1943 katika kijiji Mwaleni ya Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja na alipa elimu ya msingi na Sekondari katika skuli ya Makunduchi na mafunzo ya Ualimu katika Chuo cha Nkurumah na Nchini Uingereza.

Aidha marehemu Takrima, enzi za uhai wake amewahi kushika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Mkuu wa Wilaya ya Ngara,Mkuu wa Wilaya ya Kusini Pemba,Mkuu wa Mkoa Kusini Pemba na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi “B”.

Kwa upande wa Chama amewahi kuwa mjumbe wa NEC na mwaka 1998-2000 alishika nyadhifa ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar na Mkuu wa Idara Makao Makuu Dodoma.

Dkt.Dimwa, alifuatana na Viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar  Khamis Mbeto Khamis, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM Zanzibar Khadija Salum Ali, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Omar Ibrahim Kilupi na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Taifa Dogo Idd Mabrouk.

Akizungumza kwa niaba ya familia ya marehemu  Omar Saleh, alimshukru Naibu Katibu Mkuu Dkt.Dimwa kwa kuwafariji.

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar, Dkt.Mohammed Said Mohammed (Dimwa), akitoa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar marehemu Hassan Mussa Takrima, aliyefariki juzi nyumbani kwake Fuoni Zanzibar.

MWISHO

RAIS DK.MWINYI ASISITIZA UHARAKA WA UANZISHWAJI MAHKAMA YA RUSHWA NA UHUJUMU UCHUMI ZANZIBAR

Zanzibar, 13 Febuari, 2023

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imezitaka taasisi za umma kubadili mifumo ya zamani ya utendaji na utoaji huduma kwa wananchi kwa kuanzisha mifumo ya kisasa ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kurahisisha utendaji wao kuenda na kasi ya matumizi ya teknolojia.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo kwenye maadhimisho ya siku ya Sheria, Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema wakati huu wa sayansi na teknolojia mifumo ya uendeshaji taasisi kwa kutumia karatasi na kalamu imepitwa na wakati, hivyo alizitaka taasisi za umma zikiwemo taasisi za sheria na wadau wake kubadili mifumo ya utendaji wao ili kuendana na kasi ya teknolojia.

Alisema matumizi ya TEHAMA hurahisisha utendaji na kuondosha usumbufu pia kusaidia jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa nchi na kuimarisha ustawi wa jamii kwa kuokoa fedha nyingi zinazogharamia shughuli zinazotekelezwa kwa mifumo ya zamani na badala yake gharama ya fedha hizo zitaelekezwa kwenye shughuli nyengine za maendeleo.

Akizungumzia haki mtandao Mahakamani, Rais Dk. Mwinyi alisema ni muhimu kwa ujenzi wa taasisi bora za kisheria kwani mfumo unaendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanayotokea duniani.

Hata hivyo, aliipongeza Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mara ya kwanza kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa kusajili mawakili ambao alieleza kwa sasa watafungua mashauri na kufuatilia uendeshaji wa mashauri hayo wakiwa nyumbani, vijijini au Ofisini.

Alisema mfumo huo wa kisasa utasaidia kuokoa muda unaotumika kwenye taasisi za sheria kufanyia kazi nyengine za kuinua vipato vyao, kuimarisha uwazi, uwajibikaji, utawala bora, ukusanyaji mzuri wa mapato na kuimarisha uchumi wa nchi pamoja na kusaidia kukuza imani ya wananchi na wawekezaji wa ndani na nje kwenye vyombo vya sheria.

Akizungumiza faida za matumizi ya TEHAMA kwenye taasisi za Sheria, Dk. Mwinyi alisema usikilizaji wa haraka wa mashauri na kutolewa maamuzi, upatikanaji wa takwimu sahihi, ufuatiliaji bora na usimamizi bora wa mashauri.

“Kwa kupitia haki mtandao, hakutakuwa na ulazima kwa Waheshimiwa Majaji wa Mahkama Kuu kusafirishwa kwenda Pemba kusikiliza mashauri, kwani mashauri hayo yatasikilizwa na kuamuliwa kwa mfumo wa Tehama tuu, Shahidi hatalazimika kufika kwenye jengo la mahakama kutoa ushahidi, inaweza kuandaliwa mifumo ya kutoa ushahidi wake kupitia hata simu yake tu ya mkononi, utaratibu huu mienendo ya kesi itapatikana kwa haraka” alifafanua Dk. Mwinyi.

Rais, Dk. Mwinyi aliahidi kutoa kipaumbele kwa bajeti ya matumizi ya Tehama kwa mahakama kuu Zanzibar ili kuimarisha miundombinu ya taasisi za sheria nchini, na kusema kwamba Serikali itatumia zaidi ya bilioni nne kwa ujenzi wa Majengo manne ya Mahakama kuu na za wilaya kwa Unguja na Pemba ambazo zinaendana na mifumo ya Tehama. Aidha, aliitaka mahakama hiyo kupitia taasisi zake kujipanga na kuwasilisha Serikalini mpangokazi na bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa adhma hiyo.

Pia alitoa wito kwa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora kupitia Ofisi ya Wakala wa Serikali Mtandao kuzisimamia na kuzishauri ipasavyo taasisi zote za sheria katika kufikia lengo hilo la haki mtandao nchini.

Hata hivyo, aliiataka Mahakama kushirikiana na wadau wengine wa haki kwa maboresho yoyote kwenye mhimili wa Mahkama alisema yataleta matokeo chanya yenye ufanisi kwa ushirikiano imara na wadau.

Akizungumzia uanzishwaji wa Mahkama Maalum ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Rais Dk. Mwinyi alisifu jitihada zilizofikiwa na Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa hatua waliyofikia na kueleza kufarajika kwake kusikia tayari wameunda kamati ya wataalamu kwaajili ya kusimamia na kuratibu mchakato wa kuanzishwa Mahakama hiyo.

Alieleza Kuanzishwa kwa mahkama hiyo, kutaisaidia Serikali mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya Ofisi na rasilimali za umma ambayo huzorotesha uchumi wa nchi na ustawi wa jamii hali aliyoieleza inarejesha nyuma juhudi za Serikali za kuwaletea wananchi maendeleo.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Jaji Mkuu wa Mahakama kuu Tanzania, Prof. Ibrahim Juma alisema karne ya 21 inazitaka taasisi zote na watendaji wake kuwa na mabadiko ya fikra na kimtazamo yanayoendana na teknolojia iliopo duniani, nakuongeza kuwa mabadiliko ya teknolojia kwenye Mahakama Kuu ya Zanzibar yatasaidia utoaji wa haki na kukuza uchumi wa Zanzibar kwa kuleta mageuzi makubwa ya mabadiliko ya utendaji wao. Hivyo, aliwataka majaji kutumia jitihada za ziada ili kuendana na kasi ya huduma mtandao kwa sasa.

Naye, Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla, alisema maadhimisho ya siku ya sheria ni kuanza mwaka mpya wa mahakama na kueleza miongoni kwa mikakati ya mabadiliko yao kwenye ufanisi wa utendajikazi wao ni kuwafikia wananchi kwa haraka, kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi na kuwa karibu nao kwaajili ya kuwahudumia pamoja na kutoa mahakama rafiki zenye huduma za haraka.

Madhamisho ya Sheria yaliambatana na wiki ya sheria iliyoanza Febuari 06 mwaka huu kwa kutekelezwa shughuli mbalimbali za kisheria ikiwemo kutoa elimu kwa umma juu ya masuala ya sheria, kutambua mchango wa makaadhi kwa kutunukiwa vyeti vinara bora watoaji haki, kupokea mawakili wapywa, kuzindua mfumo wa kuwasajili mawakili kwa njia ya mtandao pamoja na kuhitimishwa kwa matembezi yaliyoandaliwa na taasisi ya “Zanzibar Maisha bora Foundation” yaliyoongozwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Mama Mariam Mwinyi yakiwa na kauli mbiu “Kupinga vita dhidi ya Udhalilishaji wa kijinsia.”

Aidha, maadhimisho ya Sheria pia yalihudhuriwa na ujumbe kutoka Mahakama kuu ya Tanzania ulioongozwa na Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Juma yalikua na kaulimbiu, “Haki mtandao ya kukuza uchumi na Ustawi wa jamii” ni maadhimisho ya 12 tokea kuanzishwa kwake mwaka 2012.

IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR

Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link