NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

Wanaobeza huduma ya umeme vijijini watakiwa kupuuzwa

Written By CCMdijitali on Tuesday, December 30, 2014 | December 30, 2014

Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO

Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO amewataka wananchi Wilayani SERENGETI mkoani MARA, kuwapuuza watu wanaohujumu mradi wa Umeme vijijini unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa huo.

Akizungumza na baadhi ya wananchi wa kijiji cha GANTAMOME wilayani humo, Profesa MUHONGO amesema baadhi ya watu wamekuwa wakiwahadaa wananchi kuwa utekelezaji wa mradi huo hautafanikiwa kama ilivyokusudiwa na Serikali jambo ambalo linalenga kuwanyima fursa wananchi wa vijijini upatikanaji wa nishati ya umeme .

Nalo shirika la Umeme nchini TANESCO limewatahadharisha wananchi kutowapa fedha watu wasio waaaminifu ili kugharamia mradi huo wa nishati ya umeme vijijini.

MH. LOWASSA AMTEMBELEA SUKWA SAID SUKWA,ZANZIBAR

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akisalimiana na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea kwa ajili ya kumjulia hali, nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea skukuu ya Krismasi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akiwa katika mazungumzo na Katibu mkuu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana. Mh. Lowassa alikuwa Zanzibar kwa mapumziko ya kusherekea sikukuu ya Krismasi. Kushoto ni Mke wa Sukwa, Fatma
Mussa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Katibu wa Zamani wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sukwa Said Sukwa alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Mpendae, mjini Unguja jana.

Balozi Seif awatakia kheri ya mwaka mpya wazee hapa Nchini

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Asili wa Ijumaa Micheweni Mjini  Sheikh Haji Khatib Haji.
Balozi Seif akitoa Mkono wa Pole kwa Watoto na Wajukuu wa Muasisi wa Afro Shirazy Party Marehemu Bibi Ashura Abeid hapo Nyumbani kwa Tibirinzi Chake chake Pemba.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mzee Khamis Mkadara Khamis wakati alipokwenda kumkagua na kumtakia kheir ya Mwaka Mpya wa 2015.
Mzee Bakari Khamis Kombo wa Kijiji cha  Micheweni akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kumjulia hali na kumtakia kheri ya mwaka mpya wa 2015.
 Balozi Seif akimsalimia mzee  Khamis Othman Kapona wa Kijiji cha Chekea Mtambwe alipokwenda kumtembelea na kujua hali yake pamoja na kumpa kheri ya mwaka mpya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimtakia kheri ya mwaka mpya wa 2015  Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jimbo la Micheweni Mzee Kombo Fundi Kombo wakati alipomtembelea na kujua hali yake.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Balozi Seif Ali Iddi ampa pole Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano

Written By CCMdijitali on Monday, December 29, 2014 | December 29, 2014

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimpa pole Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Profesa Ulpiano Nyumbani kwake Vuga Mjini Zanzibar baada ya kuvamiwa na majambazi jana usiku yeye na wenzake maeneo kati ya Kikwajuni na SUZA.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Mke wa Kiongozi wa Madaktari wa Cuba Dr. Ulpiano mara baada ya kuwapa pole kutokana na mtihani uliowapatya wa kuvamiwa na Majambazi.
Kati kati yao ni Dr. Barbara nyuma ya Balozi Seif ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA } Dr. Idrissa Rai.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na Madarkati wa Cuba hapo nyumbani kwao Vuga alipokwenda kuwafariji na kuwapa pole baada ya kuvamiwa na Majambazi.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


Press Release:-


Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi Msaidizi Kamishna wa Polisi { ACP } Mkadam Khamis Mkadam alisema Jeshi la Polisi Mkoa huo linawashikilia watu wawili miongoni mwa majambazi wanaotuhumiwa kuhusika na uvamizi wa Madaktari Bingwa wa Cuba katika maeneo kati ya Kikwajuni Wireles na Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar {SUZA } mapema jana usiku.

Alisema polisi ilianza uchunguzi mara moja baada ya kupata taarifa ya kuvamiwa kwa Madaktari hao walionyang’anywa mikoba,vitu pamoja na Fedha zao ambapo mmoja kati yao Profesa Ulpiano alijeruhiwa kwa panga kichwani.

Kamishna Msaidizi wa Polisi { ACP } Mkadam Khamis Mkadam alieleza hayo wakati Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika nyumbani kwa Madaktari hao Vuga Mjini Zanzibar kuwafaribi baada ya kupatwa na mkasa huo.

Kamanda Mkadam alisema Mkoa wa Mjini umekuwa na matukio ya kuibuka kwa vitendo vinavyoashiria kuichezea amani baadhi ya wakati jambo ambalo jamii inahusika kwa kiasi kikubwa katika kushirikiana na Jeshi la Polisi kukabiliana na vitendo hivyo.

Alisema ulinzi ni jukumu la watu wote, hivyo miundo mbinu iliyopo hivi sasa Duniani ya mitandao ya mawasiliani katika uwekaji wa Kamera za CCTV inahitajika kutumika kwa lengo la kuwabaini watu wanaojihusisha na matendo maovu.

Kamanda huo wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi alizishauri Taasisi za Umma, Binafsi na hata watu wa kawaida wakakijengea utamaduni wa kutumia mfumo huo mpya ili kuwa na maisha ya salama.

Akiwapa pole Madaktari hao Bingwa wa Cuba wanaotoa huduma katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na kusomesha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar { SUZA } Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hilo ni tukio la ajabu na la kusikitisha katika visiwa vya Zanzibar.

Balozi Seif alisema vitendo hivyo viovu vinavyofanywa na baadhi ya wahuni vimekuwa vikileta sura mbaya kutokana na sifa ya Zanzibar yenye Utamaduni wa kistaarabu wa kupenda wageni tokea karne nyingi zilizopita.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Madaktari Bingwa hao wa Cuba kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo vyake vya ulinzi inaendelea na uchunguzi wa kina na wahusika wa vitendo hivyo watapopatikana mkondo wa sheria utafanya kazi zake dhidi ya wahalifu hao.

Balozi Seif aliwataka Madaktari hao kuendelea na majukumu yao kama kawaida na Serikali itakuwa makini katika kuwahakikishia usalama wao pamoja na wageni wengine wakati wao wote wawapo hapa Nchini.

Wakitoa shukrani zao kwa faraja hiyo pamoja na juhudi zilizochukuliwa na vyombo vya ulinzi katika kuwasaka wahalifu waliohusika na tukio hilo Madaktari hao wa Cuba waliahidi kuendelea kutoa huduma kama kawaida licha ya mkasa uliowakumba.

Madaktari hao walielezea matumaini yao kwamba Serikali pamoja na vyombo vyake vya ulinzi vitafanya juhudi za ziada katika kuona kwamba matukio kama hayo yanadhibitiwa kabisa.
Madaktari hao wanne wa Cuba ni Dr. Barbara, Dr. Daisy Batle, Dr.Katia wakiwa na Kiongozi wao Profesa Ulpiano walivamiwa ghafla na vijana walioshuka na mapanga kwenye Gari aina ya Noah wakati wakitokea Kikwajuni kuelekea nyumbani kwao Vuga.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar


NAIBU WAZIRI MWIGULU NCHEMBA MGENI RASMI TAMASHA LA UPENDO WA MAMA DAR

Written By CCMdijitali on Saturday, December 27, 2014 | December 27, 2014


Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akizungumza.

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima.

Injinia Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam. Na Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha.

Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na waimbaji wengine wengi.

"...Washiriki kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake maalum, ambayo atamkabidhi wakati itakapotangazwa...kutakuwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi.

Akifafanua zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni litakapofungwa.

Aisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika familia zao.

Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Alisema baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali.

Aidha aliongeza tamasha kama hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.

Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif atembelea Tawi la CCM.

Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif akipandisha Bendera ya CCM Mbele ya Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina kabla ya kuweka jiwe la msingi la Twi hilo.
 Balozi Seif  ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM akiweka jiwe la msingi la Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Tawi la CCM  Mombasa  kwa Mchina Nd. Ahmada Yahya Abdulwakil akitoa ufafanuzi wa ujenzi mbele ya Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif mara baada ya kuweka jiwe la Msingi la Tawi hilo.
 Wanachama wapya 79 wa CCM na Jumuiya zake wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina wakila liapo mara baada ya kukabidhiwa kadi na Mlezi wa CCM Mkoa wa Magharibi Balozi Seif Ali Iddi.

Mlezi wa CCM Mkoa wa Maghribi Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na uongozi mzima wa Tawi la CCM Mmobasa kwa Mchina, Wilaya ya Dimani na Mkoa wa Magharibi mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi hilo.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


Press Release:-

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema wimbi la vijana wa vyama vya upinzani kuamua kuvihama vyama hivyo na kujiunga na CCM ni dalili za umadhubuti  wa chama hicho unaoonekana kuimarika kila wakati.

Alisema chama cha Mapinduzi chenye sera  na ilani imara inayokiwezesha kushinda kila baada ya miaka mitano tokea kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania ndio kimbilio la watu wote wenye busara ya kutaka kujiunga na ulingo wa siasa.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mlezi wa Mkoa wa Magharibi Kichama alisema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi Mombasa kwa Mchina Wilaya ya Dimani Mkoa wa Magharibi.

Alisema makundi ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanaoamuwa wenyewe kuvihama vyama vyao na kujiunga na Chama cha Mapinduzi ni muelekeo wa ishara kwa CCM kuendelea kuongoza dola katika uchaguzi  Mkuu ujao wa mwaka 2015.

Hata hivyo Balozi Seif aliwatahadharisha Viongozi na Wanachama wa CCM wasikae na kubweteka na mawazo ya kushinda uchaguzi bila ya sera na mikakati ya kujipanga vyema kwa ajili ya ushindi huo.

Aliwaomba wana CCM popote pale walipo nchini Tanzania kuendelea kushikamana na kuacha majungu, fitna na makundi ili  ushindi uwe rahisi zaidi ya chaguzi zote zilizopita za mfumo wa vyama vingi hapa Nchini.

Balozi Seif aliupongeza Uongozi, wanachama na  wapenzi wa chama hicho waliojitolewa kwa nguvu zao na kuhakikisha kwamba ujenzi wa Tawi la Mombasa kwa Mchina unasimama imara.

Alisema licha ya kuungwa mkono na wapenzi na watu tofauti katika ujenzi wa Tawi hilo lakini nguvu za ukamilishaji wa tawi hilo zitaendelea kubakia mikononi mwa Viongozi pamoja na Wanachama wenyewe wa Tawi hilo.

Aliutaka uongozi wa Mkoa wa  Magharibi kuwa na tahadhari ya uvamizi wa makaazi unaofanywa na baadhi ya watu kwa lengo maalum la kuongeza nguvu za  kuimarisha vyama vya kisiasa katika kujiandaa kwa uchaguzi Mkuu ujao.

Balozi Seif akiwa pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar   aliwakumbusha masheha na Wakuu wa Wilaya  nchini kuendelea kufuata sheria za nchi ipasavyo ili kila mwenye haki yake anapata fursa  bila ya vikwazo,ubaguzi wala itikadi za kisiasa.

Alisema tabia ya baadhi ya watu zaidi wana siasa kushindikiza masheha kutoa vibali  kwa wafuasi au vijana wao kwa kutaka kupatiwa vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi wakati muda wa ukaazi wa vijana hao haujatimia ni kuvunja sheria za nchi.

“ Suala hili la kutishwa masheha na kulaumiwa Wakuu wa Wilaya nililikemea nilipokuwa katika ziara yangu wiki hii Kisiwani Pemba. Na hapa nalirejea tena kwa kuwakumbusha masheha na wakuu hao wa Wilaya kufanya kazi zao kwa kujiamini “. Alisema Balozi Seif.

Aliwataka na kuwaasa vijana kujiepusha na ushawishi huo wa wana siasa wa kutaka kuwalazimisha kufanya mambo yaliyo kinyume na sheria na utaratibu wa Nchi.

Katika kuunga mkono ujenzi wa Tawi hilo la Mombasa Kwa mchina Mlezi huyo wa Mkoa wa Magharibi Kichama Balozi Seif aliahidi kukamilisha ukumbi wa Tawi hilo kwa kutoa mchango wa Jipsam, taa ,mafeni yote ukumbini hapo pamoja na kusaidia  Seti moja ya Jezi kwa Timu kati ya timu 16 zilizomo ndani ya Tawi hilo .

Mapema akitoa Taarifa fupi ya ujenzi wa Tawi hilo Mwenyekiti wa Ujenzi ambae pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM  Nd. Ahmada Yahya Abdulwakil  alisema ujenzi huo ulioanza rasmi Tarehe 28 Septemba 2013 umekuja kufuatia wanachama hao kukosa ofisi ya kufanyia kazi  zao za Kisiasa.

Nd. Ahmada alisema tawi hilo lenye ofisi zote zinazohitajika zikiwemo za jumuiya za chama litakuwa na huduma za kisasa zinazokwenda na wakati  pamoja na ukumbi wa Mikutano ambao utakodishwa kwa shughuli za kijamii ili kuliongezea mapato Tawi hilo.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ujenzi wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina aliwashukuru viongozi na wapenzi wote wa chama hicho waliojitolea kuunga nguvu katika ujenzi wa Tawi hilo lenye hadhi ya chama chenyewe.

Katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi la Tawi la CCM Mombasa Kwa Mchina Balozi Seif alikabidhi kadi kwa wanachama wapya  79 wa chama cha Mapinduzi pamoja na Jumuia zake wa Tawi hilo.

Ujenzi wa  Tawi la Chama cha Mapinduzi Mombasa kwa Mchina  hadi sasa umeshagharimu zaidi ya shilingi Milioni 45,100,000/- .


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

27/12/2014.
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link