Home » » Feruz Bano atangaza matokeo ya kura za maoni Jijini Arusha leo.

Feruz Bano atangaza matokeo ya kura za maoni Jijini Arusha leo.

Written By CCMdijitali on Sunday, August 2, 2015 | August 02, 2015


  • Baada ya kupokea matokeo ya kura za maoni kutoka katika Matawi yote Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini ,ameatangaza hadharani matokeo hayo, baada ya kuzijumlisha, kwa mujibu wa Kanuni za uteuzi wa Wagombea wa CCM Kuingia katika Vyombo vya Dola.

  • Aidha mara baada ya matokeo hayo kutangwazwa, Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kimekutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo.

Viva CCM vivaaaaaaaaaaaa.........
CCM 2015 ni Imara Kuliko Jana !!!

KATIBU wa CCM Wilaya ya Arusha  Feruz Bano akitangaza matokeo ya kura za maoni katika Makao Makuu ya CCM Wilaya ya Arusha leo.Kuli ni Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua.

KATIBU wa CCM Wilaya ya Arusha  Feruz Bano ametangaza matokeo ya kura za maoni kufuatia uchaguzi uliofanyika jana kote nchini ambapo katika jimbo la Arusha  Mjini mfanyabiashara anayeendesha kinu cha kusagisha nafaka cha NMC na kamanda wa vijana mkoa wa Arusha Philemon Mollel ametangazwa mshindi kwa kupata kura 5320 kati ya kura zilizopigwa.

Katika uchaguzi huo uliokuwa na wagomea 12 pia alitangazwa ikichukuliwa na mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite Justine Nyari kwa kupata kura 1894 huku mtumishi wa benki kuu ya Tanzania Dk.Mosses Mwizarubi akiibuka  mshindi wa tatu  kwa kupata kura 1005 .

Nafasi ya nne imechukuliwa na mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite Thomas Munis ambaye aliweza kujipatia kura 832 huku manasheria wa kujitegemea Victor Njau akipata kura 752 akifuatiwa na mwandishi wa habari wa kujitegemea Swalehe Kiluvia.

Naye mfanyabishara wa utalii mwenye asili ya Kiasia na mzaliwa wa Zanzibar Ndg Mustafa Panju akiibuka katika nafasi ya saba kwa kupata kura 428 akifuatiwa na Hamis Migire ambaye ni mfanyabiashara ya utalii na mmiliki wa vituo vya mafuta jijini Arusha aliyepata kura 305.

Kada mwingine ni wakili wa kujitegemea Edmund Ngemela aliyepata kura 198 huku kada Mahamod Omar akipata kura 176 na Reuben Mweteni akipata kura 171huku Emanuel Ole Njoro akishikilia mkia katika kinyang’anyiro hicho.

Akizungumza mara baada ya matokeo hayo kutangazwa Justine Nyari alisema kuwa ameridhika na matokeo hayo na kwamba ana imani na vikao vya chama vinavyoendelea kufanyika kuwa vitatoa jina la mgombea ambaye atapeperusha bendera ya CCM

Kwa upande wake Phiilemon Mollel alisema anawashukuru wana CCM waliompa ushindi wa kushindi kuwatumikia kwa dhati ambapo pia alikahidi  kuwa  atashirikiana na wagombea wenzake ili kuhakikisha ushindi wa chama unapatikana na kuijenga arusha mpya.

Pia alisema ahana wasiwasi na vikao vya juu vya chama kwakua anaamini vitatenda haki na kurejesha jina lake kwakua yeye pia alitenda haki katika kinyang’anyiro chote.

Naye Mustafa Panju alisifu mchakato mzima tangu mikutano ya kura za maoni na kwamba bado anaahidi kushirikiana vyema na wagombea wote na yule atakayepitishwa na vikao vya juu ili kuhakikisha nchi na chama vinaboreka kwakua si kwaajii ya mtu binafsi.

Hata hivyo katika hali isiyotegemewa wagombea wengine hawakuweza kutokea wakati wa kutangazwa kwa matokeo hali ambayo ilizua maswali mengi lakini katibu wa CCM wilaya Ferooz Bano alisisitiza wagombea wake wote wako wamoja na watashirikiana kama walivyokubaliana wakati wa mchakato wa kura za maoni ili kukihakikisha chama kinashinda.

Hata hivyo katibun Bano alisema hakuna mgombea yeyote wala wapambe wao waliokamatwa kwa vitendo vyovyote vya rushwa lakini alikiri kuwepo kwa kesi katika kituo cha kati kuhusu viongozi wawili wa chama ngazi ya kata ya kati kwa kukutwa na karatasi za kura zilizowekewa alama ya vema kwenye majina ya mmoja wa wagombea udiwani katika kata hiyo.

Viongozi hao ni katibu kata Ally Meku na Yakubu Mkindi ambaye ni katibu wa tawi la Bondeni.
NA LILIAN JOEL

Mfanya biashara maarufu Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Makampuni ya Arusha Trade Centre, JN Minning, Arusha Gem Trade na Arusha Parking System zote za Jijini Arusha na Kimataifa, Ndg Justin Nyari akiwasili katika viwanja vya Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilayani Arusha , kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo
Mfanya biashara maarufu Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Makampuni ya Arusha Trade Centre, JN Minning, Arusha Gem Trade na Arusha Parking System zote za Jijini Arusha na Kimataifa, Ndg Justin Nyari akiwasili katika viwanja vya Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilayani Arusha , kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo


Mfanya biashara maarufu Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Makampuni ya Arusha Trade Centre, JN Minning, Arusha Gem Trade na Arusha Parking System zote za Jijini Arusha na Kimataifa,Ndg Justin Nyari, akiongea na waandishi wa habari , mara baada ya kutangwazwa kwa kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo









Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Bush Buck Safaris Ndg Mustapha Panju, akiongea na waandishi wa habari , mara baada ya kutangwazwa kwa kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo.


 Dk  Mosses Mwizarubi au kwa jina maarufu Dr Mwiza au Nabii Mwiza (katikati ) akiwa amefuatana na Mkewe ,wakiongea na Mwandishi wa Gazeti la UHURU Jijini Arusha Ndg Shaabani, wakati walipowasili katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha leo, kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jini Arusha leo.
Mfanyabiashara anayeendesha kinu cha kusagisha nafaka cha NMC na Kamanda wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha Philemon Mollel akiwasili katika viwanja vya Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilayani Arusha , kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo

Mfanyabiashara anayeendesha kinu cha kusagisha nafaka cha NMC na Kamanda wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Arusha Philemon Mollel na Mfanya biashara maarufu Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Makampuni ya Arusha Trade Centre, JN Minning, Arusha Gem Trade na Arusha Parking System zote za Jijini Arusha na Kimataifa,Ndg Justin Nyari, (aliyevaa kofia) , wakisubiri kutangwazwa kwa kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo

Mfanyabiashara maarufu wa Kampuni ya MONABAN ya Jijini Arusha  Ndg Phillemon Mollel akiongea na waandishi wa habari , mara baada ya kutangwazwa kwa kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo.
 Kushoto -kulia ni wakili maarufu ya Jijini Arusha Ndg Victor Njau, Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Bush Buck Safaris Ndg Mustapha Panju,Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na Mkurugenzi wa Kampuni Tanzania Cabs & Transport Company,Eland Motel,Mianzini Filling Station,Katibu wa Hunters Association of Tanzania na Mjumbe wa Board of Trustees ya Jumuiya ya ZAWIYANI KADIRIA TANZANIA , Alhaji Hamisi Migire na msomi Ndg Rubeni Mwiteni mara baada ya kutangwazwa kwa kura za maoni ya Ubunge Jijini Arusha leo.
MATOKEO
Wakili maarufu Jijini Arusha Ndg Edmond Ngemela akiteta jambo akiwa katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha ,  kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jini Arusha leo.
Wakili maarufu Jijini Arusha Ndg Edmond Ngemela akiteta jambo na Mwandishi Maarufu wa Jijini Arusha ajulikanaye kwa jina maarufu NGEMELA  katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha ,mara baada ya  kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jini Arusha leo.
Mfanya biashara maarufu Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Makampuni ya Arusha Trade Centre, JN Minning, Arusha Gem Trade na Arusha Parking System zote za Jijini Arusha na Kimataifa,Ndg Justin Nyari akipeana mkono na Wakili maarufu Jijini Arusha Ndg Edmond Ngemela katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha ,mara baada ya  kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jini Arusha leo.






CCM ni raha tupu !!!





Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha , kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jini Arusha leo.
Wanachama na wafuasi wa wagombea Ubunge katika Jiji la Arusha wakisubiri  katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha leo, kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jini Arusha leo.



Baadhi ya wanachama waliofika katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha leo, kupokea matokeo ya kura za maoni ya Ubunge Jini Arusha leo. 

KIKAO MAALUMU CHA KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA YA ARUSHA 

Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi walioomba ridhaa yakuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kuwania ubunge wa jimbo la Arusha katika uchaguzi wa mwezi Oktoba Mwaka huu,wakiwa katika Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilichokutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha . .
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli na kulia kwake ni Mwenyekiti wa jumuiya ya WAZAZI Wilaya ya Arusha Ndg Mtumwa,  akiendesha Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilichokutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha .
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli na kulia kwake ni Mwenyekiti wa jumuiya ya WAZAZI Wilaya ya Arusha Ndg Mtumwa,  katika Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilichokutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha .
 Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Bush Buck Safaris Ndg Mustapha Panju  na kulia kabisa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg Godfrey Mwalusamaba ,pembeni yake ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Arusha Mama Sifa Swai ,  katika Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilichokutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha .
 Mfanya biashara maarufu jijini Arusha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Bush Buck Safaris Ndg Mustapha Panju  na kulia Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Arusha na mfanyabiashara maarufu wa Kampuni ya MONABAN ya Jijini Arusha  Ndg Phillemon Mollel ,Ndg Emmanuel Olenjoro na kushoto kabisa ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya Arusha Ndg Martini Munissi,  katika Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilichokutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg Godfrey Mwalusamaba ,pembeni yake ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Wilaya ya Arusha Mama Sifa Swai ,  katika Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilichokutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha .
Dk  Mosses Mwizarubi au kwa jina maarufu Dr Mwiza au Nabii Mwiza  na Mfanya biashara maarufu Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Makampuni ya Arusha Trade Centre, JN Minning, Arusha Gem Trade na Arusha Parking System zote za Jijini Arusha na Kimataifa, Ndg Justin Nyari ,  katika Kikao Maalumu cha Kamati ya Siasa ya Wilaya kilichokutana na Wagombea wote ili kuvunja makundi leo katika Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha .

Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha - Jasper Kishumbua.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link