NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

Dkt. Abbasi: Tutaionesha Dunia Utamaduni Wetu Kutokea Moshi

Written By CCMdijitali on Thursday, January 20, 2022 | January 20, 2022

 





Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, leo Alhamisi Januari 20, 2022, amekagua maandalizi ya Tamasha kubwa la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro.

Katika Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Januari 22, 2022, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Chifu, akitumia jina la Chifu Hangaya. 

“Maandalizi yanakamilika na tayari vikundi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huu vinaendelea na mazoezi na wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania wameendelea kuwasili hapa Moshi.

“Tamasha hili linafungua njia ya matamasha mengine ya Utamaduni  wetu kuendelea hapa nchini. 

Tunataka kutumia utamaduni na sanaa kuileta dunia na kuionesha dunia kile Tanzania ilichonacho,” amesema Dkt. Abbasi kwenye Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi.

Tamasha hilo limeandaliwa na machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Chifu Frank Marealle na kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aongoza Kikao cha Maalum cha Kamati Kuu ya CCM

 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo tarehe 20 Januari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM White House Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo tarehe 20 Januari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM White House Jijini Dodoma.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo tarehe 20 Januari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM White House Jijini Dodoma.
 

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo tarehe 20 Januari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM White House Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo tarehe 20 Januari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM White House Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo tarehe 20 Januari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM White House Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalumu cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika leo tarehe 20 Januari, 2022 katika ukumbi wa Halmashauri Kuu CCM White House Jijini Dodoma.


AWANI ZA MAKAZI KUIBADILISHA TANZANIA KUWA YA KIDIJITALI

Anwani za Makazi kuwa Msingi wa Utambuzi wa Kila Mwananchi

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi kwenye
picha ya pamoja na Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja
wakijifunza namna ya kupata postikodi ya kata mbalimbali nchini kwa kutumia
simu ya mkononi wakati wa semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa Mkoa wa
Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na Postikodi iliyofunguliwa na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mkoani hapo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.
Jim Yonazi akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa semina ya kuwajengea
uwezo viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na
Postikodi katika ukumbi wa mikutano wa Mbaraka Mwinshee leo Januari 19,
2022.
 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja, akitoa salamu za Mkoa kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mkoa huo kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mbaraka Mwinshee leo Januari 19, 2022.


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Clarence Ichwekeleza akitoa taarifa kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi kabla ya ufunguzi rasmi wa semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi uliofanywa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (hayupo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa Mbaraka Mwinshee wa Mkoani humo.

Mhandisi Jampyion Mbugi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi iliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Jim Yonazi, mkoani hapo.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (kushoto) akiongea na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja, baada ya kuwasili ofisini kwake mkoani humo kwa ajili ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa Mkoa huo kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mbaraka Mwinshee leo Januari 19, 2022.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi (aliyeketi wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Morogoro baada ya kufungua semina ya kuwajengea uwezo viongozi hao kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mbaraka Mwinshee leo Januari 19, 2022. Wa pili kushoto aliyeketi ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Bi. Mariam Mtunguja.

 Na Prisca Ulomi, WHMTH, Morogoro

Serikali imejikita kutekeleza mfumo wa Anwani za Makazi na Postikodi nchi nzima kwa
lengo la kuibadilisha Tanzania kuwa ya kidijitali kwa kuwa anwani za makazi na postikodi
ni msingi wa utambuzi wa kila mwananchi.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape
Nnauye ambaye amewakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi wakati
akifungua mafunzo ya kujenga uelewa kwa viongozi, watendaji na wataalam wa Mkoa
wa Morogoro kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi.


Dkt. Yonazi amesema kuwa anwani za makazi na postikodi ni msingi wa utambuzi ili kila
mwananchi aweze kutambuliwa pale alipo ambapo nia ya Serikali ni kuihakikisha kuwa
kila mtaa, barabara, inakuwa na jina la mtaa na kila nyumba inakuwa na namba ya
nyumba


Vile vile, ameitaka Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro kusimamia utekelezaji wa mfumo
huu ili ifikapo Mwezi Mei mwaka huu jambo hili liwe limekamilika kwa kuwa utekelezaji
wa mfumo huu utaiwezesha Serikali kuwa na sensa bora ya watu na makazi
inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.


Ameongeza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu inayoratibu jambo hili, imeelekeza taasisi zote za
Serikali nchi nzima zinatekeleza mfumo huu wamiliki wote wa majengo na nyumba nao
waweke namba za nyumba kwenye nyumba na majengo yao na wataalam wote
waliojengewa uwezo watumike vizuri kutekeleza mfumo wa anwani za makazi na
postikodi na jambo hili liwe ajenda kwenye vikao.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bi. Mariam Mtunguja akizungumza kwa niaba ya
Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigela amesema kuwa kimsingi tumechelewa kutekeleza
mfumo huu wa anwani za makazi, ila kwa kuwa viongozi mtajengewa uelewa, ni
matumaini yangu kuwa kwa pamoja tutashirikiana na wataalam wetu kutekeleza jambo
hili kwenye maeneo yetu ndani ya muda uliopangwa na niahidi kuwa Mkoa wa
Morogoro hatutawaangusha Wizara.


Naye Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza, akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi, amesema kuwa mfumo wa anwani za makazi na postikodi
ni moja ya aina ya mawasiliano kama zilivyo aina nyingine za mawasiliano na mfumo huu
unahusisha eneo husika ambapo utamuwezesha mwananchi kutoka sehemu moja
kwenda sehemu nyingine; utarahisisha shughuli za kiuchumi, kijamii na utawala


Wakitoa salamu za shukrani kwa niaba ya viongozi wengine, Mwenyekiti wa CCM Wilaya
ya Morogoro Mjini Fikiri Juma, amesema kuwa viongozi watoe majina ya mitaa ndani ya
siku moja ili kufanikisha utekelezaji na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Pascal
Kihanga amesema watahamasisha wananchi kununua vibao vya nyumba ili kufaniisha
uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi kwenye Mkoa huo

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari



Mhe. Rais samia aongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo Ikulu Chamwino Dodoma

Written By CCMdijitali on Wednesday, January 19, 2022 | January 19, 2022

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo tarehe 19 Januari, 2022 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.

 





HANDENI YAFANYA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI.

 

Mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen akiongea kwenye Baraza la wafanya kazi.









Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imefanya kikao cha baraza  la wafanyakazi Ili kupitia mpango wa rasimu ya bajeti  ya Halmashauri ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Saitoti Zelothe Stephen (Aliyevaa tai nyekundu) amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwatetea wananchi  hivyo watanzania na wafanyakazi  wote kwaujumla wazidi kumuombea Rais Afya njema Ili wazidi  kuuona upendo wake kwa wafanyakazi.

Bw. Saitoti amesema kuwa baraza  hilo ni muhimu kupitia rasimu hiyo ya bajeti ili kuboresha kabla ya kwenda  kujadiliwa kwenye baraza la madiwani pia alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Walimu kwa kusimamia Miradi ya Ujenzi wa miundombinu ya Madarasa ya UVIKO-19 na Miradi yote inayotekelezwa kwenye shule zao.

Kwakumalizia Bw. Saitoti amewaasa watumishi kusimamia uadilifu na uaminifu kwenye mazingira yao ya Kazi.

Kwaupande wa viongozi wa vyama vya Wafanyakazi wameishauri Serikali kutoa motisha kwa watumishi wanaofanya Kazi vizuri na wameomba kuboreshewa maslahi pamoja na mazingira bora ya kufanyia Kazi.

MKUU WA MKOA WA TABORA AJUMUIKA NA WANAFUNZI WA SHULE SHIKIZI KUPANDA MITI WILAYANI SIKONGE

 TABORA YA KIJANI INAWEZEKANA

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akijumuika na mwanafunzi kuchimba shimo kwa ajili ya kuotesha kwenye  shule shikizi ya Gezaulole  Wilayani Sikonge.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akijumuika na mwanafunzi wa  shule shikizi ya Gezaulolekwa kuotesha mti  Wilayani Sikonge.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt Batilda Buriani akijumuika na mwanafunzi wa  shule shikizi ya Gezaulolekwa kuotesha mti  Wilayani Sikonge.





Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Balozi Batilda Burian jana tarehe 18 Januari, 2022 na Viongozi wa Wilaya ya Sikonge walijumuika na wanafunzi wa shule shikizi ya Gezaulole kupanda miti katika eneo la Shule hiyo iliyopo Wilayani Sikonge. Mkoa wa Tabora umejiwekea malengo ya kupanda miti milioni 12 kwa mwaka.



MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKIJARIBU PIKIPIKI

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akijaribu moja ya pikipiki kati ya pikipiki 300 zilizotolewa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya kazi za  Maafisa Ugani katika Halmshauri 140 hapa nchini. Januari 17,2022.

WATAALAMU WA SEKTA YA ARDHI NCHINI WATAKIWA KUWA WABUNIFU - KIKWETE NAIBU WAZIRI

 Naibu waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Ridhiwani Kikwete (MB) amewaagiza Makamishina wa Ardhi kote wasaidizi wa Mikoa yote nchini kuhakikisha wanaweka vipimo vya utendaji kazi watumishi wa sekta ya ardhi kila baada ya mwezi mmoja ili kupima utendaji wao kwa lengo la kuleta tija katika sekta ya Ardhi 


Aidha aliwataka wataalamu wa sekta ya Ardhi nchini kuwa wabunifu sambamba na kutoa huduma bora na kwa wakati ili kusaidia serikali na wananchi kwa ujumla. #RK #kaziimeanza #ardhiyetuhakiyetu #matokeochanya


 




DC LUSHOTO AKAGUA ZOEZI LA UPOKEAJI NA UANDIKISHWAJI WA WANAFUNZI DARASA LA KWANZA NA AWALI

 MKUU WA WILAYA YA LUSHOTO ATEMBELEA NA KUKAGUA ZOEZI LA UPOKEAJI NA UANDIKISHWAJI WA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA NA AWALI KATIKA SHULE ZA MSINGI HALMASHAURI YA WILAYA YA LUSHOTO

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Ndugu Kalisti Lazaro ametembelea na Kukagua Zoezi la Upokeaji na Uandikishwaji wa Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na Awali katika Shule za Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto.

Mkuu wa Wilaya ametoa Maagizo kwa Waalimu Wakuu kuwa Wawapokee na Kuwaandikisha Wanafunzi wa Darasa la Kwanza na Awali kama Utaratibu wa Serikali unavyoelekeza na bila Kuwarudisha Nyumbani kwa Kutokuwa na Sare za Shule na Kuwachangisha Wazazi Michango isiyo na Kibali. 
Alieleza "Mwalimu wapokeeni Wanafunzi na Kuwaandikisha bila Masharti, Serikali imeweka Utaratibu Mzuri msiuvuruge, Kama Mwanafunzi hana Sare za Shule apokelewe na Mzazi wake apewe muda wa Kulitekeleza hilo bila Mwanafunzi kuzuiwa kuingia Darasani na Michango inayoruhusiwa ni ile tuu ambayo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya imeipitisha na kutoa Kibali cha Mchango"

 

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akiwa Shule ya Msingi Mbula katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto ndugu Kalisti Lazaro akiwa Shule ya Msingi Mbula katika Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto






 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link