NAIBU WAZIRI PINDA AELEKEZA UENDELEZAJI MIJI KUZINGATIA MIPANGO KABAMBE

Na Munir Shemweta, WANMM Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amezielekeza Halmashauri zote nchini kuhakik...

Latest Post

Mbowe, Mdee wahojiwa na Bunge

Written By CCMdijitali on Sunday, April 9, 2017 | April 09, 2017


    Imeandikwa na Magnus Mahenge, Dodoma | Habari Leo

MWENYEKITI wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na mbunge wa Kawe Halima Mdee, jana wamehojiwa mbele ya Kamati ya Kudumu ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, inayoongozwa na Mbunge wa Newala Vijijini, George Mkuchika (CCM).

Mbowe ambaye pia ni wmenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Kawe, Mdee walitakiwa kufika mbele ya Kamati hiyo kutokana na maagizo ya Spika wa Bunge, Job Ndugai aliyotoa bungeni Jumatano, Aprili 5, mwaka huu, akiwataka waripoti kwenye kamati hiyo siku iliyofuata.


Mbowe ambaye alikuwapo bungeni siku hiyo na Mdee ambaye hakuwapo, wote wawili wametii wito wa Spika, Ndugai wa kusimama mbele ya Mwenyekiti Mkuchika kuhojiwa kama ilivyokuwa imeagizwa na Spika wa Bunge wakitakiwakujibu tuhuma zinazowakabili. Mbowe inadaiwa alitoa lugha za matusi mtandaoni na Mdee anadaiwa kutoa lugha za matusi kwa Spika bungeni.


Mwenyekiti wa Chadema alifikishwa mbele ya Kamati hiyo akituhumiwa kufanya kosa la kulitukana Bunge mtandaoni baada ya wabunge wawili wa chama hicho kushindwa uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).


Baada ya Ezekiel Wenje na Lawrance Macha waliokuwa wakiwania nafsi za ubunge wa EALA kupitia chama hicho kupata kura nyingi za hapana, Mbowe inadaiwa alianza kutukana bunge mitandaoni.


Habari za Mbowe kwamba alitukana mitandaoni ziliibuliwa na Mbunge wa Mwibara, Kange Lugola (CCM) ambaye aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kiongozi huyo kutoa lugha za matusi mitandaoni akilitukana bunge sababu ya wabunge wake kukosa kura za kutosha kuchaguliwa kuingia EALA.


Spika Ndugai wakati akitoa mwongozo kuhusu jambo hilo, alimtaka Mwenyekiti Mbowe afike kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujibu tuhuma hizo mara moja.


Mbunge wa Kawe, Mdee, alitakiwa kujitokeza mbele ya Kamati ya Maadili kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi akimtukana Spika bungeni. Katika taarifa yake, Spika Ndugai alisema Mbunge Mdee, siku ya uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Aprili 5, mwaka huu, alimtukana na akaamua kumnyamazia siku hiyo.


“Mdee alisikika akinitukana siku hiyo ya uchaguzi wa wabunge EALA, nikajitahidi kudhibiti hasira yangu, nikashusha hasira, nikaamua kunyamaza,” alisema na kuongeza kuwa jambo hilo liliwasikitisha wengi, wengine walimtumia ujumbe na yeye kama Spika aliamua kulipeleka suala hilo kwenye Kamati ya Maadili.


Ndugai alisema huo ni mwendelezo wa kuweka na kudhibiti nidhamu ndani na nje ya Bunge hilo la Bajeti ambalo wabunge watakuwapo bungeni kwa takribani miezi mitatu.


Alisema tofauti na wakati mwingine, wakati huu mbunge mmoja mmoja atafuatiliwa na kushughulikiwa, huku akitoa tahadhari kwa wabunge wenye tabia ya kutumia lugha zisizo za staha kuziacha.


“Naanza na Halima Mdee, ambaye yeye alimtukana Spika juzi, Watanzania wengi wamesikitishwa na jambo hili, wameniandikia na kunipigia simu…hii si mara ya kwanza kwa Halima, hata juzi nilivumilia sana, nilimuomba Mungu anisaidie nikanyamaza kimya, kwa hiyo suala lake nalipeleka mara moja kwenye kamati ya maadili,” alisema.

Aliongeza kuwa, “ haiwezekani Bunge hili liwaite watu walioko nje kwa utovu wa nidhamu halafu liwafumbie macho wabunge walioko humu ndani, ambao ni watovu wa nidhamu.”


Ndugai pia alisisitiza kuwa kama Halima asiporipoti kesho yake ambayo ni Aprili 7, basi polisi imsake na kumpeleka akiwa amefungwa pingu. “Halima Mdee popote pale alipo najua hayupo Dodoma kesho muda huu awe ameripoti kwenye Kamati, kama asiporipoti akamatwe na polisi popote alipo na aletwe na pingu hapa, tumekuja mmoja mmoja na tutashughulikiana mmoja mmoja,” alisema Ndugai.


Spika wa Bunge alimuita Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti ambaye bunge hilo katika mkutano wake wa sita liliazimia aitwe kwenye kamati hiyo kwa tuhuma za kuingilia madaraka ya Bunge, aliitikia na kuhojiwa.


Maazimio yatakayofikiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, yatafikishwa kwenye ofisi ya Spika naye atatolea uamuzi au ufafanuzi mbele ya wabunge wote bungeni siku atakayoona inafaa.


Somaliland court jails journalist two years for "anti-national activity"

SOMALIA

with REUTERS

A court in Somalia’s breakaway region of Somaliland has sentenced a reporter to two years in jail for what it said was endangering peace and security, a journalists’ rights group said on Saturday.

The National Union of Somali Journalists (NUSOJ) said that Abdimalik Muse Oldon was detained in February upon his return from the Somali capital and charged with “anti-national activity and violating the sovereignty and succession of Somaliland.”


The union said the ruling was a threat to independent media and relied on unclear laws to restrict journalists’ ability to carry out their work.


Somaliland government officials were not immediately available for comment.


Somaliland broke away from Somalia in 1991 but is not internationally recognized. It has largely been spared the unrest and insurgency driven by al Qaeda-linked al Shabaab in the rest of Somalia.


In addition to being targeted by violence, journalists in Somalia are often targeted by officials and by al Shabaab for the content of their work.


In 2013, a court in Somaliland sentenced two journalists for what it said was the publication of false news.


Magazeti ya Tanzania April 9, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo




























Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini

Written By CCMdijitali on Friday, April 7, 2017 | April 07, 2017


 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji kati kati aliyevaa Suti nyeusi akikiongoza Kikao cha maandilizi ya kuanzishwa mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la kutoa elimu itakayowasaidia wanafunzi kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.


Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrandwa Pili kutoka kushoto akifafanua jambo juu ya mpango huo utakaosimamiwa na UNODC.
Picha na – OMPR – ZNZ
.

 Press Release:-

Uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } umeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la kutoa elimu itakayowasaidia kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.

Uongozi huo umekutana na Watendaji wa Tume ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya pamoja na wale wanaosimamia udhibiti wa uhalifu Chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.


Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrand alisema mpango huo wa Mafunzo utashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.


Bibi Sylvie alisema katika kuupa nguvu zaidi mpango huo ili ufanikiwe vyema Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto pia itakuwa mshirika katika mpango huo utaoratibiwa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar.
  

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/4/2017.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 7,2017

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 7,2017



Watanzania waaswa kuwa makini na mitego inayoashiria kuchezewa kwa amani Mkoani Katavi

Written By CCMdijitali on Monday, April 3, 2017 | April 03, 2017

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Nd. Abdalla Mselem mchango wa shilingi Milioni 1,000,000/- alizoahidi ndani ya muda wa saa 24 ili zisaidie kukamilisha ujenzi wa jengo la CCM Mkoa Katavi.

Mchango huo aliutoa Ikulu ndogo ya Mkoa wa Katavi akijiandaa kurejea Zanzibar baada ya kumaliza ziara yake ya siku  tatu Mkoani humo iliyoambatana na uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru.


 Wazee waasisi wa  Kamati ya siasa ya Mkoa wa Katavi wakibadilishana mawazo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani hapo ofisi ya CCM Mkoa wa Katavi.

Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Nd. Abdalla Mselem mara baada ya kukutana na Viongozi wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo.
Kulia ya Ndugu Mselem ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,Wazee, Vijana Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Moudline Cyrus Castico.
Picha na – OMPR – ZNZ.


                                   Press Release:-

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema wakati umefika kwa Wanachama wa CCM kujipanga vyema katika kuhakikisha Viongozi wanaowachagua katika ngazi mbali mbali ndani ya Chama chao wanakuwa mahiri kwa ajili ya kueperusha bendera ya ushindi wa Chama hicho ifikapo mwaka 2020.

Alisema upembuzi wa wanachama hao katika kuwatafuta viongozi mahiri ndio njia pekee na sahihi itakayokiwezesha Chama cha Mapinduzi kuendelea kuongoza Dola ya Tanzania Bara na Zanzibar katika Miaka mingi ijayo.


Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akibadilishana mawazo na Viongozi wa Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi ya Mkoa wa Katavi kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Chama hicho Mkoa mara baada ya kumalizika kwa sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika Mkoani humo.


Aliwaeleza Viongozi hao kwamba Chama pekee chenye dhamana na imani ya kuliongoza Taifa la Tanzania bila ya kutetereka ni Chama cha Mapinduzi kutokana na Historia yake iliyotokana na vyama vya Ukombozi vya TANU na Afro Shirazy Party.


Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema CCM ndio Chama Pekee Nchini Tanzania kilichoainisha ndani ya Ilani na Sera zake kuahidi kutunza Amani na Utulivu wa Taifa Uliopo sehemu zote za Jamuhuri ya Mauungano.


Aliwahimia Wanachama wa Chama hicho pamoja na Wananchi wote Nchini kujitahidi kuitunza Amani ya Taifa na kujiepusha na vishawishi vya baadhi ya Watu wanaokusudia kutaka kuichafua kwa malengo yao binafsi.


“ Wana Chama cha Chama cha Mapinduzi pamoja na Wananchi wote wasikubali kuruhusu watu wachache wanaojaribu kutaka kuichezea amani ya Nchi”. Alisema Balozi Seif Ali Iddi.


Alisema wapo baadhi ya Raia wa Mataifa Jirani waliyoamua kuzihama Nchi zao na kuomba kupatiwa Uraia wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kukimbia vita visivyokwisha vya wenyewe kwa wenyewe vilivyotokana na sababu za kuichezea amani ya Nchi hizo.


Balozi Seif alisema Watanzania wanapaswa kulazimika kuwa makini na mitego kama hiyo inayoashiria  kuchezewa kwa amani hiyo na vyenginevyo ile sifa inayoelezwa kila mara na jumuia za Kimataifa ya kuwa Tanzania ni Kisiwa cha Amani inaweza kuyayuka.


Mapema Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Katavi Ndugu Abdalla Mselem alisema Wana CCM na Wananchi wa Mkoa wa Katavi wameomba fursa zozote zinazotokezea za Kiserikali na Kichama zifikiriwe kupelekwa Mkoani humo kwa vile bado ni mpya.


Nd. Mselem alisema Mkoa wa Katavi ulioasisiwa Mwaka 2012 ulitokana na Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012 iliyopelekea mabadiliko ya mgao wa Mikoa kufuatia ongezeko la Idadi ya Watu katika maeneo mengi nchini.


Wakati huo huo Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif alikutana kwa mazungumzo mafupi na Kamati ya Waasisi wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Katavi kwenye jengo la Ofisi ya CCM ya Mkoa huo.


Katika mazungumzo hayo Waasisi hao walimlalamikia Balozi Seif  juu ya tabia mbovu ya baadhi ya Watendaji Wakuu wa Serikali wanapofanya ziara Mikoani wanakwepa kukutana na Viongozi wa Chama Tawala.


Waasisi hao walisema kitendo cha Watendaji hao kinaashiria dharau zisizo na msingi wakisahau kwamba uwajibikaji wanaoutekeleza unatokana na Sera za Chama cha Mapinduzi zilizopata ridhaa ya Wananchi walio wengi na hatimae kuunda Serikali iliyowaweka Madarakani.


Balozi Seif Ali Iddi alikuwa Mkoani Katavi kuzindua  rasmi Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein zitakazochukuwa siku 195 ndani ya Mikoa  yote 31Tanzania Bara na Zanzibar.

 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
3/4/2017.

 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link