Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Wiliam Ole Nasha akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa tovuti ya Wakala wa Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA) Mjini Dodoma jana (Picha na Sifa Lubasi)
Imeandikwa na Sifa Lubasi, Dodoma - Habari Leo
Serikali imewakata wakulima kutouza chakula ya nje ya nchi na badala yake kuhifadhi chakula kutokana na taarifa ya hali ya hewa kuonesha uwezekano wa nchi kulkumbwa na lanina.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tovuti ya wakala wa hifadhi ya taifa ya chakula (NFRA) Naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, William Ole Nasha amesema ni vyema wakulima wakahifadhi chakula na serikali itahakikisha kuna akiba ya chakula ambapo NFRA na bodi ya mazao mchanganyiko wanaendelea kununua chakula cha akiba tani 200,000 wakati mahitaji ni tani 150,000 za mahindi.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa serikali Hassan Abasi amesema atahakikisha serikali inasema kabla ya watu wengine hawajasema.
Soma habarileo Septemba 9 kwa habari zaidi.
Ole Nasha: Msiuze chakula nje ya nchi
Written By CCMdijitali on Thursday, September 8, 2016 | September 08, 2016
Labels:
BIASHARA