Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mwanachama wa Shirikisho la Vyuo Vikuu CCM Chuo cha St Augustine (Arusha Campus) Ndg Juma Richard Kashirim akisaini kitabu cha wageni, Ndg Leons Edward Silaa, wakishuhudiwa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Moivaro Ndg Philemon Meoojo wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.
Sheikh Rajabu Mtukuta, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Kata ya Kurasini Wilaya ya Temeke,Mkoa wa Dar Es Salaam akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua (hayupo pichani) akishuhudiwa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Moivaro Ndg Philemon Meoojo wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.
Kutoka kulia kwenda kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Moivaro Ndg Philemon Meoojo, Sheikh Rajabu Mtukuta, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Kata ya Kurasini Wilaya ya Temeke,Mkoa wa Dar Es Salaam na kada wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Daraja II Ndg Rahimu ,maarufu kwa jina la "MGOSI" wakiwa katika Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha |
Leo tarehe 11 Oktoba, 2016 Sheikh Rajabu Mtukuta, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Kata ya Kurasini Wilaya ya Temeke,Mkoa wa Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Moivaro Ndg Philemon Meoojo na Wanachama wa CCM kutoka Shirikisho la Vyuo Vikuu, Chuo cha St Augustine (Arusha Campus) Ndg Juma Richard Kashirim na Ndg Leons Edward Silaa walitembelea Ofisi ya Katibu wa Siasa na Uenezi ya CCM Wilaya ya Arusha na kukutana na Ndugu Jasper Kishumbua Katibu wa idara hiyo muhimu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya.
Wakiwa Wilayani hapo viongozi hao toka maeneo tofauti walibadilishana mawazo juu ya mwenendo mzima wa siasa za Wilaya ya Arusha kwa upande wa CCM na Jumuiya zake.Aidha Mwenyekiti mstaafu wa CCM Kata ya Kurasini Wilaya ya Temeke ,Mkoa wa Dar Es Salaam Sheikh Rajabu Mtukuta, alimweleza mwenyeji wake kuhusu "Kongamano la Kiislamu la Kuiombea Nchi Yetu Amani"waliloandaa na litakalofanyika katika Uwanja Sheihk Abedi tarehe 15 - 16 Oktoba 2016,Jijini Arusha.
Kwa nyakati tofauti nao Wanachama wa Shirikisho la Vyuo Vikuu nao walikuwa pia na ujumbe kuhusu "Uchagiaji damu" jambo ambalo litatolewa ufafanuzi ,mara taratibu zitakapokamilika.
Naye Katibu Mwenezi Ndugu Jasper Kishumbua aliwahakikishia kuwapa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha matukio hayo muhimu kwa mustakabali wa Amani ya Taifa letu ,lakini pia kwa Wananchi wa Jiji la Arusha.
Pamoja na yote katibu wa Siasa na Uenezi alihimiza na kusisitiza kuwa kila ngazi ya uongozi ya Chama na Jumuiya zake kufuata Kalenda ya Vikao Vya Chama Cha Mapinduzi 2016 na kusimamia yale yote yaliyohimizwa kama AGENDA ZA KUDUMU kwa kuwa haya ndiyo yatakuwa maandalizi bora zaidi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa CCM na Jumuiya zake unaotakiwa kufanyika Mwakani 2017.
"Sasa Kazi ya Kujenga Nchi na Kujenga Chama"
UMOJA NI USHINDI!