Home » , » MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM MKOA WA MBEYA YAIVA,KINANA ASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII.

MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM MKOA WA MBEYA YAIVA,KINANA ASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII.

Written By CCMdijitali on Saturday, February 1, 2014 | February 01, 2014

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la Magreth Kalimwa (wapili kulia), katika Kijiji cha Mlimanyoka, Kata ya Nsalanga, wilala ya Mbeya mjini. Kinana alifika kumsaidia mkulima huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, inayofanyika Kitaifa Jumapili hii mjini Mbeya.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Bi.Magreth Kalimwa mara baada ya kuwasili kwenye shamba lake kwa ajili ya kushiriki kupalilia shamba hilo lenye ekari moja na nusu
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi na Wanachama wa CCM,(hawapo pichani) katika kijiji cha Itesi Mashariki,Kata ya Nshalanga,alipokwenda kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya kata ya chama cha CCM,Wilaya ya Mbeya Mjini mkoani Mbeya mapema leo.
Ujenzi wa jengo la Ofisi ya kata ya chama cha CCM,Wilaya ya Mbeya Mjini mkoani Mbeya mapema leo kama ionekanavyo mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokwenda kufanya ukaguzi
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisaidiana na vijana kuandaa jukwaa litakalotumika wakati wa mapokezi ya matembezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Sokine mjini Mbeya. Matembezi hayo yanaongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
Vijana wakiwa kwenye mazoezi ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM yatakayofanyika Jumapili hii mjini Mbeya.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link