MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...

Latest Post
Showing posts with label BIASHARA. Show all posts
Showing posts with label BIASHARA. Show all posts

SEKTA YA MADINI IMEENDELEA KUWA NGUZO YA UKUAJI WA UCHUMI-MAJALIWA

Written By CCMdijitali on Monday, September 22, 2025 | September 22, 2025



WAZIRI MKUU,Kassim Majaliwa amesema kuwa Sekta ya madini imeendelea kuwa nguzo ya uchumi nchini ambapo katika mwaka 2022 sekta hiyo imekua kwa asilimia 10.9 na kufikia mchango wa asilimia 10.1 kwenye Pato la Taifa mwaka 2024, ikilinganishwa na asilimia 9.0 mwaka 2023.

Ametoa kauli hiyo Leo (Jumatatu, Septemba 22, 2025) wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya Madini Mkoa wa Geita, yaliyofanyika katika viwanja vya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema kuwa hatua hiyo imetokana na jitihada mbalimbali za Serikali ya awamu ya sita ikiwemo kuimarishwa kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa biashara ya madini, matumizi ya mifumo ya kielektroniki (online mining cadastre system), uwepo wa masoko ya madini na ufuatiliaji wa mikataba ya uwekezaji.

"Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuweka kipaumbele katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji kwenye sekta ya madini ili rasilimali za madini zichangie kwa katika ukuaji wa uchumi na ustawi wa Watanzania wote".

Waziri Mkuu ametoa rai kwa wadau wa sekta ya madini kuendelea kuwekeza katika teknolojia kwani ndiyo daraja la mageuzi kuanzia utafiti na uchimbaji, usafishaji na biashara ya madini. "Bila teknolojia sahihi, haiwezekani kuongeza tija, kuhakikisha usalama wa wachimbaji, kulinda mazingira, wala kufanya uongezaji thamani wa madini yetu".

Ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo, katika kiipindi cha mwaka 2021 hadi 2025 Wachimbaji wadogo wa Geita wamezalisha zaidi ya kilo 22,000 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi Trilioni 3.44, huku Serikali ikipata zaidi ya Shilingi Bilioni 235.5 kama mrabaha. "

Aidha, makampuni makubwa kama Geita Gold Mine na Buckreef katika kipindi hicho wamezalisha kilo 76,530 za dhahabu zenye thamani ya Shilingi Trilioni 11.38, na Serikali kupata zaidi ya Shilingi Bilioni 793 kama mrabaha."

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba amesema kuwa Tanzania sasa imepiga hatua kwa kuwa na viwanda vya kutengeneza zana mbalimbali za uchimbaji wa madini.

"Katika mwaka wa fedha 2024-2025 tumeweza kuzalisha tani 62 za dhahabu tofauti na nyuma tulikuwa tukizalisha tani 40-50 kila mwaka hii inatufanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano bora Afrika katika uzalishaji wa dhahabu."

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema huo umefanya kazi kubwa ya kusambaza umeme vijijini na kwa kuwa kazi ya uchimbaji unahitaji umeme tayari umeme umepelekwa katika maeneo mengi ya wachimbaji wadogo.

"Tumefanyia kazi maagizo ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kupeleka umeme katika maeneo ya wachimbaji wadogo ili wafanye kazi zao na kuwa na uzalishaji wa uhakika katika maeneo yao."

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. BILIONI 78.6 KUTOKA UJERUMANI

Written By CCMdijitali on Wednesday, July 9, 2025 | July 09, 2025


Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) zimesaini Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya Euro milioni 25.68 (sawa na sh. Bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya Maji na Maliasili.

Mikataba hiyo imesainiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kwa upande wa Ujerumani imesainiwa na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens.

Dkt. Mwamba alisema kuwa mikataba iliyosainiwa ni kwa ajili ya mradi wa programu ya ufadhili wa miradi ya Maji inanayotegemea matokeo (Investment Financing Facility – Output Based Approach (IFF-OBA) kwa kiasi cha Euro milini 10 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 30.6.

Mkataba mwingine ni wa fedha za kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa ustahimilivu wa tabia nchi (Climate Resilient Towns project) kwa kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 2.08.

Alisema kuwa mkataba wa tatu ni wa utekelezaji wa mradi wa Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama Project for Sustainable Development of Protected Areas kwa kiasi cha Euro milioni 15 sawa na shilingi bilioni 45.9.

Amesema lengo la miradi hiyo ni kutoa motisha kwa Mamlaka za Maji hapa Tanzania kukopa kutoka Benki za Kibiashara kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji ili kuboresha huduma na kuongeza mapato. 

Alisema kuwa Kupitia Programu ya IFF – OBA, mamlaka zilizokidhi vigezo zinaweza kukopa kutoka Benki za Biashara na kupatiwa ruzuku kutoka kwenye programu ambapo Mamlaka husika zinapokidhi vigezo, zinaweza kupatiwa ruzuku ya asilimia 50 ya gharama za miradi hadi kufikia kiwango kisichozidi Euro milioni Moja. 

Pia mikataba hiyo inalenga uhifadhi na uendelezaji wa maeneo ya Hifadhi za Serengeti na Katavi- Mahale kuhakikisha kunakuwa na uhifadhi na manufaa ya kijamii kwa jamii zinazozunguka hifadhi hizo.

Aidha Dkt. Mwamba ameihakikishia Serikali ya Ujerumani kuwa miradi iliyokusudiwa itatekelezwa kikamilifu na pia Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo na Ujerumani kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili.

Kwa Upande wake Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller, alisema kuwa utiaji saini wa mikataba hiyo mitatu ambayo ni sehemu ya muendelezo wa ushirikiano wa kifedha kati ya Tanzania na Ujerumani kupitia benki yake ya maendeleo (KfW).

“Nina furaha kubwa kufanikisha zoezi hili na Ninawatakia wananchi wa Tanzania maendeleo makubwa, hasa katika Maliasili ambayo pia inamaanisha utalii kuna watalii wengi kutoka Ulaya, hasa kutoka Ujerumani, na hiyo inaleta nguvu kubwa ya kiuchumi kwa nchi, jambo ambalo ni muhimu. Naweza kuwahakikishia kuwa Ujerumani itaendelea kuwa mshirika wa kweli wa Tanzania, Tutaendelea kusimama pamoja nanyi” alisema Mhe. Muller

Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens, alisema kuwa Mikataba hiyo, ni ishara ya hatua nyingine mbele katika ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani ambao umekuwa mzuri tangu miaka ya 1960.

Bw. Christoph Tiskens alisema kuwa, mikataba hiyo miwili itagusa sekta muhimu sana kwa maendeleo ya Tanzania, kupitia awamu ya pili ya Mfuko wa Uwekezaji wa Fedha kwa ajili ya Miundombinu ya Maji (Investment Financing Facility) yenye thamani ya Euro milioni 10, ambayo itafungua fursa mpya kwa mamlaka za maji hapa Tanzania kupitia benki za ndani. 

“Kipengele cha kupitia benki za ndani ni muhimu sana kwa sababu mbinu hii ya ubunifu inasaidia kukuza miradi inayoweza kufadhiliwa (bankable projects) kwa ajili ya mamlaka za maji, hasa katika mazingira ambayo Tanzania inahitaji kiasi kikubwa cha uwekezaji na fedha” alisema Bw. Tiskens.

Aliongeza kuwa Mkataba wa pili uliouwekwa saini, unaoitwa "Maendeleo Endelevu ya Mfumo wa Ikolojia ya Maeneo ya Hifadhi", utaimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili pamoja na wadau wa hapa nchini, na mkataba huo unalenga kuimarisha uhifadhi wa maliasili amba oni urithi wa kipekee wa Tanzania na pia kuanzisha minyororo ya thamani kwa ajili ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo haya ya asili ya maliasili, ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta ajira.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App

RAIS MHE. DKT. SAMIA AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA PAMBA CHA BIOSUSTAIN TANZANIA LIMITED MEATU

Written By CCMdijitali on Tuesday, June 17, 2025 | June 17, 2025

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited Meatu mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited Meatu mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe kuhusu Kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited Meatu mkoani Simiyu tarehe 17 Juni, 2025.






Mandhari ya kiwanda cha kuchakata pamba cha Biosustain Tanzania Limited kilichopo Meatu mkoani Simiyu ambacho kimezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 17 Juni, 2025.



WAZIRI KOMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA KAMPUNI YA VIETTEL

Written By CCMdijitali on Monday, April 28, 2025 | April 28, 2025

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amefanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Haotel Tanzania Kanali Dao Xuan Vu, katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Hanoi, Vietnam.

 

Mazungumzo hayo yalilenga kujadili kuhuhusu fursa mpya za uwekezaji zilizopo nchini na kuimarisha ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji.

 

Waziri Kombo yuko nchini Vietnam kwa ziara ya kikazi, akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini humo mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Khamis Omar, Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa Balozi John Ulanga, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Felista Rugambwa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri na Viongozi wa Sekta Binafsi na Wafanyabiashara. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Haotel Tanzania Kanali Dao Xuan Vu, wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Hanoi, Vietnam.


Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi na Biashara ya Kimataifa Balozi John Ulanga akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam

Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Bw. Gilead Teri akifafanua jambo  wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam

Mkurugenzi Mtendaji wa Nakiete Pharmacy na Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bw. Vicent Bruno Minja akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam

PICHA YA PAMOJA

Balozi wa Tanzania nchini Vietnam mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Khamis Omar,akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam

Balozi wa Tanzania nchini Vietnam mwenye Makazi yake Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Khamis Omar,akichangia jambo wakati wa mazungumzo na Kampuni Viettel ya Vietnam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Viettel, ambayo ni kampuni tanzu ya Kampuni ya Mawasiliano ya Haotel Tanzania Kanali Dao Xuan Vu, wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Hanoi, Vietnam.


WAKOPAJI WAKUMBUSHWA KUSOMA MIKATABA KABLA YA KUCHUKUA MIKOPO

Written By CCMdijitali on Saturday, March 22, 2025 | March 22, 2025

Serikali imewakumbusha wakopaji kusoma kwa kina masharti yote ya mikataba kabla ya kuchukua mikopo kutoka kwa Taasisi za kifedha ili kujiepusha na matatizo yanayoweza kutokea kutokana na masharti magumu au riba kubwa ambazo huathiri urejeshaji wa mkopo.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Arch. Chagu Nghoma, aliyasema hayo  alipokutana na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Fedha pamoja  na Taasisi zake  ambayo imewasili mkoani humo kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha  kwa Wananchi wa mkoa huo katika makundi mbalimbali.

“Tunaendelea kuwakumbusha wakopaji kuongeza umakini katika kusoma mikataba wanayoingia kutokana na kuongezeka kwa malalamiko kutoka kwa wakopaji ambao wanakabiliwa na riba kubwa, masharti magumu ya marejesho, na faini zisizoeleweka baada ya kushindwa kutimiza masharti ya mikopo.

Aliongeza kuwa ni muhimu kwa mkopaji ikiwa hajaelewa mkataba vizuri, atafute  ushauri wa kisheria au wa kifedha kabla ya kutia saini mkataba wowote wa mkopo ili kujiepusha na matatizo yanayoweza kujitokeza baadae.

Arch. Chagu Nghoma, aliwasisitiza wakopaji kuwa waangalifu na kuepuka kukopa kwenye Taasisi za Fedha zisizo rasmi ambazo zinaweza kuwa na masharti kandamizi iwapo watashindwa kulipa mkopo.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo ya elimu ya fedha, mkazi wa Buhongwa, Mwanza, Bi. Julieth Siange, alishukuru kwa elimu waliyoipata ikiwemo msisitizo waliopewa wa kutojiunga na vikundi ambavyo havijasajiliwa bali wajiunge katika vikundi rasmi vilivyosajiliwa na vinavyotambulika na Serikali ili matatizo yanapotokea waweze kusaidiwa kisheria.

Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa utoaji wa elimu ya fedha kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Salim Khalfan Kimaro, alisema kuwa, pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kuweka sheria na kanuni mbalimbali kwa watoa huduma za fedha jinsi wanavyotakiwa kuendesha Taasisi hizo, bado kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya watoa huduma kutofuata sheria na kanuni.

Bw. Kimaro, alifafanua kuwa kutokana na changamoto hizo kutoka kwa watoa huduma  kutokuwa waaminifu, Serikali itaendelea kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuzichukulia hatua za kinidhamu ili kuhakikisha Taasisi hizo zinafanya kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni na sheria.

Wizara ya Fedha inaendelea na zoezi la utoaji elimu ya fedha kwa wananchi wa makundi yote ikiwa ni utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha kwa mwaka 2021/2022 hadi 2029/2030.








SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA UWEKEZAJI NA UKUAJI WA UCHUMI

Written By CCMdijitali on Friday, February 28, 2025 | February 28, 2025

 Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na ukuaji wa uchumi nchini.

Dkt. Nchemba alisema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano ya Kimkakati kati ya Serikali na Washirika wa Maendeleo Ngazi ya Juu, ambao unalenga kubadilishana maarifa, taarifa, na uzoefu kuhusu sera na mikakati ya maendeleo ya nchi.

Alisema Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Uwekezaji Tanzania (Tanzania Investment Act, 2024) na kuanzisha Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi (Tanzania Investment and Special Economic Zones Authority) ili kuboresha mazingira ya uwekezaji. 

“Serikali kupitia Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Kituo cha Uwekezaji kati ya Sekta Binafsi na Umma (CPPP) imeendeleza majadiliano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika maamuzi”, aliongeza Mhe. Dkt. Nchemba.

Mhe. Dkt. Nchemba ambaye ni Mwenyekiti wa Mkutano huo, alisema Serikali pia inaandaa Mkakati wa Kitaifa wa Uendelezaji wa Uwekezaji (2025/2026 – 2034/2035) ambao utakuwa na mpango wa utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini, unaoeleza majukumu ya kila mdau na viashiria vya kupima maendeleo.

Dkt. Nchemba alibanisha kuwa katika kipindi cha mwezi Julai 2024 hadi Desemba 2024, Serikali imeongeza uwezo wa uzalishaji umeme kwa asilimia 30.3, hasa kupitia Mradi wa Umeme wa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kupunguza gharama za biashara.

“Kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2024, Serikali imepunguza au kuondoa ada na tozo mbalimbali ili kuboresha mazingira ya biashara”, aliongeza Mhe. Nchemba.

Dkt. Nchemba alisema Serikali pia imepata mafaniko makubwa katika ukuaji wa uchumi jumuishi ambapo idadi ya shule na wanafunzi imeongezeka, vituo vya afya vimeongezeka na huduma zimeboreshwa, huduma za maji zimeongezeka katika maeneo yote nchini pamoja na ongezeko la ajira.

Aidha, alitoa rai kwa wadau wote kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kufanikisha utekelezaji wa Mwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo (DCF) ambao umetilia mkazo utaratibu wa ufadhili wa miradi ya mabadiliko ya tabianchi (climate financing modality) na kuimarisha Ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kama njia mbadala za ufadhili.

Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa Kundi la Washirika wa Maendeleo na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Nicola Brennan aliishauri Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya biashara kwa kuondoa vikwazo vinavyozuia uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni.

Alisema hii itaongeza mchango wa sekta binafsi katika kuleta uwekezaji, ajira, uvumbuzi, na suluhisho kwa changamoto mbalimbali ili kujenga uchumi imara.

“Wadau wa Maendeleo tayari tumekuwa na majadiliano mazuri kuhusu hili, na tunapongeza utayari wa Serikali kushirikiana nasi kuona jinsi bora ya kuondoa vikwazo na kuvutia uwekezaji zaidi wa moja kwa moja wa kigeni (FDI) nchini Tanzania, pamoja na kuimarisha sekta ya biashara ya ndani”, aliongeza.

Mhe. Brennan alisema Washirika wa Maendeleo watahakikisha kuwa Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2050 inapata ufadhili wa uhakika na endelevu, hasa katika sekta za afya, elimu na sekta ya kijamii kwa ujumla.

“Tunapopanga vipaumbele katika matumizi ya rasilimali finyu za Msaada wa Maendeleo (ODA), ni muhimu pia kuelewa vyema vyanzo vingine vya ufadhili vinavyopatikana kwa nchi zenye kipato cha kati nje ya ODA, pamoja na mchango ambao sisi kama Wadau wa Maendeleo tunaweza kutoa kusaidia Tanzania kuzifikia na kuzitumia fursa hizo ipasavyo. Tunatazamia kujadili zaidi suala hili kwa kina.”

Aliahidi kuwa Washirika hao wataendelea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha maendeleo yanapatikana na kustawisha jamii.



















 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link