Home »
KITAIFA
,
National News
» KATIBU MKUU WA CCM NDG KINANA ALIA NA UMANGIMEZA KWA KUTOKUWAHUDUMIA WANANCHI.
KATIBU MKUU WA CCM NDG KINANA ALIA NA UMANGIMEZA KWA KUTOKUWAHUDUMIA WANANCHI.
Written By CCMdijitali on Tuesday, April 15, 2014 | April 15, 2014
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa soko la samaki la Ikola wilayani Mpanda mkoani Katavi
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa soko la Samaki (Mwalo),ambao imeelezwa kuwa utapunguza umaskini kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo imeelezwa kuwa mradi huo wa soko na kuhifadhia samaki umechelewa kukamilika na kupitisha miaka miwili ya zaidi ya muda ulipangwa kwenye mkataba,Kinana amewahidi Wananchi kuwa atalifuatilia tatizoo hilo na kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyoahidiwa.Eneo hilo la kisasa kabisa litatumika kuongeza thamani ya samaki.
Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,akiuliza swali la zahanati na ,Elimu na Barabara kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana (pichani kulia),alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa Samaki (Mwalo).
Kinana akipata maelezo mafupi kuhisiana na eneo la soko hilo la kukaushia samaki na dagaa
Ndugu Kinana akikaribishwa kwa balozi.
Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakiwa wameketi kwa balozi wa shina namba 2,tawi la Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani Katavi.
Ndugu Kinana akizungumza na wajumbe wa shina namba 2 (hawapo pichani),tawi la Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani Katavi.
Wajumbe wa tawi la Ikolasto wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.(hayupo pichani).
Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, akijibu na kutoa taarifa mbalimbali kuhusiana na jimbo lake katika suala zima la kutekeleza na kuhumiza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,mbele ya wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo,katika mkutano wa hadhara,Kinana alijikuta akigeuka mbogo na kuwaomba radhi wakazi wa kata ya Kirema, Ikola na Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi, baada ya kubaini kuwa,kumekuwepo na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa Serikali.Kinana amesema chama chake kamwe hakitowavumilia watendaji wanaoendekeza vitendo vya urasimu na umangimeza wa kutumia makaratasi ofisini badala ya kuwatumikia wananchi kwa kuwajibika ipasavyo.
Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume akizungumza na wananchi kwenye mwalo wa Ikola
Wananchi wa Ikola wakimshangilia Kinana katika mkutano aliofanya baada ya kukagua ujenzi wa mwalo wa Ikola wilaya ya Mpanda mkoani katavi
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao kilichofanyika kwenye shina namba mbili, tawi la Ikola Store. Wapili kulia ni Mjumbe wa Mwenyekiti wa shina hilo, Kawawa Mustafa. Picha zote na Bashir Nkoromo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wananchi baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa Mwalo au soko la samaki la Ikola wilayani Mpanda
Mkazi wa Ikola akiwa na samaki aina ya kambale wakati akitafuta wateja katika eneo hilo la ikola wakati Kinana alipokuwa akikagua ujenzi wa soko la samaki au mwalo katika eneo hilo leo -
Labels:
KITAIFA,
National News