Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika
mkutano ulioandaliwa rasmi kuwaambia wananchi wa Mponde, Halmashauri ya Wilaya
ya Bumburi, Lushoto mkoani Tanga, kuwa
Rais Jakaya Kikwete amekubali kukirudisha Kiwanda cha Chai cha Mponde kwa wananchi baada ya mgogoro dhidi mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mula uliodumu kwa takribani miaka 10 na kusababisha kiwanda hicho kufungwa maiaka miwili iliyopita na kuwaacha wananchi kwenye lindi kubwa la umasikini.
Hayo ni Mafanikio ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman. Kinana
ambaye katika mkutano wa hadhara uliofanyika Septemba mwaka jana katika Kijiji
cha Mponde, aliahidi kupata suluhu ya mgogoro wa kiwanda hicho ulioshindikana
kutatuliwa kwa muda mrefu kwa kuupeleka kujadiliwa katika Kamati Kuu ya CCM na kupata
ufumbuzi ndani ya mwezi mmoja, ahadi ambayo aliitimiza.
Kiwanda hicho kilifungwa baada ya wananchi kususia kuendelea
kulima mashamba ya chai kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutatua haraka
mgogoro dhidi ya Mwekezaji wa kiwanda hicho, Yusufu Mulla, ambaye walidai kuwa
alikuwa anawanyanyasa wakulima wa zao hilo pamoja na wafanyakazi kuwalipa ujira
mdogo.
Kinana amesema Serikali itanunua hisa za mwekezaji ili
aondoke na kuwaachia wananchi kiwanda hicho.Pia Serikali itatuma jopo la
wataalamu watakao tathmini hasara iliyopo, na kutafuta mtaji wa kukifufua
kiwanda ili kianze kufanya kazi.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli,Mh. January Makamba akiishukuru
Serikali kwa uamuzi wake wa kukirudisha kiwanda hicho kwa wananchi ambapo pia
alimshukuru Rais Jakaya Kiwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman kwa kufanya
jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata haki yao hiyo walioisotea kwa
takribani miaka 10.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na
Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mh. Januari Makamba wakati alipowasili jimboni humo
katika wilaya ya Lushoto, akiwa katika ziara ya siku mbili ambapo amefanya
mkutano wa hadhara katika kata ya Mponde na kuwataarifu wananchi na wakulima wa
Chai kuhusu maagizo ya Rais Jakaya Kikwete juu ya kukirejesha kiwanda cha Chai cha
Mponde kwa wananchi .
Baadhi ya Wananchi
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini.
Wananchi wa Bumbuli
wakifuatilia mkutano wa hadhara.
Mkutano ukiendelea
katika uwanja wa Mponde,katika Halmashauri ya Bumbuli mkoani Tanga jioni ya
leo.
Mkuu wa Wilaya ya
Lushoto,Mh.Majid Hemed akizungumza na Wananchi katika mkutano wa hadhara
uliofanyika jioni ya leo katika kijiji cha Mponde,mkoani Tanga.
Baadhi ya Wananchi
waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo wa hadhara wakisikiliza kwa makini
Mmoja wa Wananchi
akishangilia kwa namna yake mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
kutamka kuwa kiwanda cha Chai cha Mponde Rais Kikwete ameamuru kilejeshwe
mikononi mwa Wananchi na Wakulima wa Chai.
Wananchi wakifuatilia
yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Magalulla Said Magalulla akiwasalimia na kujitambulisha kwa wakazi wa
Bumbuli na Vitongoji vyake,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo
katika uwanja wa Mponde,Mkoani Tanga.
Mbunge wa Jimbo la
Lushoto na Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga,Henry Shekifu akifafanua jambo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika uwanja wa Mponde,Mkoani Tanga.