Home » » NCHI ZA AFRIKA ZATOA MSIMAMO WAO KWA IMF NA WB

NCHI ZA AFRIKA ZATOA MSIMAMO WAO KWA IMF NA WB

Written By CCMdijitali on Monday, April 20, 2015 | April 20, 2015


Akizungumza na vyombo vya habari,waziri wa fedha wa Tanzania Mhe. Saada Salum Mkuyaalisema” Sisi kama nchi tuliwasilisha nini tunaona katika utekelezaji wa mipango ya Benki.Tumeshukuru sana Benki ya Dunia kwa kuendeleza mipango ya kuweza kusaidia nchi zakiafrika ,hususan kwenye mipango ya kujenga miundo mbinu ya kiuchumi kama vile barabara,kilimo pamoja na miundo mbinu ya maji na umeme”.


“Lakini vilevile tumeonyesha wasiwasi wetu kutokana na sera ambazo Benki ya Duniaimeziweka, kama vile kuangalia sera zile za watu wa kiasili ya kiafrika, sisi tumehisi mbali ya nia nzuri na njema ya Benki hii ya Dunia, lakini inaweza kuwa ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi zetu kwa sababu sera hiyo inaweza kutumika kuigawa nchi ambayo misingi yake imekuwa ikijengwa kwa umoja kutoka uhuru”.Alisistiza Mkuya.


Hakuishia hapo aliendelea kutoa mfano kuwa “sisi watanzania tumekuwa wamoja ingawa tunalugha mbalimbali kutokana na makabila tofauti. Lakini tumekuwa pamoja kwa kipindi cha miaka 50.Kwa hiyo tumeona sera hiyo isije ikatumika kwa ajili ya kuwa kigezo cha utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini . Sisi kama wa Afrika na viongozi wa Afrika tunashirikiana kuona kuwa sera zinazowekwa hazitukwamishi”.

Hali hii ya kudai uasilia (indigenous) imeibuka zaidi katika miongo hii miwili, wakati kukiwakumejitokeza watu wanaodai kuwa wao hawatambuliki na hoja hii inaihusu hasa nchi ya Tanzania.

Mawaziri wa Fedha kutoka Afrika wamejadili mambo mbali mbali ambapo ni pamoja na masuala ya maendeleo na mahusiano yao na Benki ya Dunia.

Katika Mkutano huo wa kisheria Mkurugenzi Mtendaji ndiye ambaye amewasilisha 
maazimio ya Benki katika kipindi cha miezi sita.
Aliongeza Mkuya.

Aidha katika mkutano huo pia walizungimzia suala la Ebola. “Kwa kweli wamekubali kusaidianchi zile ambazo zimekumbwa na gonjwa hili lakini wamezitaka nchi za afrika na zenyewekushirikiana katika kupambana na gonjwa hili”.Alimalizia Mkuya.Mikutano hiyo bado inaendelea hapa mjini Washington DC. Hali ya hewa ni baridi kiasi.

Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto kwake kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mkutano wa 10 wa kisheria wa kundi la Afrika (Afrikca Group Constituency) uliokuwa ukiendelea mjini Washington DC.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Salum Mkuya akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius Likwelile kushoto wakifuatilia semina iliyokuwa ikitolewa kuhusu uimarishaji wa makazi mijini.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link