Home » » UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA KURA YA MAONI

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA NA KURA YA MAONI

Written By CCMdijitali on Monday, April 6, 2015 | April 06, 2015

Kama inavyofahamika, chini ya Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi
Sura ya 343 ya mwaka 2010, jukumu la Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni kusimamia na
kuendesha Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na
Madiwani kwa Tanzania Bara. Aidha, Sheria ya Kura ya Maoni imezipa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar jukumu la kuendesha Kura ya
Maoni kwa ajili ya kuhalalisha Katiba Inayopendekezwa. Kwa mujibu wa Katiba na
Sheria, Tume hizi huendesha shughuli zake kwa uhuru bila kuingiliwa na mamlaka
nyingine yeyote. 


Ni jambo linaloeleweka kwamba, zoezi
lolote la Uchaguzi huanzia na Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Wapiga Kura
wote wenye sifa za Kikatiba na Kisheria ya Kupiga Kura ni lazima kwanza
waandikishwe katika Daftari na kupata Kadi kama Kitambulisho kinacho thibitisha
kuwa ameandikishwa na ndicho atakachotumia kujitambulisha siku ya kupiga kura.
Hivyo, ni muhimu sana kuwa na Daftari la Wapiga Kura linaloaminika ili
kuhakikisha kuwa wote wanaopiga kura kweli ni wale tu walioandikishwa. 


Kutokana na chaguzi zilizopita, za mwaka 2010, Chaguzi Ndogo za Igunga, Arumeru Mashariki, Kalenga na Chalinze,Daftari lililokuwa linatumika limekuwa lilalamikiwa Tume imelalamikiwa sana hivyo, linahitaji kuboreshwa. 


Hivyo, Tume ilifanya tafiti za kutosha katika nchi mbalimbali ikiwemo wenzetu wa Zanzibar na tuliridhika kwa dhati kuwa, Kuboresha Daftari kwa mfumo wa BVR unafaa. Hata hivyo, kwa Tanzania mfumo huo utatumika kwa Kuandikisha Wapiga Kura tu na siyo kwa shughuli
nyingine za Mchakato wa Kupiga Kura.



Kwa kuwa kazi ya kuboresha Daftari
la Kudumu la Wapiga Kura ni ya msingi kabla ya zoezi la Kupiga Kura, Tume
wakati wote imesisitiza kuwa jukumu lake la kwanza ni kukamilisha kazi ya
Kuboresha Daftari. Mengine yatafuata baada ya hapo.


Kama inavyofahamika, zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lilizinduliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu tarehe 24 Februari, 2015 katika Halmashauri ya Mji wa Makambako, Mkoani Njombe. Zoezi
lilianza kwa kutumia vifaa 250 vya BVR vilivyokuwa vimefika nchini na ndivyo
pia vilitumika wakati wa Zoezi la Majaribio katika maeneo ya Kawe Dar es
Salaam, Kilombero Morogoro na Mlele Mkoani Katavi. 


 Pamoja na changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika matumizi ya mfumo huu, kwa ujumla zoezi limeendelea vizuri. Mwitikio wa wananchi ni mkubwa sana. Kwa mfano katika maeneo fulani ya Kata mbili tumeongeza muda ili kumaliza Uandikishaji kwa wananchi
waliojitokeza. 


Inatarajiwa kwamba, zoezi litakamilika Mkoani Njombe tarehe 18/04/2015. Hadi kipindi hiki kwa Kata ambazo Tume imeishapita, hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza Kituoni ambaye aliachwa kuandikishwa. 


Tume inawahakikishia wananchi kuwa
wakati ambapo vifaa vingine vya BVR vinaendelea kupokelewa na Tume wanachi wote
watakaojitokeza katika Mikoa mingine nchini wenye sifa wataandikishwa. Baada ya
zoezi kukamilika Mkoani Njombe, kwa tarehe zitakazo ainishwa, Tume itaendelea
na Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura katika Mikoa ya
Ruvuma, iringa, Mtwara, na Lindi. 


Kama ilivyofanyika Mkoani Njombe ni
tegemeo la Tume kuwa Mikoa inayofuata itawahamasisha wananchi kujitokeza kwa
wingi katika maeneo yao na kujiandikisha kwa tarehe zitakazotangazwa kwenye
Mikoa husika. Ni upotoshaji kwa wananchi kwamba mistari/foleni ni dalili ya
ubovu wa mfumo wa BVR badala ya kuonyesha kwamba ndiyo kukolea kwa demokrasia
nchini. 


Mara kwa mara, Tume imeulizwa
itakuwaje kama tarehe 30 April, 2015 inakaribia na Tume haijakamilisha
Uboreshaji wa Daftari. Wakati wote Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu
wananchi.
haijakamilisha Uboreshaji wa
Daftari. Wakati wote Tume imesema, ikitokea hivyo itawaarifu wananchi kwa jumla
hali itakavyokuwa.


Kwa muktadha huo leo tarehe 02/04/2015, Tume inapenda kuwaarifu wananchi kama
ifuatavyo;
i. Kwa vile kazi ya Uboreshaji Daftari la Kudumu la Mpiga Kura ni ya msingi
kabla ya Zoezi la Kupiga Kura na kutokana na uzoefu tuliopata Mkoani Njombe,
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura bado halijakamilika
Mkoani Njombe na katika Mikoa mingine. 

ii. Kwa vile zoezi la Uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura halijakamilika, Tume haitaweza kuendelea na
zoezi la upigaji wa kura ya maoni.  


Hivyo, kwa heshima na taadhima Tume
inawaarifu kuwa Zoezi lililotangazwa awali la Kura ya Maoni kufanyika

 tarehe 30
Aprili, 2015 limeahirishwa hadi tarehe itakapotangazwa na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi baada ya kushauriana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link