Home » » VILABU VYA JOGGING MKOA WA DAR ES SALAAM, VIJANA WATAKIWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

VILABU VYA JOGGING MKOA WA DAR ES SALAAM, VIJANA WATAKIWA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

Written By CCMdijitali on Monday, April 20, 2015 | April 20, 2015

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi na waratibu wa Bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika Daftari Maalum la kupiga kura mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Gonga, Karakata tayari kushiriki mchaka mchaka na vijana zaidi ya 500 kutoka vikundi mbali mbali vya wilaya ya Ilala na Temeke.

Vijana wakiwa wamekusanyika tayari kuanza kushiriki mazoezi ya jogging kwenye uwanja wa Gonga, Karakata ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana, Katikabu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (katikati) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida (kulia) wakisubiri utaratibu wa kuanza mazoezi ya mchaka mchaka (jogging) na vijana zaidi ya 500 ambapo mazoezi hayo yalibeba ujumbe wa kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura.


Kikundi mwenyeji Kaza Roho ambacho kimeandaa Bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura wakijiandaa kuongoza mchaka mchaka (jogging)ambapo ilianzia Karakata,Jet na kumalizikia kwenye viwanja vya Social, Sitaki Shari.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye fulana ya rangi ya blu bahari) akikatiza mitaa ya Karakata wakati wa kushiriki jogging iliyoandaliwa na Kikundi cha Kaza Roho.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye fulana ya rangi ya blu bahari)akishiriki mazoezi ya jogging pamoaja na viongozi wengine wa chama na serikali yalioandaliwa na kikundi cha jogging cha KazaRoho kutoka Sitaki Shari.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (mwenye kofia nyeusi) akishiriki kikamilifu kukimbia mchaka mchaka na vijana zaidi ya 500 kutoka wilaya ya Ilala na Temeke.







Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea Ndugu Makongoro Mahanga wakati wa kupokea vikundi vya vijana kwenye viwanja vya Social ,Sitaki Shari .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea bendera ya Taifa kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha jogging Kaza Roho kama ishara ya kupokea vijana wa jogging kwenye viwanja vya Social Sitaki Shari jijini Dar Es salaam.



Vijana wa Mnyama Jogging wakiingia kwenye uwanja wa Social, Sitaki Shari.
Viongozi wa Vikundi mbali mbali vya Jogging wakiongoza mazoezi katika viwanja vya Social, Sitaki Shari jijini Dar es Salaam.



Vijana wakishiriki mazoezi ya Pamoja.
 Viongozi wa Vikundi vya Jogging pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiongoza vijana kufanya mazoezi.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki pamoja na vijana kufanya mazoezi ya pamoja kwenye viwanja vya Social Sitaki Shari.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiruka kutoka jukwaani kuonyesha ukakamavu wakati wa mazoezi ya pamoja na vikundi zaidi ya 30 vya jogging kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari jijini Dar es Salaam.



Msaga Sumu akitumbuiza vijana wa mazoezi ya Jogging kwenye uwanja wa Social,Sitaki Shari.



Msanii wa siku nyingi ambaye alishawahi kuwa na kundi la Free Dogs Camp lililojuisha wasanii kama P wa Black, Nale Nale, OMG akitumbuiza kwenye bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwenye viwanja vya Social ,Sitaki Shari.

Wawakilishi wa Kikundi cha Kaza Roho Bi,Sabrina Yasin(kulia) na Herieth Noel wakisoma risala ya kikundi chao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye viwanja vya Social, Sitaki Shari jijini Dar es salaam.



Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu vijana kwenye uwanja wa Social ambao walihudhuria bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftrai la kudumu la kupiga kura.



Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa jogging walishiriki bonanza maalum la kuhimiza wananchi wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwenye viwanja vya Social,Sitaki Shari jijini Dar es salaam.



Wasanii wa Yamoto Band wakionyesha umahiri wao kwenye Bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akianza mazoezi wakati akishiriki katika bonanza la Jogging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Jogging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. 


Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gongo Gongo la Mboto kupitia Kipawa na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga ujumbe mkuu wa Bonanza hilo ulikuwa ni kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kupata haki ya kupiga kura kuliko kuwa mashabiki tu.

 Bonanza hilo la mazoezi limeshirikisha vilabu mbalimbali vya Jogging kutoka mkoa wa Dar es salaam, Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa tatu akiendelea na mazoezi wakati akishiriki Mazoezi katika bonanza la Joging lililoandaliwa na Kundi la Kaza Moyo Joging Club la Ukonga Sitakishari ili kuhamasisha vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. 

Mazoezi hayo yameanzia katika viwanja vya Gonga Gongo la Mboto kupitia Kipawa na kuishia kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga, Kutoka kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida



Wakiendelea na mazoezi hayo.



Makundi mbalimbali ya Jogging kutoka mkoa wa Dar es salaam yakishiriki katika mazoezi hayo.



Ndugu Abdulrahman Kinana akiendelea na mazoezi hayo katika maeneo ya Kipawa pamoja navijana na watoto wadogo kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ramadhan Madabida na kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Mogo George Shinga Mtambalike



Mazoezi yakiwa yamepamba moto eneo la uwanja wa Ndege




Kinana akifurahia jambo na watoto katika mazoezi hayo huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida kulia akimuangalia.



Makundi mbalimbali ya vilabu vya Jogging mkoa wa Dar es salaam yakiwasili katika viwanja vya Social Sitaki Shari Ukonga.







 Umati wa vijana kutoka Vilabu mbalimbali vya Jogging mkoa wa Dar es salaam wakiendelea na mazoezi mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Social Ukonga Sitaki Shari.


Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongoza Mazoezi hayo kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari Ukonga.





 Msanii wa musiki wa Mchiriku Maarufu kama Mkaanga Sumu akitumbuiza katika bonanza hilo.



Mratibu wa bonanza hilo Bw.Msafiri akizungumza na vijana waliojitokeza kwa wingi.




Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kulia akifurahia jambo na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi



Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinanaakizungumza na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhan Madabida.



Dogo Asley wa Yamoto Band ya Mkubwa na Wanawe akifanya vitu vyake jukwaani katika bonanza hilo.



Kundi zima la Yamoto Bandi likifunika kwa shoo kali katika bonanza hilo.




Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha na pamoja na vijana wa klabu ya Kaza Moyo Jogging Club mara baada ya kushiriki katika bonanza lao, Kulia ni Bona Kaluwa Diwani wa Kata ya Kipawa na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mogo Ndugu George Mtambalike.

Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotoa wito kwa tume ya uchaguzi kuhakikisha wanawahamasisha vijana ili kuiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link