Home » » MKUU WA WILAYA YA MOSHI,NDG NOVATUS MAKUNGA AKIPOKEA MSAADA KUTOKA KAMPUNI YA BONITE BOTTLERS LTD

MKUU WA WILAYA YA MOSHI,NDG NOVATUS MAKUNGA AKIPOKEA MSAADA KUTOKA KAMPUNI YA BONITE BOTTLERS LTD

Written By CCMdijitali on Friday, May 22, 2015 | May 22, 2015


Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa sukari kilo 750 kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Ndg Novatus Makunga kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemi chemi.

Meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers Ltd ,Christopher Loiruk akikabidhi msaada wa maji zikiwa ni  katoni 500 kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Ndg Novatus Makunga kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemi chemi.

Meneja muajiri wa Bonite Bottlers ,Joyce Sengoda akikabidhi ndoo za mafuta kwa mkuu wa wilaya ya Moshi,Ndg Novatus Makunga ambazo zimetolewa 30 kwa ajili ya waathirika wa mafuriko katika vijiji vya Mikocheni,Kilungu na Chemchem.

Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Ndg Novatus Makunga akipokea msaada wa sabuni kutoka kwa meneja masoko na mauzo wa kampuni ya Bonite Bottlers,Christopher Loiruk kwa ajili ya waathirika wa mafuriko yaliyotokea wilaya ya Moshi vijijini.

Mkuu wa wilaya ya Moshi,Ndg Novatus Makunga akipokea msaada wa unga kutoka kwa Meneja mwajiri wa kampuni ya Bonite Bottlers,Joyce Sengoda kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko.


Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Ndg Novatus Makunga akizungumza mara baada ya kupokea msaada kutoka kampuni ya Bonite Botttlers kwa ajili ya waathirika wa mafuriko.

Eneo mojawapo ambalo wakazi wake wameathirika kwa mafuriko katika kijiji cha Kilungu.

Msaada wa maji ambayo yametolewa kwa waathirika wa mafuriko katika vijiji hivyo ili kupunguza kutokea kwa maradhi ya tumbo yanayoweza kutokea kwa matumizi ya maji machafu.

 Unga wa ngano ukishushwa kwa ajili ya waathirika hao.
Unga wa ngano ukishushwa kwa ajili ya waathirika hao.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link