Katibu wa Siasa na Uenezi awataka watangaza nia kuzingatia :
Katiba ya Chama Cha Mapinduzi
Kanuni za Uongozi na maadili za CCM
Kanuni za Uchaguzi wa CCM
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akiwa na Ndg Mustapha Panju ambaye ameonyesha nia ya kuomba nafasi Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi ,baada ya kumtembelea Mwenezi wa CCM Wilaya kwa ajili kufahamu taratibu na Kanuni za Chama kuhusu Wanachama wanaotangaza nia ya kugombea nafasi mbali mbali katika Chama kwa msimu unaofuata.Picha na Idara ya Uenezi CCM Wilaya Arusha.
Aidha Katibu wa Siasa na Uenezi amemsifu mtangaza nia huyo kwa kufika Ofisini kujua taratibu na kanuni wanazotakiwa kuzingatia pindi nafasi hizi zinapotokea ,ili kujua mambo wanayopaswa kufanya na yasiyotakiwa kufanywa.