Home » » Dodoma kumekucha, matano yajulikana

Dodoma kumekucha, matano yajulikana

Written By CCMdijitali on Friday, July 10, 2015 | July 10, 2015

Kwa ufupi
Kikao cha Kamati Kuu ya chama cha mapinduzi (CC) kimemalizika hivi punde mjini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Ueneze Nape Nnauye ameshindwa kutaja majina matano ambayo yatapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC)

Habari toka MWANANCHI

1:32 Tovuti ya CCM imeyatangaza majina matano yaliyopitishwa na Kamati ya CCM (CC) kuwa ni Bernard Membe, John Magufuli, Asha-Rose Migiro, January Makamba na Amina S Ali

12:55 Kikao cha Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) kimemalizika hivi punde mjini Dodoma na Katibu wa Itikadi na Ueneze Nape Nnauye ameshindwa kutaja majina matano ambayo yatapelekwa kwenye Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC)

Badala yake amewaambia waandishi wa habari kuwa majina hayo yatatangazwa saa nne asubuhi.

Aidha kwa mujibu wa Matangazo yaliyorushwa moja kwa moja na kituo cha redio Uhuru, Sophia Simba alisikika akisema kuwa mvutano mkali ulikuwemo ndani kikao hicho na wajumbe, Adam Kimbisa, Dk Emmanuel Nchimbi na yeye mwenyewe hawakukubaliana na maamuzi ya kikao yaliyofikiwa.

10:10 Bado kikao cha Kamati Kuu (CC) kinaendelea taarifa zilizopo ni kwamba kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kimeahirishwa hadi kesho saa nne asubuhi

8:12 Kikao cha Kamati Kuu kinarudi kuendelea na kitatoa taarifa ya majina matano ambayo kwa sababu ya muda yatajadiliwa kesho na Kikao cha Halmashauri na Mkutano Mkuu utafanyika kesho mchana, Kwa mujibu wa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

7:00 Kamati Kuu ya CCM imeeenda mapumziko mafupi kwa ajili ya Kufuturu na watarejea tena majira ya saa mbili usiku.

4:30 KUMEKUCHA Dodoma, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mkutano wake wa Kamati Kuu saa chache zilizopita.

Taarifa kutoka Dodoma zinasema watu wote wameondolewa ndani ukumbi mpya wa CCM ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari ambapo hivi sasa wanasubiri taarifa hizo nje ya ukumbi huo.

Endelea kuwa nasi kwa habari zaidi kutoka Dodoma ......

 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari usiku huu nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokaa kupitisha majina matano ya wagombea Urais yatakayopelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kujadiliawa hapo saa nne asubuhi. Nape hakutaja majina ya wagombea hao waliopita kwenye tano bora, kwa kusema atataja asubuhi.

Muda mfupi baada ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari, walitoka wajumbe watatu wa Kamati Kuu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mh. Sophia Simba na Mh. Adam Kimbisa ambao walizungumza na waandishi wa habari juu ya walichokizungumza kwenye kikao hicho, ambapo wao walisema wamegomea makubaliano ya majina yaliyopitishwa kwenye kikao hicho kwa madai kwamba Kikao kimekiuka tararibu za uchujaji wa majina hayo. Kwani yalijadiliwa majina machache tu na kupitishwa kwenda tano bora, lakini nao hawakuyataja majina hayo.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link