Home » » Katibu Hamasa UVCCM Chuo Kikuu Dodoma 2013 - 2014 Bi Z. Saidi atua Ofisi za CCM Wilaya ya Arusha.

Katibu Hamasa UVCCM Chuo Kikuu Dodoma 2013 - 2014 Bi Z. Saidi atua Ofisi za CCM Wilaya ya Arusha.

Written By CCMdijitali on Thursday, July 2, 2015 | July 02, 2015

 Katibu Hamasa UVCCM Chuo Kikuu Dodoma 2013 - 2014 Bi Z. Saidi na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Mjini Ndg Jasper Kishumbua.

Katibu Hamasa UVCCM Chuo Kikuu Dodoma 2013 - 2014 Bi Z. Saidi akiwa na  Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Mjini Ndg Jasper Kishumbua leo, alipokwenda kutembelea Ofisi hizo kubadilishana uzoefu na kujufinza jinsi Chama kinavyofanya kazi katika Wilaya ya Arusha.

Hii ni kutokana na hisia kwa wananchi walioko Mikoani kuamini kuwa CCM Arusha haipo. Aidha amefurahi kuona takwimu za uingizaji wanachama, ukaaji vikao,uvaaji sare ,ni mambo yanayoonekana na WanaCCM wanavaa sare bila bughudha.

Aidha ameutaka uongozi wa Vijana kuendelea kuhamasisha vijana kujiunga na Chama, kwani fursa zipo nyingi zinazopatikana kutokana na Ilani nzuri ya Chama Cha Mapinduzi, kwani hata yeye amesoma na kumaliza Chuo Kikuuu kwa kupata mkopo toka serekalini.

katibu Mwenezi na Siasa Wilaya ya arusha Mjini pia amemshukuru kada huyo na kuahidi kuwasilisha mikakati mizuri aliyoitoa kwa Uongozi wa UVCCM na UWT Wilaya.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link