- Kamati ya Usalama na Maadili
- Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa - iliyopendekeza majina 5
- Halmashauri Kuu ya Taifa - iliyopendekeza majina 3
- Mkutano Mkuu - uliyomchgua Mgombea 1
Baadhi ya Viongozi wa Jumuiya za CCM Wilaya ya Arusha wakiwa katika mkutano wa kumsimika Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Arusha 18/08/2015
Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg Philemon Mollel akimsimika Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Karimu Mushi , akishuhudiwa na Mbunge wa Viti maalum UWT Mkoa Bi Catherine Magige, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Bi Mwajuma Rashidi. Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arsuha Ndg Martin Munisi,Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Ndg Saidi Abdul,Katibu Hamasa wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Mutu Marijani, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Meru Ndg Elirehema na kushoto kabisa ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru Bi Fatuma Ngairo.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arumeru Ndg Boniface Mungaya akisoma tamko liloandaliwa na Wenyeviti wa UVCCM na Shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Arusha, katika ukumbi wa CCM Mkoa Arusha.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arumeru Ndg Boniface Mungaya akisoma tamko liloandaliwa na Wenyeviti wa UVCCM na Shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Arusha, katika ukumbi wa CCM Mkoa Arusha.
Baadhi ya Wenyeviti wa UVCCM kutoak Wilaya mbali mbali wakitoa tamko la Wenyeviti wa UVCCM na Shirikisho la Vyuo Vikuu mkoani Arusha , katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
TAMKO
Wamesikitishwa na kitendo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Ndg Robinson Laban Meitinyiku kuudanganya umma wa Watanzania na WanaCCM kuwa amehama CCM pamoja na Wenyeviti wake wa Wilaya zote za Arusha.
Aidha vijana wa Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha wapo imara na wana hari na wataendelea kukitimkia Chama mwanzo mpaka mwisho.
Tunawapa pole kwa kwa usumbufu mlioupata kutokana na taarifa hiyo ya uongo, kwani hakuna Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya aliyehama.
walidai kuwa wanaendelea kukitumikia Chama Cha Mapinduzi katika mikakati na mipango ya kupata ushindi wa Udiwani, Ubunge pamoja na mgombea mteule wa Chama Cha Mapinduzi Dk Johhn Pombe Magufuli.
Tunaheshimu Katiba na Kanuni za CCM zilizotumika katika uteuzi wa kumpata mgombea Urais.
Tumesikitishwa na kitendo cha Mzee wetu aliyekuwa Kada wa CCM Ndg Edward Ngoyai Lowassa pamoja na kukitumikia Chama katika nafasi mbalimbali, alidiriki kupotosha UMMA wa Watanzania kuwa Chama Cha Mapinduzi kimumuonea kwa jina lake kutokuwepo kwenye tano bora.
Kuhusu Wanachama kuhama Chama Cha Mapinduzi na kwenda upinzani, wanaonekana hawajui Demokrasia na ni Wafuasi wa Mtu binafsi, Lowassa kuhama Chama nao wakamfuata kwa maslahi yao binafsi.
Kama kuna mwanachama mwingine yeyote anayehisi kuwa Edward lowassa ameonewa ni vyema akamfuata, tuheshimu kauli ya CHAMA KWANZA MTU BAADAYE"
Tunawahakikishia mkoa wa arusha uko salama kabisa na hatuyumbi.
Pia tunatoa onyo kwa wale wote wanaopotosha kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere kuwa wasipoyapata mabadiliko ndani ya CCM, Watayatafuta nnje ya CCM, si kweli ,kwani hawa hawatafuti mabadiliko kwa ajili ya Wananchi , bali wanatafuta mabadiliko nnje ya CCM kwa manufaa yao binafsi .
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi akiwatambulisha na kuwakaribisha Viongozi mbali waliohudhuria Mkutano ulioandaliwa na UVCCM Wilaya ya Arusha katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Mkoa wa Vyuo Vikuu Mkoani Arusha Ndg Ridhwani Ridhwani akiwasilisha msimamo wa Shirikisho hilo katika Mkutano wa Viongozi wa CCM na Jumuiya zake katika Wilaya ya Arusha.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Meru Ndg Elirehema akiwasilisha salaamu kutoka kwa Wanachama wa UVCCM Wilaya ya Meru na kusema kuwa Jumuiya imezidi kuimarika.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ngorongoro Ndg Telele akitoa tamko kuhusu hali ya Jumuiya katika Wilaya yake kuwa ni imara na haujaathiriwa na baadhi ya Viongozi walioasi chama.
Katibu wa Hamasa wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Mutu Marijani akikanusha uvumi unaoenezwa kuwa naye atajiunga na UKAWA.Aidha aliwaambia Wanachama hao kuwa yeye ni CCM damu damu na alikuwa CCM kuanzia tumboni kwa mama yake,
hivyo wasubiri kuisoma namba.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua akiwaeleza viongozi wa Jumuiya za CCM Wilaya ya Arusha jinsi mchakato wa kumpata mgombea Uraisi ulivyoendeshwa Dodoma .
Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Karimu Mushi , Mbunge wa Viti maalum UWT Mkoa Bi Catherine Magige,akiteta jambo na Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Bi Fatuma Tse katika mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Ndg Saidi Abdul,Katibu Hamasa wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Mutu Marijani, na aliyesimama ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Jamal Kihmji.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru au Arusha DC Bi Fatuma Ngairo katika pozi kwenye Mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Katibu wa CCM Mkoa wa arusha Ndg Alphonce Kinamhala kulia na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Bi Mwajuma Rajabu ,katika Mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Mbunge wa Viti maalum UWT Mkoa Bi Catherine Magige,akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Ndg Saidi Abdul,katika Mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Baaadhi ya Makatibu wa Jumuiya za CCM Wilaya ya Arusha kutoka kushoto ni Katibu wa WAZAZI Bi Rehema Mohamed, katikati aliyevaa sare za Chama ni Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg jamal Kimji akifuatiwa na Katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Jane Nyari, katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Katibu wa CCM Mkoa wa arusha Ndg Alphonce Kinamhala akiongea na viongozi wa Jumuiya za CCM Wilaya ya Arusha, kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya WAZAZI Taifa Ndg Daudi Felix Ntibenda akiteta jambo na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Muniss katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Katibu wa CCM Mkoa wa arusha Ndg Alphonce Kinamhala akiongea na viongozi wa Jumuiya za CCM Wilaya ya Arusha, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya WAZAZI Taifa Ndg Daudi Felix Ntibenda na kushoto ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha
Bi Mwajuma Rashidi.
Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha Ndg Martin Muniss,Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg Philemon Mollel, Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Karimu Mushi,katika Mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa
CCM Mkoa wa Arusha
Meza Kuu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya WAZAZI Taifa Ndg Daudi Felix Ntibenda (KIJIKO) akiongea katika Mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha na wengine katika meza kuu ni Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg Philemon Mollel, Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Karimu Mushi , Mbunge wa Viti maalum UWT Mkoa Bi Catherine Magige, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Ndg Saidi Abdul,Katibu Hamasa wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Mutu Marijani.
Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi mama Neema Nassoro wakiwa katika Mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Sekei Bi Akira akifurahia jambo katika Mkutano wa Viongozi wa JUMUIYA za CCM Wilaya ya Arusha katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Arusha.
Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Levolosi Bi Shida, akifuatilia jambo kwa makini.
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano .