Home » » CCM Wilaya ya Arusha ,yapata ushindi wa kishindo ktk Uchaguzi Serekali Mitaa.

CCM Wilaya ya Arusha ,yapata ushindi wa kishindo ktk Uchaguzi Serekali Mitaa.

Written By CCMdijitali on Monday, April 18, 2016 | April 18, 2016

Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Wakaazi wa Mtaa wa Makao Mapya Kata ya Sinoni, wakishangilia ushindi mara baada ya matokeo kutangazwa.

 Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Sinoni , Bi Hilda Malisa akitangaza matokeo ya Uchaguzi jana katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi ya Sinoni .
Mgombea wa Chadema Ndg Nurusindiko Kivuyo (kulia) akisikiliza matokeo katika chumba cha Uchaguzi jana 17/04/2016 wa  Mtaa wa Makao Mapya Kata ya Sinoni.

 Dolee tuuuuuu.....
 Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli,akiwapongeza Wakazi na  Wanachama wa CCM katika Ofisi ya Kata ya Sinoni,mara baada ya mgombea wa CCM kutangazwa mshindi,jana 17/04/2016
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi,akiongea na baadhi ya Wanachama wa CCM katika Ofisi ya Kata ya Sinoni ,mara baada ya mgombea wa CCM kutangazwa mshindi,jana 17/04/2016.

CHAMA Cha Mapinduzi wilaya ya Arusha Mjini kimepata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa wenyeviti wa serikali ya mtaa kwa kupata viti vitano na CHADEMA vitatu.

Uchaguzi huo ulifanyika (Jana) juzi kutokana na wenyeiti wa mitaa tisa kuhamia katika vyama mbalimbali vya siasa wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka jana.

Akizungumza na UHURU ofisini kwake katibu wa CCM wilaya ya Arusha mjini Feruzi Bano alisema ushindi huo unatokana na kasi ya Rais Dk John Magufuli ya utumbuaji majipu ambayo imewakuna wananchi wengi na kuanza kuipenda CCM

Bano alitaja mitaa ambayo CCM imeshinda ni pamoja na mtaa wa Olamuriaki katika kata ya Sombetini na mtaa wa Shangarau kaya ya Moivaro ambapo katika mitaa yote hiyo CCM imepita bila kupingwa baada ya CHADEMA kushindwa kusimamisha wagombea.

Alitaja mitaa mingine ambayo CCM imeshinda ni pamoja na mtaa wa Makao mapya kata ya Sinoni,mtaa wa Bondeni kata ya Kati,mtaa wa Kilimaji kata ya Moshono.

Kwa upande wa wajumbe wa serikali za mitaa alisema CCM ilipata ushindi wa kishindo kwa kupata wajumbe watatu huku CHADEMA ikiambulia mjumbe mmoja.

Kwa mujibu wa Bano CCM ilishindwa kushinda katika mitaa hiyo mitatu kutokana na mvua kubwa iliyokuwa inayesha jijini hapa juzi hali iliyosababisha wana CCM wenye umri mkubwa kushindwa kwenda kupiga kura .

Aliongeza sababu nyingine kuwa ni karatasi za kupigia kura kutokuwa na muhuri wa Halmashauri ya Jiji pamoja na kutukuwa na vitambulisho vya kuonyesha kama kweli waliopiga kura katika mitaa hiyo walikuwa wakazi husika.

Katika uchaguzi huo kwenye kata ya Daraja mbili mtaa Sanare CCM na CHADEMA wagombea wa nafasi ya uenyekiti wa serikali ya mtaa walifungana hivyo uchaguzi huo utarudiwa tena baada ya msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mkurugenzi wa Jiji Juma Iddy kutangaza tarehe nyingine ya uchguzi
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link