Home » » Mkutano Mkuu Maalum wa UWT Wilaya ya Arusha, wampongeza Mhe. Rais Dk John P. Magufuli

Mkutano Mkuu Maalum wa UWT Wilaya ya Arusha, wampongeza Mhe. Rais Dk John P. Magufuli

Written By CCMdijitali on Friday, May 20, 2016 | May 20, 2016

  • UWT Wilaya ya Arusha yamchagua Bi Mary Kisaka kwa kura zote ndiyo 319

  • Mkt wa UWT Mkoa Bi Flora Zelote na mgeni rasmi, katika Mkutano Mkuu Maalum wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Arusha awamwagia sifa lukuki wakina mama wa Arusha.

  • Asema walioletwa CCM walishaondoka na waliobaki ni waumini wa CCM

Picha baada ya uchaguzi ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli,Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Mary Kisaka (katikati) na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Bi Flora Zelote wakiwa nnje ya ukumbi wa CCM Mkoa 19 Mei 2016.
Mwenyekiti mpya wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Mary Kisaka,aliyejizolea kura zote 319 .
Picha baada ya uchaguzi ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli,Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Mary Kisaka (katikati) na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Bi Flora Zelote wakiwa nnje ya ukumbi wa CCM Mkoa 19 Mei 2016.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Mary Kisaka akiteta jambo na Katibu wake wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Jane Nnyari (katikati) aliyesimama ni Bi Sophia (Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Wilaya akiongea jambo katika Baraza la UWT Wilaya ya Arusha mara baada ya Uchaguzi.





Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Arusha wakifanya uchaguzi wa wa kujaza nafasi.



Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Bano na msimamizi wa Uchaguzi, Bi Fatuma Ngairo Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arumeru na Katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Jane Nnyari wakiwa katika ukumbi wa CCM Mkoa Arusha katika Mkutano wa Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Arusha uliofanyika 20 Mei 2016.

Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Bano na msimamizi wa Uchaguzi (aliyesima) akitangaza matokeo ya Wajumbe waliochaguliwa 20 Mei 2016 katika Ukumbi wa CCM Mkoa akishuhudiwa na (kushoto) Mwenyekiti mpya baada ya kuchaguliwa na Mkutano Mkuu Maalum wa UWT na kulia ni Katibu wa UWT Wilaya ya Arusha Bi Jane Nnyari.

Katibu wa UWT Kata ya Levolosi Bi Aisha katika Mkutano wa Baraza la UWT Wilaya ya Arusha.

Mwenyekiti wa UWT Kata ya Sekei Bi Akira akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Arusha mara baada ya uchaguzi.


Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Wilfred Soileli na Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli Ndg Elisante Kimaro.


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Arusha mara baada ya uchaguzi .
Picha na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha , Ndg Jasper Kishumbua

Press Release ;

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Arusha wamefanya Uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Wilaya ya Arusha 19 Mei 2016 kujaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya Chama Wilaya ya Arusha Arusha kumsimamisha na yeye kuhamia  upinzani wakati wa uchaguzi Mkuu 2015.

Mgeni rasmi katika uchaguzi huo alikuwa Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Arusha Bi Flora Zelote ambaye katika hotuba yake ya ufunguzi aliwasifia Wakina Mama wa Jiji la Arusha kwa kuonyesha mshikamano na upendo na pia kutokuyumbishwa kwao na MAFURIKO.

Pia aliendelea kuwaeleza Wajumbe hao kuwa walioletwa CCM , walishaondoka na waliobaki ndiyo Wanachama sahihi wa CCM,kwani ni kweli kwamba watu wengi Arusha walikuwa na mapenzi mema na  Ndg Lowassa wakati alipokuwa Chama Cha Mapinduzi kama mtu wao na kijana wao. 
Lakini mara baada ya kuhama , mapenzi ya  Wanachama wanaokipenda  Chama Cha mapinduzi yataendelea kubaki CCM.

 Pia aliwataka Wajumbe hao kutambua kuwa heshima aliyonayo leo ,ni kutokana na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha alisema kuwa Mkutano Mkuu Maalum wa UWT Wilaya ya Arusha, unampongeza sana Mhe. Rais Dk John P. Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kupigania wanyonge walio wengi Tanzania.

Aidha aliwashukuru kwa kuwatoa kimasomaso kwenye mapokezi ya Viongozi wa Kitaifa mara wanapotembelea Mkoa huo,kupitia Vikundi vya hamasa.

MWENYEKITI WA UWT WILAYA ARUSHA - 

Bi MARY KISAKA :

Bi Mary kisaka alisema kuwa anawashukuru wanawake wa Wilaya ya Arusha waliomchagua ,kwani atawatumikia wana CCM kwa kuwapa mshikamano wa kutosha na kuhakikisha Jumuiya ya wanawake inafanya kazi kikamilifu na kuanzisha vikundi mbalimbali.

Pia aliwataka Wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi ndani ya Chama au jumuiya yoyote  na kuwasaidia wale wenye uwezo ndani ya Chama ili kuweza kuwainua wanawake.

Sanjari na hayo amewaahidi Wanawake kuhakikisha kuwa kwa utendaji kazi wake mzuri na Umoja watakaompa atahakikisha kuwa ifikapo 2020 Jimbo hili linarudi mikononi mwa Chama Cha Mapinduzi.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link