Home » » MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA 27 WA AU NCHINI RWANDA

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AMUWAKILISHA RAIS DKT MAGUFULI MKUTANO WA 27 WA AU NCHINI RWANDA

Written By CCMdijitali on Monday, July 18, 2016 | July 18, 2016


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 27 kwa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU ulioanza jana katika ukumbi wa KCC
mjini Kigali Rwanda. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo.Picha na OMR.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, Francis Gatare alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kigali, Rwanda kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika mkutano huo picha na (OMR).

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda ,Francis Gatare mara alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kigali kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na SerIkali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli Katika Mkutano huo .

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Maendeleo ya Rwanda,Francis Gatare kwenye Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kigali, Rwanda mara baada ya Kuwasili nchini humo kwa ajili ya Kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU). Makamu wa Rais anamwakilisha Rais Dkt John Magufuli katika Mkutano huo. (Picha na OMR)

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link