Home » » Shirika la Nyumba lageukia Arusha

Shirika la Nyumba lageukia Arusha

Written By CCMdijitali on Wednesday, July 27, 2016 | July 27, 2016

Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Arusha, James Kisarika


Kwa ufupi

  • Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Arusha, James Kisarika amesema mjini Arusha kuwa bei ya viwanja hivyo vitamwezesha mwananchi wa kawaida kumudu gharama. 
  •  Amesema katika mradi huo kutakuwapo na ujenzi wa nyumba mbalimbali za shughuli za kijamii ikiwamo shule, hospitali, kituo cha polisi, maeneo ya biashara na maendeleo ya viwanda vidogo vidogo.


By Happy Lazaro, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz


Arusha. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limeanza kuelekeza nguvu zake mkoani Arusha baada ya kutenga viwanja zaidi ya 600 kwa ajili ya uwekezaji na makazi.

Viwanja hivyo vipo eneo la Mateves mkoani Arusha na vitauzwa kwa wananchi.

Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Arusha, James Kisarika amesema mjini Arusha kuwa bei ya viwanja hivyo vitamwezesha mwananchi wa kawaida kumudu gharama.

Amesema katika mradi huo kutakuwapo na ujenzi wa nyumba mbalimbali za shughuli za kijamii ikiwamo shule, hospitali, kituo cha polisi, maeneo ya biashara na maendeleo ya viwanda vidogo vidogo.

“Viwanja hivi vitauzwa kwa mita moja ya mraba Sh35,000 na hatutaki udalali katika mradi huu wa Safari City lengo kubwa ni kuhakikisha kila mwananchi anamudu gharama kununua viwanja hivyo,” alisema Kisarika.

Asema Shirika limetenga Sh1 bilioni kwa ajili ya kusambaza maji katika eneo la mradi na Sh3 bilioni kutengeneza barabara.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link