Sehemu ya Mabinti wa Swaziland wakiimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokelewa na ngoma mbali mbali mjini Mbabane nchini Swaziland.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(kushoto) akizungumza na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Phiwayinkhosi Mabuza wa Swaziland ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha mara baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mfalme Mswati III.
-------------------------------------------------------
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo kwa
ajili ya kuhudhuria mkutano wa 36 wa Wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
atamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika
mkutano huo ambao utafanyika tarehe 29 Agosti 2016 ambapo Tanzania inatarajiwa kukabidhiwa nafasi ya Uenyekiti wa Jumuiya hiyo.
Mkutano huo wa 36 wa SADC ni maalum kwa
wakuu wa nchi na serikali wanaounda Kamati ya siasa,ulinzi na usalama ambao watajadili
kwa kina hali ya siasa na usalama, demokrasia na maombi ya Burundi na Comoro
kwa ajili ya kujiunga na SADC.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa
Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Augustine
Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Amina Salum Ali.
-------------------------------------------------------
-------------------------------------------------------
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage (kulia) akizungumza na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Phiwayinkhosi Mabuza wa Swaziland ambaye pia ni Kaimu Waziri wa Fedha mara baada ya kuwasili kwenye kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Mfalme Mswati III.