KAIMU KATIBU MKUU UVCCM TAIFA COMRADE Shaka Hamdu |
Asubuhi mapema taarifa na picha za kufungwa ofisi za UVCCM Mkoa wa Arusha zilisambaa katika mitandao ya kijamii.
Mwenyekiti UVCCM Mkoa Ole Sabaya |
Vijana hawamtaki katibu wa Mkoa aliyehamishwa Ezekiel Mollel ambae amegoma kuondoka akilindwa na Mwenyekiti UVCCM Mkoa Ole Sabaya
Vijana wamefunga ofisi ili Ezekiel Mollel asingie hawaridhishwa na uendeshaji wa jumuiya mkoani humo.
Kaimu katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka saa 6 mchana leo awasili Mkoani Arusha.
Afanya kikao na uongozi wa CCM Mkoani wa Arusha
Ezekiel Mollel |
Mwenyekiti wa CCM, katibu wa CCM na baadhi ya wajumbe kamati ya siasa ya Mkoa wa Arusha.
Saa 1 usiku huu Kaimu Katibu Mkuu ashuhudia makabidhiano ya ofisi baina ya Ezekiel Mollel na Said Goha.
Kutoka saa 6 mchana hadi saa 1 usiku wandishi wa habari wamejaa ofisi za CCM mkoa Arusha kutaka kauli ya Katibu Mkuu UVCCM kuhusiana na vurugu na mtafaruki huo
Saa 1 usiku Kaimu Katibu Mkuu akiwa na viongozi wa CCM mkoa wa Arusha watoka nje na kutoa neno kwa wandishi wa habari
Kaimu Katibu Mkuu asema yafuatayo:
Jumuiya ya Vijana Arusha iko salama na itaendelea kuwa salama chini ya malezi ya CCM
Jumuiya inaendeshwa kwa taratibu kanuni na miongozo1. Kanuni ya Vijana 2008 marekebisho 2012
2. Kanuni ya Utumishi ya UVCCM 2009
3. Kanuni ya Fedha
4. Kanuni ya Maadili
Jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM imemsimamisha kazi aliyekuwa Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel kwa kutotiii agizo la Makao Makuu linalomtaka kuhama na kusababisha mvutamo na malumbano yasio na tija kwa chama cha Mapinduzi mkoani Arusha.
Jumuiya imewataka vijana wa UVCCM kutambua kuwa shughuli za uendeshaji wa umoja huo zinafanyika kwa kufuata taratibu za kikanuni chini ya misingi ya nidhamu na utii.
Tarehe 25 August 2016 makao makuu ilimuandikia barua Mollel kumuhamishia Makao Makuu Dar Es Salam lakini cha ajabu kwa muda wote amekuwa akikaidi kuhama kwa sababu zake binafsi.
Kikao cha sekreterieti ya Baraza kuu UVCCM Taifa kilichoketi jijijini Dar es salaam 14 September 2016 kimeamaua kumsimamisha kazi katibu huyo na ampishe katibu wa mkoa mpya Said Goha aliyehamia Arusha akitokea lindi
Mollel amekuwa akidai kuwa Arusha kuna harufu ya ubadhirifu wa mali na miradi ya Jumuiya, Makao makuu haijapinga dai hilo , kuhama kwake si kikwazo cha kuzuia kubaini nani amehusika na tuhuma hizo, amehamishwa kwa sababu za kawaida pia kutokana na sintofahamu iliopo
Chini ya Mwenyekiti wa CCM Dkt Magufuli hakuna ubadhirifu utakaofumbiwa macho ndani ya UVCCM
Iwapo ni mpango wa kumuondoa Mollel ili kuficha ukweli wa ufujaji wa miradi, kuhama kwake hakuwezi kuzuia ukweli usijulikane, Jumuiya inaendelea kufanya uchunguzi wa miradi na rasilimali zake pia vyombo vya serikali vimeombwa viingiliie sakata hilo ili kupata ukweli wa mambo.
Mtumishi unapohamishwa toka kituo kimoja kwenda kingine na kukataa huo ni uvunjaji wa taratibu, ukiukaji wa kanuni na kutoonyesha nidhamu ya kazi Ezekiel Mollel amesimamishwa kazi hadi jambo lake litakapifikishwa katika vikao vya kitaifa vyenye mamlaka ya uteuzi wake wa mwisho kwa mujibu wa kanuni ya UVCCM.
Kwamba katibu huyo amekuwa akikaidi kuondoka kwa sababu analindwa na baadhi ya wakubwa wa makao Makuu pia makao makuu ikitaka kumlinda kiongozi mmoja wa juu asihusishwe na ubadhirifu huo, shaka alikana na kusema wanaoeneza maneno hayo ni ushabiki usio na tija.
Vijana wa Arusha wafahamu uendeshaji wa kazi za jumuiya ni uzingatiaji wa taratibu za kikanuni, makao makuu haiwezi kumkingia kifua mwizi na kumtetea , kumlinda na kumtetea mvunja taratibu husika
Kazi ya ufuatiliaji miradi, mikataba , mapato na matumizi yake yatafuatiliwa hatua kwa hatua na ukweli wa jambo hilo utaanikwaa bila mtu kulindwa na kuogopwa.
Mtu anayedaiwa kufanya hadaa na kukutwa na vitambulisho feki madai hayo ni binafsi yenye mwekeleo wa jinai na iwapo ukweli wa tuhuma hizo vyombo vya dola vitajiridhisha vinapaswa kuchukua hatua haraka UVCCM haitamlinda mtu katika jambo lolote lililo kinyume na maadili ya Chama na uvunjaji wa Katiba ya nchi.
Baadhi ya Vijana waache tabia ya kubuni au kubashiri mambo ambayo mtu hana ushahidi nayo akidai kwamba kiongozi fulani anamlinda mtu fulani wakati hakuna kiongozi makini anayeweza kumlinda mtu anayekiuka kanuni na kuvunja taratibu halali.
Chama chetu kina Katiba jumuiya yetu ina kanuni toleo la 2012 tuna kanuni ya utumishi kanuni ya fedha na maadili iyo ndio miongozo yetu katika kutekeleza majukumu ya kila siku hatutafumbia macho mtu yoyote atakaepindisha mstari mmoja wa kanuni au taratibu kwa vile hakuna aliye juu ya miongozo hiyo"
Vijana wa Arusha kuwa watulivu kwani viongozi wote wako makini katika kila jambo na jumuiya Arusha itaendelea kubaki salama.
Usiku huu baadhi ya Vijana wako na Katibu Mkuu wakimpongeza kwa umakini alionao katika kusimamia uendeshaji wa jumuiya. Wamempongeza jinsi alivyo makini kukabiliana na mambo mbali mbali kwa wakati yanapojitokeza ndani ya UVCCM.
Hawakutegema kuona Katibu mkuu akiwasili Arusha muda mfupi sana baada kuibuka mzozo huo Asubuhi ya Leo na kuusimamia hadi kumaliza Leo hii.