Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyesimama) akiongea na wananchi wa mtaa wa Kilimani kwa mama hadija kuhusu hatma ya nyumba zao zilizokuwa zibomolewe kupisha mradi wa maji.
Viongozi walioshiriki kwenye Mkutano na wananchi wa mtaa wa Kilimani kwa mama hadija, Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji Ndg. Athumani Kihamia, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo, Mwenyekiti wa Bodi ya AUWSA Dr. Laiza pamoja na Mkurugenzi wa AUWSA Eng Ruth Koya .
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Daqarro (aliyesimama) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo kutoa tamko la Serikali kwa wananchi wa mtaa wa Mlimani kwa mama Hadija
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Kilimani kwa Mama Hadija wakiskiliza tamko la Serikali kuhusu hatma yao kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha(hayupo pichani)
NTEGHENJWA HOSSEAH - ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amewafuta machozi wananchi wa mtaa wa Mlimani kwa mama hadija kwa kumaliza mgogoro uliodumu muda mrefu ambao ulilenga kubomoa nyumba zaidi ya 127 za makazi na biashara kwa wananchi wa eneo hilo ili kupisha mradi mkubwa wa maji uliopangwa kutekelezwa na Idara ya mji safi na maji taka (AUWSA).
Uamuzi huo ulitoka kwenye bodi ya maji ya AUWSA ambayo miongoni mwa wajumbe wake ni Meya wa Jiji, Mkurugenzi pamoja na Katibu tawala Mkoa wa Arusha kupitia vikao vyao vya kisheria walipitisha maamuzi ya kuweka X kwenye nyumba hizo kwa nia njema ya kutekeleza mradi mkubwa wa maji ambayo ungewasaidia wananchi wa eneo la kwa mrombo na Murieti kuondokana kabisa na changamoto kubwa ya maji waliyonayo.
Kitendo hicho chenye nia njema kililtea tafrani na sinfofahamu kwa wananchi waliojenga nyumba kwenye maeneo hayo. Kupitia kilio hicho cha wananchi Serikali ya Mkoa iliyapitia kwa kina malalamiko hayo na kutoa Tamko la Serikali la kuwataka Mamlaka zinazohusika yaani Jiji la Arusha na Mamlaka ya Maji kusitisha mara moja zoezi la bomoa bomoa na kuwataka watafute chanzo kingine cha maji ili wananchi waweze kupata maji kama Serikali ilivyokusudia.
Akizungumza na hadhara hiyo Mkuu wa Mkoa Mhe Gambo alisema zoezi la bomoa bomoa lililokuwa lifanyike katika eneo hili limesitishwa si kwa sababu hakuna Maji katika eneo hilo lakini tumethamini jasho lenu na nguvu mlizotumia kujenga nyumba hizi hivyo kwa maslahi mapana ya wananchi wetu haswa wanyonge tumeona tuliondoe eneo hili kwenye orodha ya maeneo yaliyokua yatumike kuchimba visima vya AUWSA na kwa ajili yenu tumelibakiza kwa ajili ya makazi halali na tutangalia namna nyingine ya kuwapatia maji safi ila sio kwa kubomoa hizi nyumba zenu hivyo kuanzia sasa alama za X zilizowekwa kwenye nyumba zenu zisiwazuie kuendelea na shughuli zenu za kuendeleza maeneo yenu na kuishi kwa mani.
Aidha alimuelekekeza Mkurugenzi wa Jiji kumuandikia barua Mtendaji wa Kata na Mtaa unaohusika ili kuwajulisha wananchi hao kwa maandishi kwamba Serikali imesitisha zoezi la bomoa bomoa na wananchi wabaki huru kwenye maeneo yao.
Akitoa Shukrani kwa Serikali Ndg. Iddi Ally Hindi alisema hawaamini kwamba suala hili limepatiwa ufumbuzi maana mgogoro huu umedumu kwa muda mrefu na muda wote huo wamekua wakiishi kwa mashaka kwenye nyumba zao kutokana na alama za X zilizowekwa zikimaanisha kwamba siku yeyeote nyumba hizo zingebomolewa hivyo walisubiria lolote kutokea lakini kwa kauli hii kutoka Mkuu wa Mkoa imewatia faraja na sasa wataishi kwa amani.
Aidha wananchi walitoa malalamiko yako kwa Viongozi wa Serikali kwamba wanaomba kujengewa Zahanti kwa kuwa hivi sasa wanatembea umbali mrefu kufuata huduma za Afya na aliyekuwa mmiliki wa eneo hilo Bi. Thedy James maarufu kama Mama hadija alitoa eneo la nusu heka kwa Serikali ili iweze kujenga Zahanati kwa wateja wake aliowauzia maeneo hayo ambapo kwa sasa wakazi wa eneo hilo ni zaidi ya elf elfu mbili.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Gambo alimshukuru Bi. Thedy kwa kutoa eneo hilo pia alimuagiza Mkurugenzi wa Jiji kutuma wataalamu kwenda kuangalia eneo na kuanza maandalizi ya awali kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo.
Mwisho