Home » » Mkuu wa Mkoa wa Arusha akagua ujenzi wa barabara ya Friends corner –Muriet inayojengwa kwa kiwango cha Lami

Mkuu wa Mkoa wa Arusha akagua ujenzi wa barabara ya Friends corner –Muriet inayojengwa kwa kiwango cha Lami

Written By CCMdijitali on Wednesday, October 12, 2016 | October 12, 2016

  Mkuu wa Mkoa wa Arusha (mbele kulia) akikagua ujenzi wa barabara ya Friends corner –Muriet inayojengwa kwa kiwango cha Lami kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) unaotekelezwa na Tamisemi. Barabara hiyo itajengwa kwa urefu wa Km 6.5

Kupitia Ziara hiyo pia Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisikiliza kero za wananchi wa eneo la soko Mjinga Kata ya Sokoni 1 ambapo kero kubwa ilikuwa ni kufungwa kwa barabara kutokana na ujenzi holela.


 Kutoka Kulia ni Mhandishi wa Ujenzi Jiji Eng. Gaston Gasana akifuatiwa na Mhandisi Mshauri wa Mradi wakielezea kazi zitakazofanyika katika Mradi huu.


Mkuu wa Mkoa  wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kulia) akiskiliza taarifa ya kazi zinazoendelea katika Dampo la kisasa la Muriet toka kwa Afisa Usafishaji wa Jiji Bw. James Lobikoki.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha  Mhe. Mrisho Gambo (kushoto) akihoji kuhusu zabuni za ujenzi wa barabara ya Oljoro – Muriet kwa Afisa Manunuzi wa Jiji Bw. Seif Kasori(kulia). Mkandarasi anayejenga barabara hiyo toka kampuni ya Surchet Building and Civil works yuko nyuma ya muda na ametakiwa kukamilisha kazi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.


Nteghenjwa Hosseah - Arusha
Mzabuni achunguzwa ujenzi wa Barabara  ya Oljoro - Muriet

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kuchunguza kwa undani juu ya zabuni aliyopewa
mkandarasi anaye jenga Barabara   katika barabara ya Oljoro /Murriet Jijini
hapa.

Gambo ametoa agizo hilo wakati alipokuwa katika ziara ya siku moja
 ya kukagua ujenzi wa Barabara ya Friends corner - Muriet  inayojengwa Kwa kiwango cha Lami na mradi wa Mpango Miji Mkakati ( Tanzania Strategic Cities Project)  unaotekeleza  na Tamisemi pamoja Barabara hiyo ya Oljoro - Muriet inayojengwa Kwa kiwango cha Changarawe kwa Fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.

Amesema amegundua kasoro Kwa  Kampuni  ya Surchet Building and Civil
works   inayojenga Barabara ya Oljoro  kwa kuwa Mkandarasi yuko  nyuma ya muda na  huenda asimalize kazi kwa wakati. Pia dhamana ya Utekelezaji wa Mradi aliyoweka ni kubwa kulinganisha na inayotakiwa hali hii inaonyesha kuwa   zabuni hiyo ilitolewa kwa  mianya ya rushwa au dhamana hiyo Ni feki.

Kwa kawaida Dhamana ya Utekelezaji wa Mradi ( Perfomance bond) huwa ni 10% mpaka 15% ya gharama ya Mradi lakini  mkandarasi huyu amewasilisha 30% je dhamana hiyo ni halali kweli kwanini alete kiasi kikubwa zaidi ya kinachohitajika huenda ni batili ndio maana hana uchungu nayo  na  mpaka sasa kazi iliyokamilika ni ya ujenzi wa Mifereji tu sasa kupitia ziara hii  nahitaji uchunguzi wa kina ufanyike na kazi hii ikamilike ndani ya muda wa mkataba alisema  Gambo.

Barabara ya Oljoro Muriet inajengwa Kwa urefu wa Km 2.6 sambamba na Mifereji ya kusafirishia maji yenye urefu km 1.1, Gharama Za Mradi ni Tsh Mil 157.8 na  barabara hii inategemewa kukamilika Mwishoni mwa mwezi Oktoba 2016.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link