Aliyekuwa Mbunge wa Longido Onesmo Ole Nangole (Chadema), akiwa na Mwenyekiti wa Chadema Ndg Freeman Mbowe wakiteta jambo mara baada ya kesi kusikilizwa muda wa asubuhi.
Nnje ya jengo la Mahakama Kuu Arusha leo.
Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa CCM wakiwa katika viwanja vya Makama KUU ya Arusha leo.
Diwani wa Kata ya Kimandolu Bw Rayson Ngowi,mara baada ya kupata dhamana kwa kesi ya kujimikilisha mali ya Halmashauri nnje ya utaratibu akiongea na baadhi ya waandishi wa habari
Mbunge wa Wilaya ya Monduli Ndg Kalanga akiongea na baadhi ya wafuasi wa Chadema nnje ya Jengo la Mahakama Kuu Arusha leo.
Mwenyekiti wa Chadema Ndg Freeman Mbowe akitoka Mahakamani leo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha Ndg Omari Bilali akitoka Mahakamani ,mara baada ya kesi kusikilizwa leo, akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi leo.
Mwenyekiti wa Chadema Ndg Freeman Mbowe mara baada ya kutoka Mahakamani akiongea na baadhi Viongozi wa Chadema waliofika Makamani leo.
RUFAA ya aliyekuwa Mbunge wa Longido, Mkoani Arusha, Onesmo ole Nangole (Chadema), imesikilizwa leo katika kikao cha Mahakama ya Rufaa chini ya majaji watatu kilichofanyika jijini Arusha leo.
Majaji wa Mahakama ya Rufaa waliosikiliza kesi hiyo ni Sauda Mjasiri ambaye alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho akisaidiwa na Mussa Kipenka na Ibrahimu Juma.
Nangole katika rufaa yake amepinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha uliotolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, Silvangirwa Mwangesi, Juni 29 mwaka huu ambaye alitengua ushindi wake wa ubunge wa Longido.
Alitengua ubunge huo katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi namba 36 ya mwaka jana iliyowasilishwa na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Stephen Kiruswa.
Nangole amewakilishwa na mawakili wawili waliomtetea Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha ambao ni Method Kimomogolo na John Materu na Dk Kiruswa alikuwa akitetewa na mawakili watatu Dk Masumbuko Lamwai, Edmund Ngemela na Daud Haraka.