Home » » MZEE MANGULA AFURAHISHWA 100 KUFUKUZWA UANACHAMA WA CCM MWANZA

MZEE MANGULA AFURAHISHWA 100 KUFUKUZWA UANACHAMA WA CCM MWANZA

Written By CCMdijitali on Sunday, October 23, 2016 | October 23, 2016

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula

Na Bashir Nkoromo, Mkuranga


MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula ameelezea kufurahishwa kwake
kufukuzwa kwa wanachama 100 mkoani Mwanza kwa kubainika kukisaliti chama
wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

"Haiwezekani,unajiita mwanachama, halafu badala ya kujitolea kwa nguvu zako zote
chama kishinde vita ya kushika dola, wewe unakisaliti,  hapo unakuwa si
mwanachama bali jeshi la kukodiwa",  

Mangula alisema, hayo jana, wakati
akizungumza na Vijana wanaosoma na waliohitimu vyuo vikuu 20, ambao
wameweka kambi ya kufyatua matofali kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na
nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Nasabagani, Mkuranga mkoa wa
Pwani.

 "Taarifa ya Chama kuwafukuza uanachama wale 100 kule Mwanza imenifurahisha sana,
ni matumaini yangu kwamba hatua kama hizi zitaendelea kuchukuliwa  kila
mahala nchini kote kwa waliokisaliti chama. hivi ni mchezaji gani
anayempiga ngwara mchezaji wa timu yake wakati wa mechi ya kutafuta
ubingwa halafu akaachwa kuendelea kuwa katika timu?" Mangula alisema na
kuhoji kwa mshangao.

Mangula alisema, wakati mikoa itaendelea kuchukua hatua, lakini pia kwa ngazi
ya taifa hatua dhidi ya waliokisaliti chama zitaendelea kuchukuliwa,
ikiwa ni pamoja na kuwatupilia mbali watakaojaribu kuomba nafasi za
uongozi wakati wa uchaguzi wa Chama mwakani, huku wakiwa wameshabainika
kuwa walikisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu ulipita.

Mangula aliwataka vijana nchini kote hasa wasomi, kuepuka kutumiwa vibaya na
wanachama watakaokuwa wanasaka uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa CCM
unaotarajiwa kufanyika mwakani, kwa kuwa kijana yeyote atakayekubali
kutumiwa vibaya atakuwa amekisaliti na kuchangia kunyong'onyesha nguvu
na uhai wa Chama.

"Hili la kutumiwa vibaya hasa ninyi vijana, nawaasa sana kuepuka nalo, jambo
hili ni baya sana, na si kwa Chama tu lakini hata kwa wewe uliyekubali
kutumika, maana utatumiwa kama ngazi, halafu akishapita hatakuwa na
manufaa kwako na hata kwa taifa maana atakuwa mvurugaji tu, badala ya
kushiriki kuleta maendeleo ya chama na taifa", Alisisitiza mangula.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link