Na Evelyn Mkokoi – Singida.
Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.
Akishiriki zoezi hilo Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoezi hilo.
Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.
“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.
Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki na wananchi katika zoezi la kupanda miti
mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.
Picha ⬇⬇
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipeleka uchafu katika kizimba cha uchafu cha soko kuu la Singida lililoko katika Mtaa wa Ipembe.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiandaa mche wa mti kitalam kabla ya kuupanda katika zoezi la usafi na upandaji miti mjini Singida.
Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina Akipanda Mti aina ya Mparachichi katika eneo la Misuna Stand Mpya Mjini Singida leo katika Zezi la usafi wa mazingira Kitaifa. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)