Home » » Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini

Written By CCMdijitali on Friday, April 7, 2017 | April 07, 2017


 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji kati kati aliyevaa Suti nyeusi akikiongoza Kikao cha maandilizi ya kuanzishwa mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la kutoa elimu itakayowasaidia wanafunzi kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.


Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrandwa Pili kutoka kushoto akifafanua jambo juu ya mpango huo utakaosimamiwa na UNODC.
Picha na – OMPR – ZNZ
.

 Press Release:-

Uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } umeamua kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuanzisha mafunzo maalum ya kinga ya msingi Maskulini kwa lengo la kutoa elimu itakayowasaidia kujikinga dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya.

Uongozi huo umekutana na Watendaji wa Tume ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya pamoja na wale wanaosimamia udhibiti wa uhalifu Chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim Haji Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.


Mshauri wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mapambano dhidi ya uhalifu na Dawa za kulevya { UNODC } Bibi Sylvie Bertrand alisema mpango huo wa Mafunzo utashirikisha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.


Bibi Sylvie alisema katika kuupa nguvu zaidi mpango huo ili ufanikiwe vyema Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto pia itakuwa mshirika katika mpango huo utaoratibiwa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Zanzibar.
  

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/4/2017.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link