Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan
Abbasi, leo Alhamisi Januari 20, 2022, amekagua maandalizi ya Tamasha
kubwa la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro.
Katika
Tamasha hilo litakalofanyika Jumamosi hii Januari 22, 2022, mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ambaye pia ni Chifu, akitumia jina la Chifu Hangaya.
“Maandalizi yanakamilika na tayari vikundi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huu vinaendelea na mazoezi na wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania wameendelea kuwasili hapa Moshi.
“Tamasha hili linafungua njia ya matamasha mengine ya Utamaduni wetu kuendelea hapa nchini.
Tunataka
kutumia utamaduni na sanaa kuileta dunia na kuionesha dunia kile
Tanzania ilichonacho,” amesema Dkt. Abbasi kwenye Viwanja vya Chuo cha
Ushirika Moshi.
Tamasha hilo limeandaliwa na
machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro chini ya Chifu Frank Marealle na
kuratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.