Home » » SERIKALI KUTEKELEZA ANWANI ZA MAKAZI KWA MIEZI MITANO BADALA YA MIAKA MITANO

SERIKALI KUTEKELEZA ANWANI ZA MAKAZI KWA MIEZI MITANO BADALA YA MIAKA MITANO

Written By CCMdijitali on Tuesday, January 18, 2022 | January 18, 2022

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye
akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo
wataalam wa Mkoa wa Pwani kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na
Postikodi katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa huo leo Januari 18,
2022.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye
akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo
wataalam wa Mkoa wa Pwani kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na
Postikodi katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa huo leo Januari 18,
2022.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye
akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo
wataalam wa Mkoa wa Pwani kuhusu mfumo wa anwani za Makazi na
Postikodi katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa huo leo Januari 18,
2022.

 
Mhandisi Jampyion Mbugi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari akiwasilisha mada ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mkoa wa
Pwani kuhusu mfumo wa anwani za makazi na ostikodi iliyofunguliwa na
Waziri wa Wizara hiyo, Nape Nnauye, mkoani hapo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Nickson John na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo
Zainabu Abudallah wakifuatilia maelezo kuhusu namna ya kupata postikodi
ya kata mbalimbali nchini kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa semina
ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mkoa Pwani kuhusu mfumo wa anwani
za makazi na postikodi iliyofunguliwa na Waziri wa Wizara hiyo, Nape
Nnauye, Mkoani hapo.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye
(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge,
katika hafla ya ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mkoa
wa Pwani kuhusu mfumo wa anwani za makazi na postikodi katika ukumbi
wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa huo leo Januari 18, 2022.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye
akizungumza na viongozi wa Mkoa na Wilaya za Pwani kabla ya ufunguzi wa
semina ya kuwajengea uwezo wataalam wa Mkoa huo kuhusu mfumo wa
anwani za makazi na postikodi katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa
huo leo Januari 18, 2022.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza akimuonesha Katibu wa CCM Mkoa
wa Pwani Cde, Said Yusuf Goha namna ya kupata postikodi ya kata
mbalimbali nchini kwa kutumia simu ya mkononi wakati wa semina ya
kuwajengea uwezo wataalam wa Mkoa Pwani kuhusu mfumo wa anwani za
Makazi na Postikodi iliyofunguliwa na Waziri wa Wizara hiyo, Nape Nnauye,
Mkoani hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge, akitoa salamu za Mkoa kabla
ya kumkaribisha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Nape Nnauye (hayupo pichani) kwa ajili ya kufungua semina ya kuwajengea
uwezo wataalam wa Mkoa huo kuhusu mfumo wa anwani za makazi na
postikodi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari Mhandisi Clarence Ichwekeleza akitoa taarifa kwa niaba ya Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi kabla ya ufunguzi rasmi wa semina ya
kuwajengea uwezo wataalam wa Mkoa wa Pwani kuhusu mfumo wa anwani
za makazi na postikodi uliofanywa na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape
Nnauye (hayupo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Mkoa wa
Pwani.

Prisca Ulomi na Paschal Dotto, Pwani


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa
Serikali itatekeleza uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa muda wa miezi mitano
badala ya miaka mitano kama ilivyokuwa itekelezwe hapo mwanzo kulingana na Ilani ya
Chama cha Mapinduzi Ibara ya 61(M) ya mwaka 2020 - 2025.


Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa semina ya utekelezaji mfumo huo katika Mkoa wa
Pwani, Waziri Nape alisema kuwa zoezi hilo linafanyika kutokana na misingi mitatu ikiwemo
ile ya Ilani ya CCM, Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 pamoja na Tanzania kuwa sehemu
ya dunia kwani ni mwanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Umoja wa Posta
Duniani (UPU).


“Msingi wa anwani za makazi unajengwa na msingi mitatu ikiwemo Ilani ya CCM ya 2020 -
2025, Sera ya Taifa ya Posta ya mwaka 2003 pamoja na Tanzania kuwa mwanachama wa
Umoja wa Posta Afrika (PAPU) na Umojan wa Posta Duniani (UPU), suala hili linatekelezwa
kwa miezi mitano tu badala ya miaka mitano kama Ilani inavyoelekeza, kwani itasaidia sana
katika utekelezaji wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti mwaka huu”,

amesema Waziri Nape.


Nape alisema kuwa katika utekelezaji wa zoezi hili hakuna mbadala isipokuwa ni kutekeleza
kwa nguvu zote kwani Serikali ya Awamu ya Sita inadhamiria kuwasaidia wananchi katika
kuboresha mawasiliano katika sehemu mbalimbali ikiwemo makazi yao, sehemu zao za
biashara na maeneo mengine ya huduma za kijamii.


Aidha, Waziri Nape alisema utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi ni jambo la kihistoria
ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
amedhamiria kuacha alama kwa watanzania na lengo lake ni kurahisisha mawasiliano na
kuifanya jamii kuwa ya kisasa zaidi bila kusahau kuimarisha ulinzi katika makazi yao.


Nape aliwataka viongozi wa Mkoa wa Pwani kusimamia kwa jitihada kubwa ili kurahisisha
utekelezaji wa zoezi hilo kwani Mkoa huo bado uko nyuma katika utekelezaji huku
akiwaomba uongozi wa CCM kutoka ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya tawi kuhamasisha jambo
hilo kwani ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya chama hicho ambapo wenyewe ndiyo
wasimamizi.


“Hapa hatuna kitu kingine zaidi ya utekelezaji wa zoezi hili, iwe mvua, iwe jua lazima jambo
hili litekelezwe, Pwani mko nyuma sana mna kata 3 ambazo zimetekeleza jambo hili na
nguzo 439 zimewekwa lakini bado kata 139, mahitaji yenu ni nguzo 75,392 na vibao 912,640
kwa hiyo utekelezaji wenu umefikia asilimia 1 bado asilimia 99”, amesema Waziri Nape.

 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema kuwa zoezi la
uwekeji wa anwani za makazi litarahisisha utambuzi wa maeneo ya shughuli mbalimbali za
mkoa wa Pwani yakiwemo maeneo ya viwanda.

“Anwani za Makazi na Postikodi ni mfumo mzuri ambao utatuonesha maeneo yetu
mbalimbali kama mnavyofahamu kuwa Pwani ina viwanda vingi sana kwa hiyo uwepo wa
anwani za makazi zitawarahisishia wananchi na zitarahisisha usafirishaji katika maeneo
yetu”, alisema Kunenge.


Naye, Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza alisema kuwa Sekta ya Mawasiliano ni Sekta
mtambuka ambayo inawezesha sekta nyingine kuendelea.


“Kama mnavyofahamu kwamba Sekta ya Mawasiliano ni sekta mtambuka, sekta zote
zinategemea sekta hii, kwa hiyo uwekaji wa anwani za makazi itarahisisha mawasiliano kwa
wananchi, Wizara ya Mawasiliano inashirikiana na TAMISEMI na Wizara ya Ardhi ili
kutekeleza jambo hili”, amesema Mhandisi Ichwekeleza.


Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link