Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Hamid Seif Said |
Wilaya ya Kaskazini B
Mkuu wa
wilaya ya kaskazini B Hamid Seif Said ameiagiza idara ya misitu Zanzibar
kumchukulia hatua za kisheria msimamizi wa shamba liliopo miulani
shehiya ya matetema bwana Saleh Salum Haji kwa kosa la kukata miti zaidi
ya 60 bila ya
kibali chochote kutoka serikalini
Amesema
idadi ya miti iliyokatwa ni kubwa hivyo ni vyema Kwa idara hiyo
kumchukulia hatua za kisheria mtu huyo Ili iwe fundisho kwake na Kwa
wananchi wengine
Akizungumza
mara baada ya kulikagua shamba Hilo na kukuta vigogo vya miti ambayo
tayari vimeandaliwa Kwa ajili ya kuchomwa mkaa akiwa na kamati ya ulinzi
na usalama ,watendaji wa wilaya ,watendaji wa idara ya misitu pamoja na
uongozi wa shehiya
Amesema
kumiliki shamba au kulisimamia Bado haijawa kigezo Cha mtu kukata miti
bila ya kuwa na kibali Cha misitu hivyo ameahidi kufanya Ziara za mara
Kwa mara katika mashamba yote ya wilaya ya kaskazini B Ili kubaini
waharibifu wa mazingira na kuwachikulia hatua za kisheria
Amesema
licha ya kuikosesha serikali mapato yake lakini pia kitendo hicho
kinarudisha nyuma juhudi za serikali za kutunza mazingira kutokana na
kutumia gharama kubwa katika kuzalisha miti na kuigawa Kwa wananchi wake
bila ya malipo
Hata
hivyo bwana Hamid amewataka wananchi kuacha kujichukulia maamuzi mikononi
mwao na badala yake wazingatie sheria zilizowekwa na serikali Ili
kuepuka usumbufu
Kaimu
mkurugenzi kutoka idara ya misitu said juma Ali Amesema utaratibu wa
serikali unaelekeza kuwa mmiliki wa shamba anapotaka kusafisha shamba
lake Kwa kukata miti anatakiwa kufika idara ya misitu Ili aweze
kutembelewa na kubainishiwa miti inayotakiwa kukatwa Kwa mujibu wa
sheria
Hata hivyo
amepongeza uongozi wa wilaya Kwa mashirikiano unayoyatoa Kwa idara hiyo
na kusema kuwa ushirikiano huo utasaidia Kwa kiasi kikubwa kidhibiti
vitendo Kama visiendelee kutokea na kuathiri mazingiza.
Akitoa
ufafaunuzi wa sheria kuhusu ukataji wa miti katika shamba Hilo mwana
sheria kutoka idara ya misitu Asha Muhammed Ahmed Amesema kitendo hicho
ni kinyume na sheria namba 10 ya mwaka 1996 ambayo inakataza mwananchi
yoyote kukata mti bila ya kibali kutoka serikalini
Ziara
hiyo ya kushtukiza imekuja baada ya hivi karibuni mkuu wa wilaya ya
kaskazini B kufika katika eneo Hilo Kwa ajili ya kusikiliza mgogoro wa
shamba ndipo alipokuta uharibifu huo na kuwasiliana na watendaji wa
idara ya misitu Kwa ajili ya kupata muongozo wa serikali kuhusu ukataji
wa miti Kwa mujibu wa sheria ya misitu.