Home » » NMB KANDA YA MAGHARIBI YATOA VIFAA VYA TSH 22./- MILIONI - TABORA

NMB KANDA YA MAGHARIBI YATOA VIFAA VYA TSH 22./- MILIONI - TABORA

Written By CCMdijitali on Friday, March 11, 2022 | March 11, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mh Balozi Dkt Batilda S Burian apokea madawati 150 , viti 150 na mabati 200, vyenye thamani ya Tsh.22,300,000/= kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Magharibi Ndugu Sospeter Magese wa  Kanda ya Magharibi.




Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mh Balozi Dkt Batilda S Burian

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mh Balozi Dkt Batilda S Burian apokea madawati 150 , viti 150 na mabati 200, vyenye thamani ya Tsh.22,300,000/= kutoka benki ya NMB kanda ya magharibi.

Madawati hayo yamekabidhiwa na Meneja wa kanda ya Magharibi Ndugu Sospeter Magese kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora. Shule zilizopata madawati na viti ni Mwakipanga, Ngulumwa na Kamando. Shule iliyopata mabati ni Itumba.Hafla hiyo fupi imefanyika katika Shule ya Sekondari Kamando iliyopo Mjini Igunga(tarehe 11.03.2022).

Ndugu Sospeter Magese amesema kuwa wametoa msaada huo ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link