WAGANGA WAKUU WA MIKOA
ONGEZENI KASI KATIKA MAPAMBANO
DHIDI YA MAGONJWA YA MLIPUKO
- DKT. SICHALWE
Na WAF - DSM.
MGANGA Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuongeza kasi ya ufuatiliaji (survaillence) ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ikiwemo ugonjwa wa UVIKO 19 ili kuwakinga wananchi dhidi ya magonjwa hayo katika mikoa wanayoiongoza.
Dkt. Sichalwe ametoa maelekezo hayo leo Machi 17, 2022 wakati akifunga kikao kazi cha mafunzo ya Sheria mbalimbali za afya ya jamii, ikiwemo sheria ya kitaifa ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009 na ile ya Kimataifa( International Health Regualation) ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Afya, OR-TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu katika kupambana dhidi ya magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa UVIKO-19.
Amesema, takwimu zinaonesha kuwa, zaidi ya asilimia 96% ya wagonjwa wa UVIKO-19 ni wale ambao hawajapata Chanjo ya UVIKO-19, hivyo ni wajibu wetu kama wasimamizi wa masuala ya Afya ngazi ya Mkoa kuhakikisha tunaongeza ufuatiliaji na usimamizi katika mapambano dhidi ya UVIKO-19 ili tuwakinge wananchi.
" Nyie ndio wasimamizi wa masuala ya Afya katika ngazi ya Mkoa, nitoe rai kwenu nyote kwenda kusimamia ufuatiliaji (Survaillence) ya magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19. Takwimu zipo wazi kabisa na zinaonesha kuwa zaidi ya 96% ya wagonjwa wa UVIKO-19 ni wale ambao hawajapata chanjo." Amesema Dkt. Sichalwe.
Takwimu zinaonesha Chanjo ni afua muhimu na ni salama katika mapambano dhidi ya UVIKO-19, hivyo niwatoe hofu wananchi kuendelea kuwa na imani na afua hii ili kujikinga dhidi ya maambukizi na kujikinga dhidi ya madhara ya madhara yake ikiwemo kifo, amesisitiza Dkt. Sichalwe.
Sambamba na hilo, amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa kuongeza kasi ya ukusanyaji sampuli za wagonjwa wa UVIKO-19 ili kujua hali ya maambukizi ya wagonjwa katika maeneo yao na kuwakinga mapema dhidi ya madhara yanayoweza kuzuilika.
Aidha, Dkt. Sichalwe amewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa, hasa wa Mikoa ya mipakani kuendelea kutoa Elimu ya UVIKO-19 ili wananchi waendelee kunufaika na huduma hiyo, hii ni kutokana na mwingiliano wa karibu wa wananchi katika Mikoa hiyo ya mipakani...
#AfyaKwanza