HEKO KWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KUBORESHA HUDUMA ZA MATIBABU BINGWA NA BINGWA BOBEZI NCHINI.
Bodi
ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Care for Child's Heart yenye makazi yake
nchini Marekani na Kenya wametoa salamu za pongezi na shukrani kwa
Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI) kwa kufanya upasuaji wa moyo wenye mafanikio kwa watoto sita (6)
walioletwa JKCI.
Katika barua iliyotumwa kwenda JKCI, Mkurugenzi
wa Taasisi ya Care for Child's Heart (CFACH) Bi. Irene Mukuria
ameshukuru JKCI kwa kufanya upasuaji wenye mafanikio kwa watoto 6 na
kutoa tumaini jipya la maisha kwa watoto hao.
"Kwa niaba ya CFACH napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ukarimu na huduma bora zilizotolewa kwa watoto walioletwa JKCI kwa ajili ya matibabu" amesema Bi. Mukuria.
Pongezi hizi zinakuja wakati muafaka ambapo Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Afya inaendela kuwekeza kwenye miundombinu ya kutolea huduma za afya nchini, pamoja na kuboreaha huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi na hivyo Tanzania kuwa kituo cha utalii wa tiba (medical tourism) kwa wageni kutoka nchi jirani kuja nchini kwa ajili ya kupata huduma bora za matibabu.
#KaziIendelee #AfyaKwanza #JaliAfyaYako
@ummymwalimu @dr_mollel @taasisiyamoyo_jkci