Home » » KIKAO UIMARISHAJI MPAKA TZ NA KENYA CHAANZA TARIME

KIKAO UIMARISHAJI MPAKA TZ NA KENYA CHAANZA TARIME

Written By CCMdijitali on Monday, April 11, 2022 | April 11, 2022

 

Mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Kanali Michael Mangwela akifungua kikao cha pamoja cha Wataalamu wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime tarehe 11 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Mkuu wa wilaya ya Tarime mkoani Mara Kanali Michael Mangwela  akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa mipaka wa Tanzania na Kenya wakati wa kikao cha kujadili uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya nchi hizo mbili tarehe 11 April 2022 wilayani Tarime mkoani Mara. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


Sehemu ya washiriki kutoka Tanzania. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


Mratibu Msaidizi wa Uimarishaji mpaka wa Kimataifa wa Tanzania na Kenya Joseph Ikorongo akiwasilisha taarifa wakati wa kikao cha pamoja cha wataalamu wa mipaka kutoka Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime tarehe 11 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


Ujumbe wa Tanzania na Kenya ukiwa kwenye kikao cha Pamoja cha Wataalamu wa mipaka wa nchi hizo mbili kinachoendelea wilayani Tarime tarehe 11 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Balozi Joseph Vungo akizungumza kwenye kikao cha pamoja na wataalam wa mipaka wa Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 11 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Hamdouny Mansoor (Kulia) Mkuu wa ujumbe kutoka Kenya Juster Nkoroi (Katikati) na Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya Balozi Joseph Ungo (kushoto) wakiwa kwenye kikao cha pamoja cha wataalam wa mipaka wa Tanzania na Kenya kinachoendelea wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 11 April 2022. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)


KIKAO UIMARISHAJI MPAKA TZ NA KENYA CHAANZA TARIME

 

Na Munir Shemweta, WANMM TARIME

 

Kikao cha Kamati ya pamoja ya Wataalamu wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya kimeanza leo tarehe 11 April 2022 wilayani Tarime mkoa wa Mara.

 

Kikao hicho cha Kamati ya Pamoja kati ya nchi hizo mbili kinachotarajiwa kumalizika April 15, 2022 wilayani humo kitapokea mawasilisho ya kazi iliyofanyika na kutoa muongozo juu ya namna bora ya kutekeleza kazi iliyobaki. 

 

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho wilayani Tarime mkoani Mara tarehe 11 April 2022 kwa niaba ya mkuu wa mkoa, Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mangwela alisema uimarishaji mpaka wa kimataifa baina ya Tanzania na Kenya ulenge kuimarisha mahusiano ya nchi hizo pamoja na kujadili changamoto za maeneo ya mipakani.

 

"Pamoja na kuimarishwa mipaka kati ya Tanzania na Kenya lakini bado kuna maeneo ambayo baadhi ya wananchi kutoka kila upande wanaingia na kuendesha shughuli zao hivyo mjadili changamoto hizi kwa kina na kuja na maamuzi yatakayoleta tija" alisema Kanali Mangwela.

 

Timu ya wataalamu wa Tanzania na Kenya imefanikiwa kukamilisha uimarishaji mpaka wa kimataifa wa awamu ya kwanza na kuanza awamu ya pili iliyosimama kutokana na changamoto mbalimbali.

 

Kwa upande wake mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Kenya Balozi Joseph Vungo aliwataka wataalamu wanaoshiriki kikao hicho kuhakikisha wanajadili na kuzitolea maamuzi changamoto kwa amani hasa wakizingatia nchi ya Tanzania na Kenya zimekuwa na mahusiano mazuri.

 

Kwa mujibu wa Balozi Vungo, maamuzi yoyote yatakayoamuliwa katika kikao hicho yalenge kuleta tija na kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo.

 

Zoezi la uimarishaji mpaka wa Kimataifa kati ya Tanzania na Kenya awamu ya kwanza  limeanzia hifadhi ya Serengeti / Masai Mara kipande cha Kilomita 60 hadi  eneo la Ziwa Natron kilomita 23 na awamu ya pili inaanzia Ziwa Natron hadi Namanga eneo la Kilomita 110.

 

--------------MWISHO----------------

 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link